Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Maelezo Mafupi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aliyoandika baada ya Kusoma Kitabu kuhu Chapa
05/11/2011

Kitabu hiki kwa mara nyingine kinatutia hamu kubwa ya kwenda kuzuru Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na kwenda kumzuru Mtume Muhammad SAW. Kinatupa hamu kubwa kiasi chote hiki katika hali ambayo hatuna matumaini ya kwenda huko. Kama ninavyokumbuka – tangu miaka mingi nyuma tokea ujanani – kitovu cha moyo wangu kimeshindwa kuzima joto la hamu hii kubwa. Lakini hata katika kipindi cheusi cha ukandamizaji ambacho kila mtu wa dini aliweza kirahisi kuingia katika msafara wa Hija… mimi haikuwa rahisi kwangu kufanya hivyo! Au ni vyema niseme kwamba: Msafara wowote ule au mkuu yeyote wa msafara wa Hija alikuwa hathubutu kuweka jina langu hata katika orodha ya mahujaji wake tu kutokana na kuwaogopa Savak (Shirika la Usalama wa Ndani la utawala wa kidikteta na kitaghuti wa wakati huo nchini Iran) sisemi tena Sheikh wa msafara. Naam, hata katika kipindi hicho kigumu, moyo wangu ulikuwa na matumaini ya kuweza kuizuru Alkaaba na kubusu sehemu takatifu ya Bwana Mtume Muhammad SAW huko Makkah na Madina… na licha ya kwamba katika Hija ya mwaka 1358 (mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia uliosadifiana na mwaka 1399 Hijria na 1979 Milaadia) nilipata taufiki ya kwenda kuhiji na kuzuru maeneo hayo matakatifu kwa msaada wa Shahid Mahallati, lakini joto la hamu yangu yangu hiyo liliongezeka na kuwa kali zaidi. Wakati nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu nilipata tena matumaini ya kufanya ziara hiyo tukufu baada ya kupita kipindi kirefu lakini leo…? Hamu na shauku isiyozimika imenijaa huku matumaini ya kupata taufiki hiyo yakiwa karibu yamekufa kabisa na kilichosalia ni kuliwazika kwa kusoma vitabu kama hivi vinavyozungumzia safari za Hija au kusikia maelezo ya watu waliopata taufiki ya kwenda kwenye maeneo hayo matakatifu jambo ambalo nalo linazidisha hamu na shauku yangu hiyo.

 
< Nyuma   Mbele >

^