Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Miongozo ya Kiongozi Muadhamu Alipoonana na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Chapa
12/08/2012

Ifuatayo ni matini kamili ya Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, aliyoitoa mbele ya hadhara ya mamia ya wahadhiri, wahakiki na watafiti wa Vyuo Vikuu mbali mbali vya Iran tarehe 12/08/2012

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

Ninatumia fursa hii adhimu kukukaribisheni hapa makaka na madada wapendwa na azizi. Kwa hakika kikao hiki ni kizuri mno na chenye kufurahisha sana; anga inayotawala kikao hiki nayo ni anga ya kimaanawi. Usiku wa jana ulikuwa usiku wa mwisho wa nyusiku zenye baraka tele za Laylatul Qadr (nyusiku zenye heshima na hadhi kubwa); mikono ya kuomba (dua) ilinyanyuliwa (juu), machozi yakabubujika, nyoyo zikalainika na Inshallah imepatikana akiba kubwa ya kimaanawi kwa ajili ya nchi hii, waumini na kwa ajili ya nyinyi wapendwa ambao mumehudhuria hapa. Naona ni jukumu langu kuonyesha heshima na taadhima kwenu nyinyi waheshimiwa wahadhiri kutokana na daraja ya juu ya elimu yenu na kutokana na nafasi muhimu waliyonayo wahadhiri wetu azizi katika maendeleo na ustawi wa nchi. Katika hatua ya awali, kikao hiki ni nembo ya kuonyesha heshima na taadhima kwa daraja la elimu, msomi (alimu) na mhadhiri.
Tab'an, tumestafidi na miongozo ya ndugu na kile walichokisema hapa, na nina matumaini kwamba, mzunguko wa maamuzi ya nchi utakuwa na manufaa na watu watanufaika na kustafidi nao. Nukta na mambo yaliyobainishwa hapa zilikuwa wazi, bainifu na nzuri sana na kwa hakika tunatoa shukurani zetu; lakini katika hatua ya awali dhumuni na ghaya yetu ni kuonyesha heshima na taadhima kwa elimu, msomi na alimu.
Kikao chetu cha leo kimeshuhudia mahudhurio ya familia tukufu za mashahidi wa elimu, mashahidi wa nyuklia ambapo natumia fursa hii pia kuwakaribisha familia hizi azizi; familia heshimiwa ya shahidi Ali muhammadi, shahidi Shahriyari, shahidi Ridhainejad na shahidi Ahmadiroshan; ambapo kwa hakika utajo wao katu hauwezi kusahauliwa na kumbukumbu za wananchi wa taifa hili na kumbukumbu ya historia yetu.
Katika mambo yaliyozungumzwa na ndugu, makaka na madada hapa, kulikuweko na nukta nzuri mno na mimi hapa nimezinakili baadhi ya nukta hizo. Kitu jumla na kiini ambacho nimekiona kimeashiriwa na ndugu hapa na ambacho wamekitilia mkazo ni kile kile kitu ambacho ndio wasi wasi wetu mkubwa na kwa hakika mimi nimefurahi kuona kwamba, harakati za kifikra katika Vyuo Vikuu hapa nchini inaelekea upande wa mambo ambayo ni wasi wasi wa kimsingi wa nchi hii. Suala la ratiba na mipango na uwekezaji katika uga wa utafiti, katika kazi za kimsingi, iwe ni sayansi ya jamii au iwe ni elimu za majaribio ambapo watu kadhaa hapa wametilia mkazo juu ya haya; mambo ambayo ni miongoni mwa wasi wasi wetu na bila shaka lazima haya yafanyiwe kazi. Mawasiliano ya viwanda na Chuo Kikuu ni miongoni mwa mambo ambayo tumekuwa tukiyausia; kuna nukta nzuri ambazo zimebainishwa katika uwanja huu; imeeleweka na kubainika kwamba, kuna kazi nzuri pia ambazo zimekwishafanyika.
Huku kuunda kikundi cha viwanda muhimu, kubainisha thamani ya kazi - ikiwa kama ni kazi - ambapo baadhi ya ndugu hapa wamelibainisha hilo, na wametoa mapendekezo na kubainisha nukta za lazima katika uga huu. Miongoni mwa mambo yaliyosemwa hapa ni suala la makala za kielimu, suala la kuchapishwa makala za kielimu katika majarida ya kielimu yenye itibari; ambapo haya nayo ni miongoni mwa mambo ambayo tumekuwa tukiyasema na kuyazungumzia sana, kwa hakika ni miongoni mwa wasi wasi wetu; hivyo kuna ulazima kwa wakurugenzi, wapangaji ratiba na waandaaji wakuu wa masuala ya kielimu hapa nchini wakae chini na kutafakari kuhusiana na masuala haya na kupata njia sahihi - ambapo baadhi yake zimetajwa hapa - kuhusiana na hili.
Kwa hakika, utekelezaji wa mipango kwa fikra aali ni miongoni mwa mambo ambayo binafsi nimekuwa nikiyatilia mkazo mno. Ukweli wa mambo ni kuwa, kile ambacho kimesemwa hapa, ni fikra nzuri mno; lakini aghalabu mambo haya yanahitaji kuweko mipango madhubuti ya utekelezaji. Miongoni mwa kazi ambazo ni lazima zifanyike katika Vyuo Vikuu ni hizi. Kwa mfano jaalieni kwamba, "Uchumi wa Kiakhlaqi" ambao umebainishwa na mmoja wa watu waliozungumza hapa; vizuri sana, fikra hii ni nzuri mno, kwa hakika ni fikra sahihi kabisa; njia za kufikia hili ni zipi; au kwa mfano katika uwanja huu huu unaohusiana na Chuo Kikuu na na viwanda ambapo katika miaka yote hii kumekuweko na mijadala na midahalo tofauti kuhusiana na haya na kwa bahati nzuri kumependekezwa mambo kuhusiana na hili, lakini pamoja na hayo kuna mapungufu; vizuri, kifanyike nini ili kuondoa mapungufu haya? Haya ni miongoni mwa mahitaji yetu.
Ninawaomba waheshimiwa wahadhiri na wanafikra watafakari na kulifanyia fikra jambo hili. Ala Kulli haal, natoa shukurani zangu za dhati kutokana na matilaba ambayo yamezungumzwa na kubainishwa na ndugu hapa. Ninashukuru sana uongozi wa Janabi Dakta Rahbar - ambaye kama kawaida ni kiongozi mstahiki - kwa hakika amefanya hima kubwa mno. Ninawaomba ndugu iwe ni wa ofisi yangu, au wa kutoka katika wizara mbalimbali, Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na vile vile wa ofisi ya Makamu wa Rais na vile vile wawakilishi ya kwamba, wazingatie na kuyafanyia kazi haya mambo yaliyobainishwa hapa na wahadhiri waheshimiwa; wakae chini na kutafakari, wakusanye nukta jumla; na wastafidi na kikao hiki kikamilifu kwa ajili ya harakati ya kusonga mbele.
Hata hivyo kile ambacho mimi ninataka kukisema - tab'an, Inshallah kama kutakuwa na muda na kupata uwezo na tawfiki ya kubainisha yale yote ambayo nimeyapanga - ni hili kwamba, hii leo hakuna mtu yoyote anayeweza kukana kwamba, ulimwengu hivi sasa umo katika hali ya kupita kuelekea katika hatua na marhala mpya; hili ni jambo ambalo bila shaka mnalishuhudia waziu kabisa. Naona hapa bora nibainishe taswira mukhtasari, kisha niulize suali na kisha nizungumzie na kutoa nasaha mbili tatu hivi kuhusiana na Vyuo Vikuu. Ulimwengu hivi sasa umo katika kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye muundo na sura mpya ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa hakika hali ya mambo duniani iko katika hali ya kubadilika na kuwa na muundo na sura mpya. Kama tunataka kupata kipindi cha mfano wa hiki ambacho ni cha karibu - kwa mfano takribani karne moja au mbili zilizopita - basi kipindi hiki ambacho ulimwengu umo ndani yake hivi sasa, kinaweza katika sura yake ya dhahiri, kufananishwa na kipindi cha baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia na kile kipindi cha kujitokeza ukoloni wa nchi za Ulaya.
Katika kipindi hicho kulikuwa na hali kama hii mpya ulimwenguni. Mabadiliko ambayo leo yanashuhudiwa duniani ni ya namna hii; ni aina ya mabadiliko jumla; taba'an, muelekeo yanakoelekea mabadiliko ya baadaye duniani ni tofauti na ule wa kipindi hicho, bali muelekeo wa kipindi hiki ni wa kubadilishana nguvu na uwezo wa sehemu fulani ya mataifa ya dunia kwenda kwa mataifa mengine; yaani mabadilishano ya nguvu na uwezo jumla baina ya Mashariki na Magharibi, au baina ya mataifa fulani ya dunia na sehemu nyingine ya ulimwengu. Ni wazi kwamba, tunaelekea katika mabadiliko mapya. Ushahidi na ishara za mabadiliko haya ni vitu gani? hapa mimi nitaashiria mifano kadhaa.
Mosi, mwamko wa Kiislamu. Kwa hakika katika kipindi chote cha historia yetu, hatujawahi kushuhudia hali kama hii katika nchi za Kiislamu. Kujitokeza hisia za kujijua na kujitambua mataifa mbali mbali ya Kiislamu, sio katika taifa moja, bali katika nchi kadhaa za Kiislamu na hii hisia ya mwamko, kupitia mwamko uliosimama juu ya mafundisho ya Kiislamu, ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa mfano wake katika historia, hili ni jambo la leo; na jambo hilo linabashiri wazi kutokea mageuzi na mabadiliko makubwa katika muundo ujao wa ulimwengu.
Kwani Waislamu wanaunda idadi ya watu bilioni moja na nusu ya watu duniani, makumi ya nchi duniani akthari ya watu wake ni Waislamu na nchi nazo ziko katika mazingira nyeti, kwa hivyo mwamko huu sio jambo la kawaida; jambo hili linaonyesha kutokea mageuzi na mabadiliko makubwa katika muundo ujao wa ulimwengu.
Kushindwa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kulidhibiti eneo la magharibi mwa Asia ni ushahidi mwingine wa kipindi cha hivi sasa cha mageuzi. Kushindwa vibaya Marekani kulidhibiti eneo hili muhimu na nyeti ikiwa ni pamoja na kadhia za Iraq na Afghanistan ni jambo lililo wazi kabisa, na hiyo ni ishara nyingine ya kutokea mabadiliko makubwa duniani leo hii. Matukio yanayoendelea katika kona mbali mbali za Ulaya na kiza kikubwa kilichogubika mustakbali wa nchi zenye nguvu za bara hilo ni ushahidi mwingine wa kuthibitisha kuwa dunia imo katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye muundo na sura mpya. Kwa hakika Wamagharibi waliandaa mipango madhubuti kwa ajili ya kutekeleza haya; lengo likiwa ni Magharibi kuwa na satwa na udhibiti kamili wa eneo lote hili kwa uongozi wa Marekani.
Tab'an, mimi ninasisitiza kwamba, eneo hili liitwe "Asia ya Magharibi" na sio Mashariki ya Kati. Majina ya Mashariki ya Mbali, Mashariki ya Karibu na Mashariki ya Kati sio sahihi (kwa mtazamo wangu). Wanaposema Mashariki ya Mbali, wanakusudia Mbali kutoka wapi? Kutoka Ulaya. Wanaposema Mashariki ya Karibu, wanakusudia karibu na wapi? Na Ulaya. Yaani kitovu cha dunia ni Ulaya; kila mahala ambapo ni mbali na Ulaya, jina lake ni Mashariki ya Mbali; kila mahala ambapo ni karibu zaidi na Ulaya jina la lake ni Mashariki ya Karibu, kila mahala ambapo ni katikati, ni Mashariki ya Kati! Hii ni maana na fasili ambayo imewekwa na watu wa Ulaya (wazungu); hapana, sisi hatulikubali hili. Asia ni bara moja; bara hilo lina mashariki, magharibi na katikati; sisi tupo Asia ya Magharibi. Kwa hivyo, basi eneo letu ni eneo la magharibi mwa Asia na ni sio Mashariki ya Kati. Kwa msingi huo hii ni ishara nyingine ya udhibiti, udhibiti na satwa kamili kwa eneo hili nyeti.
Kwa nini eneo hili ni nyeti? Kwa sababu mosi, eneo hili lina vyanzo nyingi na vikubwa vya utajiri; maliasili ambazo Wamagharibi wanazihitajia na katika hatua ya awali kabisa, wanahitaji hii nishati inayopatikana katika eneo hili. Pili, katika eneo hili daima kumekuweko na matarajio ya wimbi la Kiislamu; hususan baada ya kutokea Mapinduzi ya Kiislamu na (kuundwa) Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, wimbi hili daima limekuwa likitarajiwa kwa namna tata zaidi; na ndio maana wamekuwa wakifanya kila wawezalo kulidhibiti eneo hili.
Kwa msingi huo jitihada za kuwa na satwa na udhibiti zinafanyika kwa lengo la kudhibiti utajiri na wakati huo huo kuwa na satwa kwa wimbi la Kiislamu. Na ndio maana Wamagharibi wamejitayarisha ili wawe na satwa kwa eneo hili; hata hivyo wamekwama katikati ya njia; kama ambavyo mtu amejitayarisha na kuchukua kasi kwa ajili ya kuvuka kitu au kizingiti fulani, lakini anaishiwa nguvu na hivyo kukwama katikati. Hivyo kumetokea kitu kama hiki. Hili lenyewe ni ishara ya mabadiliko.
Kwa hakika matukio yanayoendelea katika kona mbali mbali za Ulaya na kiza kikubwa kilichogubika mustakbali wa nchi zenye nguvu na utajiri za Ulaya na nchi za magharibi mwa Ulaya ni ushahidi mwingine wa kudhibitisha kuwa dunia imo katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye muundo na sura mpya. Kwa hakika hali ya mgogoro wa kiuchumi inayolikabili Bara la Ulaya hivi sasa ambayo hatimaye italipiga chini bara hilo, haitokani na mikakati ya mbinu stadi za kiistratijia bali inatokana na makosa makubwa ya kimsingi yaliyofanywa na nchi za bara hilo katika suala zima la kuyaangalia na kuyapima matukio ya dunia. Tab'an, makosa kama haya, sio kama makosa ya kiistratijia, taathira yake sio ya kasi; sio kama makosa ya mikakati, taathira yake sio ya muda mchache; taathira ya makosa yake ni ya muda mrefu.
Makosa haya yanaanza kujionyesha na kujidhihirisha yenyewe baada ya karne mbili tatu na tambueni kwamba, makosa haya yatatoa pigo na kuliangusha chini bara la Ulaya. Ishara na ushahidi mwingine unaothibitisha kwamba, dunia hivi sasa imo katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye sura na mazingira mapya, ni kufeli na kupoteza itibari na heshima yake Marekani duniani hii leo. Kwa hakika kwa miongo mingi Marekani ilikuwa na heshima na itibari nzuri mbele ya walimwengu kutokana na kuwa kwake dola kuu katika upande wa elimu, utajiri, sayansi na teknolojia ya kijeshi na isiyo ya kijeshi na kuifanya kuwa na satwa; lakini hivi sasa nchi hiyo imepoteza heshima kabisa.
Itibari hiyo ya Marekani ilifikia kilele katika muongo wa kwanza wa nusu ya pili ya karne ya ishirini. Katika Iran hali ilikuwa hivi; serikali ya kitaifa kama ya Musaddiq ambayo ilikuwa ikikimbia kutoka katika satwa ya Uingereza, ilikuwa ikinasa katika mtego wa Marekani; hii ndio hali iliyokuwako katika zama hizo. Hali hii ilikuwa hivi katika kila kona ya dunia. Hii leo itibari hii ya Marekani imepotea kikamilifu na kuyeyuka; yaani hii leo Marekani ni mtuhumiwa duniani. Hii leo Marekani haina itibari katika nchi yoyote ile, na katika taifa lolote lile. Kwa hakika nara na kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani" sio miongoni mwa kaulimbiu ambazo ni maalumu na makhsusi tu kwa taifa la Iran; la hasha, bali nara hii leo imekuwa ikipigwa katika nchi nyingi.
Hii leo Marekani inatambuliwa na kuonekana mbele ya macho ya walimwengu kuwa ni nembo ya dhulma, ubeberu, mabavu, kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine na kueneza vita katika sehemu mbalimbali duniani. Kwa hivyo, hivi ndivyo inavyoonekana Marekani katika kila kona ya dunia. Kwa hakika huu nao ni ushahidi na ishara nyingine ya kuweko mabadiliko na mageuzi duniani. Kwa msingi huo, mabadiliko katika kiwango cha dunia ni jambo ambalo halina shaka tena. Kuna ushahidi na ishara nyingine nyingi, lakini hapa mimi ninatosheka na mifano hii. Hii ni nukta moja.
Amma, nukta ya pili ni hii kwamba, haiwezekani kukana kwamba, nchi na taifa la Iran lina nafasi muhimu na nyeti katika kipindi hiki (cha mpito) na katika kisa hiki kirefu. Kwa hakika sisi sio watazamaji tu katika kadhia hii, sio watu ambao tuko pembeni; kwa hakika nchi yetu ina nafasi muhimu mno katika kadhia hii. Nafasi hii muhimu chimbuko lake ni nini?
Kwanza kabisa ni kuwa, mwamko wa Kiislamu umeanzia hapa. Hili ni jambo ambalo linasemwa na wote, watu wote wanalielewa na kulifahamu vyema kabisa. Hili ambalo leo sisi tunalisema kuwa ni mwamko wa Kiislamu, lilianzia katika nchi hii miaka kadhaa iliyopita, ukachukua wahanga wake, ukaonyesha mapambano yake na ukafanikiwa kufikia malengo yake ambayo ni kuundwa mfumo wa Kiislamu. Kwa hakika, mwamko uliojitokeza hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu ni katika matunda ya Mapinduzi ya Kiislamu (nchini Iran) na kusimama imara na kidete kwa namna ya kupigiwa mfano mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Pili, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika nchi yetu ni imara na madhubuti na umejengeka juu ya misingi yake ya kiitikadi, kiimani, kiakili, na kihisia na bila shaka mambo hayo ndiyo yanayoifanya Iran iwe na nafasi muhimu, ya kipekee na isiyo na kifani katika matukio yanayoendelea hivi sasa duniani. Inshallah kama fursa itakuweko nitaashiria baadhi ya misingi hiyo ya kiakili na kihisia. Kwa hivyo kumejitokeza jengo imara kama hili ambapo kwa hakika mimi sina mfano wa hili kwa sasa hapa duniani; kwa hakika huu ni mfumo (Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu) ambao unategemea imani na wakati huo huo misingi ya kiitikadi na vile vile misingi ya kiakili na ile ya kihisia.
Tatu, sehemu kubwa ya utajiri huu nilioutaja ambao nimesema Wamagharibi wanaukodolea macho na kuumezea mate na kwa miaka mia moja wamekuwa wakiutamani - yaani nishati, mafuta na gesi - unapatikana katika ardhi yetu. Utajiri na vyanzo adhimu vya neema za Mwenyezi Mungu nchini Iran vikiwemo vyanzo vya nishati na nguvukazi yenye vipaji vya hali ya juu ni mambo ambayo yanaipa Iran nafasi ya kipekee katika mabadiliko na mageuzi makubwa yanayoshuhudiwa duniani leo hii.
Kuna wakati miaka kadhaa iliyopita tukiwa katika Husseiniya hii hii, nilibainisha kwa mapana na marefu kuhusiana na takwimu ambapo sisi tunaunda takribani asilimia moja ya watu duniani; lakini tunamiliki zaidi ya asilimia moja ya vyanzo muhimu na vya kimsingi vya utajiri ambavyo ni mahitajio ya maisha ya leo ya mwanadamu. Mbali na mafuta sisi tuna madini muhimu na nyeti ambayo ni takribani asilimia mbili, tatu, tano mpaka saba. Fauka ya hayo, tuna nguvukazi na vipaji vya hali ya juu katika nchi yetu. Kwa hakika katika nchi yetu kuna vipaji vya hali ya juu; ambavyo viko juu ya kiwango cha kati katika dunia.
Hivyo basi sisi ni nchi ambayo ina utajiri wa mali na utajiri wa nguvukazi tena ambayo inahitajiwa na Magharibi. Leo hii si tunaona jinsi Wamagharibi wanavyowafuata vijana wetu wenye vipawa, vipawa vinavyoko hapa nchini; wamekuwa wakiwafuata wahadhiri wetu mmoja mmoja, wanachuo wetu ili wawajue na kuwafahamu wale ambao wana vipaji ili wawachukue na kuwapeleka katika nchi zao. Sisi tuna udhaifu na mapungufu ambapo wao kwa hakika wamekuwa wakitumia udhaifu na mapungufu yetu haya na wamekuwa wakifanikiwa. Vyovyote itakavyokuwa, hii ni ishara na dalili kwamba, hapa kuna utajiri; hii nayo ni engo nyingine ya Wamagharibi kuwa na unyeti maalumu na nchi yetu katika matukio na mabadiliko haya yanayotokea katika kona mbalimbali duniani hii leo.
Nne, mkabala na ugumba na utasa wa Magharibi katika kuzalisha na kumpatia mwanadamu fikra na aidiolojia - ambapo baada ya Humanism (elimu ya ubinaadamu inayohusu binadamu kwanza na mahitaji yake kuliko misingi ya dini, mapote yanayoegemea humanism na falsafa iliyozaliwa kutokana na fikra hizo za humanism ya Magharibi) Magharibi haijaweza tena kuzalisha na kuleta fikra mpya kwa ajili ya mwanaadamu na maisha ya mwanadamu - Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina fikra, aidiolojia na maneno mengi mapya na yenye faida kwa jamii ya mwanadamu. Kwa hakika sina tuna maneno mapya katika masuala mbali mbali ya kisiasa, kiroho, kiserikali, kimaadili, kiutamaduni, kijamii na kiuchumi. Maneno mapya haina maana kwamba, yanaposemwa, dunia yote (lazima) itayakubali; maana yake ni hii kwamba, kumejitokeza harakati mpya katika ziwa kubwa la fikra za mwanadamu; ambayo inaleta mawimbi.
Kwa hakika hii leo masuala kama demokrasia ya kidini, ustaarabu uliojengeka juu ya umaanawi na kuchanganyika vizuri dini na maisha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya mwanadamu ni miongoni mwa fikra na aidiolojia mpya ambazo taifa la Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu imeonyesha mifano yake kwa walimwengu. Yaani haya ni mambo mapya ambayo yameletwa na taifa la Iran na mfumo wake wa Jamhuri ya Kiislamu. Haya ni mambo ambayo hayakuwahi kuweko duniani; hata katika kipindi cha umaada na humanism (elimu ya ubinaadamu inayohusu binadamu kwanza na mahitaji yake kuliko misingi ya dini) ya Magharibi na kuja fikra za kisekula hali haikuwa hivi kwamba, dini ichanganyike na maisha; hasha wakala. Ndio katika sehemu fulani ya dunia kulikuweko na utawala wa viongozi wa dini; utawala wa kanisa.
Sasa kutokana na historia tata na ndefu iliyonayo Ulaya, kulikuweko na vita baina ya vyombo vya kanisa na utawala; ala kulli haal, vyombo vya kanisa navyo vilikuwa na utawala. Hii haina maana kwamba, maisha ya watu yalikuwa yamechanganyika na dini; dini ni chimbuko la sheria na kanuni za maisha ya mwanadamu; hakukuweko kabisa kitu kama hiki katika ulimwengu wa Magharibi; na katika nchi za Kiislamu pia, hakukuweko na kitu kama hiki; isipokuwa mwanzoni mwa Uislamu. Haya ni maneno mapya ambayo sisi tunayaleta na tunasema kwamba, dini na maisha ni kitu kimoja. Maisha ni nini? Maisha maana yake ni siasa, harakati, biashara, uchumi na vitu vyote; haya ni maneno mapya ambayo yanasemwa.
Nukta ya tano na sababu ambayo inaifanya nchi hii (Iran) kuwa na nafasi maalumu na ya kipekee ni kusimama kidete na imara mkabala na mbinu za kuendelea za Magharibi katika kusukuma mbele gurudumu la kazi zake. Katika kipindi chote hiki ambacho Magharibi imekuwa na uongozi na satwa katika siasa za dunia, kumetumika mbinu mbalimbali; viongozi wa Magharibi wamekuwa wakitoa vitisho, wamekuwa wakipiga ngoma ya vita, wakifanya ugaidi, wanafanya mauaji na kuzusha fakachi na hitilafu. Hizi ni mbinu maarufu na za wazi za Wamagharibi ambazo sasa zinatambulika na kufahamika na zimekuweko katika kipindi chote cha satwa yao ya miaka mia mbili au mia tatu hivi. Iran, watu wake, vigogo wake na viongozi wake wamesimama imara mbele ya vitisho, vita, ugaidi, mauaji na njama za Magharibi za kuzusha hitilafu katika safu za Wairani, na bila shaka uhakika huo nao unaipa sifa za kipekee nchi na taifa hili kubwa (la Kiislamu).
Vitisho vya Wamagharibi havijakuwa na taathira, njama zao za kuzusha hitlafu hazijazaa matunda - suala la kuzusha hitilafu ni muhimu mno - na hazijaweza kushinda harakati jumla ya taifa la Iran. Kwa hivyo basi haya ni mambo ambayo yanaifanya nchi yetu ya Iran kuwa na nafasi maalumu na ya kiekee. Kwa muktadha huo basi, hii hali iliyoko duniani inaonyesha kwamba, dunia inakaribia kupata mabadailiko au iko katika hali ya mabadiliko na hili ni jambo ambalo halikanushiki hata kidogo; nafasi maalumu ya nchi yetu nayo haiwezi kukanushika. Sasa hapa kuna swali linalojitokeza.
Swali lenyewe ni je Vyuo Vikuu na Hawza (Vyuo Vikuu vya Kidini), vina jukumu lolote katika matukio haya muhimu mno au havina? Mimi ninawataka waheshimiwa wahadhiri, wasomi wapendwa, watu wenye vipawa vikubwa nchini muwe makini katika jambo hili. Je Hawza za kidini na Vyuo Vikuu havina jukumu lolote na hivyo vinaweza kuwa watazamaji tu katika matukio haya muhimu bila ya kutoa mchango wowote? Seuze kwa mfano (Mwenyezi Mungu aepushie mbali) vitake kuunga mkono kambi ambayo imesimama dhidi ya kambi ya haki. Kile ambacho kwa uoni na mtazamo wangu ni cha lazima ni hiki kwamba, masuuliya na majukumu ya Vyuo Vikuu na Hawza (Vyuo Vikuu vya Kidini) katika mazingira haya ni mazito mno.
Jukumu la kuliwafikisha na kuliwezesha taifa la Iran kutoa mchango unaostahiki katika kipindi hiki muhimu mno cha historia liko juu ya mabega ya wasomi nchini kabla ya kuwa kwa mtu mwingine yoyote na kwa yakini Vyuo Vikuu ni miongoni mwa vituo vya daraja la kwanza kabisa vya kuweza kutoa taathira yake katika mabadiliko hayo. Na kama hatutasema kwamba, wao ndio wako katika daraja la kwanza, basi bila shaka wao (watu wa Vyuo Vikuu) wako mstari wa mbele katika kuwa na taathira katika matukio na mabadiliko haya.
Chuo Kikuu kinaweza kufanya mambo ambayo yataifanya nchi, taifa na historia yetu ishinde katika matukio na mabadiliko haya; kinaweza pia (Mwenyezi Mungu aepushie mbali) kikalifanya taifa hili lisishinde. Kwa uoni wangu Chuo Kikuu kina nafasi muhimu na jukumu nyeti na kubwa katika uwanja huu. Kile ambacho kimebainishwa na ndugu hapa katika hotuba na mazungumzo yao ni kazi muhimu sana na za lazima. Tab'an, maendeleo na ustawi uliopatikana ni mkubwa, na kuna nukta chanya ambazo zimebainishwa na ndugu hapa na kuna nukta hasi pia ambapo katika mazungumzo ya ndugu hapa wametosheka tu na kuashiria haya; yaani mambo hayo hayakubainishwa kwa undani zaidi.
Sisi tuna nukta hasi katika uwanja wa usimiaji masuala ya kielimu na vile vile katika uga wa mipango mbalimbali kwa mujibu wa elimu ambazo zinazalishwa katika Chuo Kikuu, katika uga wa nchi na katika uga wa jamii; hivyo kuna ulazima kwa mambo haya kupatiwa ufumbuzi. Marejeo ya kuyapatia ufumbuzi haya ni Chuo Kikuu; kwa hakika Chuo Kikuu chenyewe ndicho ambacho kinaweza kuwa na athari. Ukweli wa mambo ni huu kwamba, njia pekee ya kuweza kukabiliana na nukta hizo hasi ni Vyuo Vikuu kulipa umuhimu wa hali ya juu suala la kutumia hazina yake ya kielimu na kiutaalamu katika kukabiliana na mambo hayo hasi. Hii leo viongozi na maafisa wa serikali, mawaziri, maafisa watendaji na maafisa wengi wasio watendaji katika utungaji sheria na mahakama ni wahitimu wa Vyuo Vikuu, watu wa Vyuo Vikuu na Wajumbe wa Bodi ya Elimu.
Mawasiliano yenye umakini, muelekeo na malengo ni mambo ambayo yanaweza kusaidia kuifanya dafina na akiba ya kitaalamu ya elimu hapa nchini kuwa katika huduma ya kusahihisha kazi na kuondoa nakisi na mapungufu. Hili kwa upande mmoja ni jukumu la Vyuo Vikuu na kwa upande mwingine ni masuuliya ya maafisa na wakurugenzi ambapo leo mimi niko na nyinyi; Inshallah nitakutana na kubainisha majukumu ya wakurugenzi katika wakati na mahala pake, Inshallah tunataraji haya yatakuwa na taathira.
Yumkini hapa kukajitokeza shubha na utata - wakati mwingine hujitokeza watu na kutoa shubha na utata - huleta hali ya mkanganyo juu ya elimu kutoegemea upande wowote kwamba, bwana wewe msichanganye elimu na siasa; elimu haiegemei upande wowote! Ndio! bila shaka elimu haiegemei upande wowote katika hatua ya kugundua uhakika na ukweli; wakati elimu inapotaka kufichua uhakika wa jambo fulani miongoni mwa uhakika wa ulimwengu, iwe ni uhakika wa kimaada au usio wa kimaada bila shaka haiwezekani (kulifikia hilo) kwa kutoa hukumu kabla (yaani kuwa na uamuzi juu ya jambo hilo kabla hata ya kufanyika uchunguzi wenyewe); kwa hakika elimu katika upeo wa kutafuta mambo ya kweli na ya uhakika huwa haina upendeleo; lakini wakati elimu inapotumiwa kwa ajili ya kufanikisha malengo ya mrengo fulani kamwe haiwezi kuwa huru na wala isiyopendelea upande wowote na hilo ndilo tunalolishuhudia hivi sasa ulimwenguni.
Wale wale watu ambao wakati mwingine wanaipigia makeleke Jamhuri ya Kiislamu (ya Iran) na majimui ya watu wa Chuo Kikuu walioshikamana na dini hapa nchini kwamba, bwana we, mumeifanya elimu kuwa jambo la kisiasa, mumeifanya elimu iwe na muelekeo fulani, wao wenyewe waliiweka elimu na kuifanya kuwa inahudumia ukoloni, waliifanya elimu ikawa inahudumia madola yaliyokuwa na satwa na udhibit kwa mataifa mengine duniani na waliifanya elimu ikawa minyororo ya kuvurutia mataifa mengine. Ukoloni ulikuja kutokana na elimu; lau (wahusika) wasingelikuwa na elimu wasingweza kukoloni nchi na mataifa yote haya na wala wasingekuwa na silaha zote hizi duniani. Hivi vita vikubwa ambavyo Wamagharibi, watu wa Ulaya na kisha baadaye Marekani ambavyo wameitwisha dunia na mataifa mbalimbali ulimwenguni, watu wote hawa waliouawa katika njia hii; anzia kona ya mbali kabisa ya Asia mpaka Afrika na kisha nenda mpaka Amerika ya Latini - wamefanya nini hawa (wakoloni)? - wamefanya yote hayo kwa kutumia elimu.
Hivyo elimu imefanywa kuwa wenzo wa kuhudumia dhulma, kwa ajili ya kuhudumia ubeberu na utumiaji mabavu; kwa nini elimu haijafanywa iwe inahudumia uadilifu? Kwa nini elimu isiwekwe na kufanywa iwe inahudumia thamani na matukufu. Vipi iwe ni sahihi kwa elimu kutumikia malengo ya madola ya kibeberu na kikoloni kwa karne nyingi katika kutengeneza silaha za mauaji ya umati na halaiki ya watu na kueneza vita duniani, lakini isiwe sahihi kwa elimu kutumikia uadilifu, kudumisha na kuimarisha thamani za kibinaadamu na kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa walimwengu?
Mkanganyiko na mgongano mwengine - ambapo kwa sasa sitaki kuuzungumzia kwa mapana na marefu sana - ni kugawanywa vyombo vya kusambaza elimu katika makundi mawili ya vyombo vya kusambaza elimu vya serikali na vile visivyo vya serikali; yaani kikundi (cha elimu) cha serikali, wanachuo wa serikali na mhadhiri wa serikali haya yamezungumziwa katika njia ya kupaka matope na kama ni kitu kibaya! Mtu anaona kuwa watu wengine wanayazungumzia haya na kisha hayo kuakisiwa hapa ndani (ndani ya nchi).
Mimi ninaamini kwamba, hili sio jina baya bali hili ni jambo la fakhari kubwa kabisa. Mwanachuo ambaye anaunga mkono serikali yake na mfumo wake - utawala ambao ni mfumo ambao umesimama juu ya misingi ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu na ni mfumo wa Kiislamu - na vikundi ambavyo vinausaidia mfumo huu, mhadhiri ambaye ni msingi wa kifikra anayesaidia mfumo wa Kiislamu anapaswa kujifakharisha na hili. Kile ambacho kinampaka matope na kumfanya mtu kuwa na jina baya kikweli kweli ni mwanachuo wetu, mhadhiri wetu majimui yetu kuweko kwa ajili ya kuhudumia Marekani, kwa ajili ya kuuhudumia Uzayuni; hili ni jambo baya mno na ambalo linampaka matope mtu.
Ndio, kama mtu kama huyu atatuhumiwa kwamba, yuko kwa ajili ya kuhudumia Marekani, kwa ajili ya kuuhudumia Uzayuni, anawahudumia wapinzani wa mamlaka ya kujitawala nchi na nchi kuwa kifua mbele, kwa hakika huku kutakuwa ni jambo baya na hatua hii ni ya mtu kujitia madoa machafu kabisa; na huku ni kuwa na jina baya. Kwa hivyo basi hii kwamba, inasemwa, mwanchuo fulani ni mwanaserikali, au mhadhiri fulani ni mfuasi wa serikali au majimui fulani ni mfuasi wa serikali, sio kupakwa matope hata kidogo, hiki sio kitu kibaya; bali wahusika wanapaswa kujivunia na kujifakharisha kwa hili, serikali yaani inahusiana na mfumo.
Kuna wajibu wa kuongezewa nguvu utamaduni wa kufanya idili na jitihada za kambi ya kupigania haki katika Vyuo Vikuu ambapo tab'an, jukumu la walimu na wahadhiri wa Vyuo Vikuu katika jambo hilo ni kubwa sana. Hili nalo ni jambo ambalo linapaswa kufahamika vyema.
Miongoni mwa mambo ambayo yamezungumziwa na ndugu hapa hili ni mojawapo; utamaduni wa kimaanawi na kiakhlaqi (kimaadili) au kama alivyobainisha hapa mmoja wa ndugu waliozungumza ya kwamba, sanaa kwa maana ya uhuru, kwa maana ya kuwa kifua mbele (kupata mafanikio) kwa maana ya thamani, kwa hakika ni sahihi kabisa. Utamaduni huu unapaswa kupanuliwa katika Vyuo Vikuu. Kuhusiana na nafasi ya wahadhiri, bila shaka wahusika wana nafasi muhimu sana; na huku ni kuongoza mapambano katika vita laini jambo ambalo nimelikariri mara chungu nzima na kusema kwamba, wahadhiri ni makamanda wa vita laini. Kwa maneno mengine ni kuwa, kustawishwa na kupanuliwa utamaduni wa kufanyika idili na jitihada za kambi ya haki, kwa kweli ni sawa kabisa na kuimarisha kambi ya kuongoza mapambano katika vita laini, jukumu ambalo kwa daraja ya kwanza, linawaelekea wahadhiri wa Vyuo Vikuu.
Nasaha ya mwisho - kwani inaonekana muda nao umetupa mkono sana - ni nasaha ambayo inahusiana na suala la mfumo wa taifa wa ubunifu wa mambo mapya. Hivi sasa pengo la kutokuwepo mfumo wa taifa wa ubunifu wa mambo mapya, kitu ambacho kwa kweli ni kanali ya mawasiliano yenye mlolongo mrefu na mkubwa wa vyombo vidogo vidogo vya elimu nchini, baina ya vyombo vya kielimu vya nchi, iwe ni katika mazingira ya elimu au nje ya mazingira hayo, ni jambo ambalo linahisika vibaya sana nchini na inabidi zifikiriwe njia mwafaka za kuondoa pengo hilo. Hivyo basi kuna haja ya kuweko kitu kama hiki ambacho kitakuwa na anuani ya Mfumo wa Taifa wa Ubunifu wa Mambo Mapya; kazi yake iwe ni kusimamia harakati ya kielimu na ubunifu wa mambo mapya, ichunguze, ifanye tathmini na kuongoza haya. Hili ni jambo la lazima ambalo linahitajika leo, na kwa uoni na mtazamo wangu viongozi na maafisa (wa serikali) wanapaswa kutaamali na kulizingatia sana suala hili (la kuleta mfumo wa taifa wa ubunifu wa mambo mapya).
Ewe Mwenyezi Mungu! Kile ambacho tumekisema na ambacho tumekisikia kifanye kiwe kwa ajili Yako na katika njia Yako. Ewe Mwenyezi Mungu! Tunakuomba kwa kwa haki ya Muhammad na Aali Muhammad, utupe msaada kulingana na uwezo wetu, kulingana na nafasi yetu na kulingana na mchango wetu wa kuifanya kambi ya haki iishinde kambi ya batili. Ewe Mwenyezi Mungu! Ufanye moyo mtukufu wa Walii Asr Imam wa Zama (roho zetu ziwe fidia kwake) na roho takatifu ya Mtume wa Mwisho Muhammad saw ziwe radhi na wananchi wetu, taifa letu, wasomi wetu na wanaofanya hima na idili katika njia hii. Zifufue roho takasifu za mashahidi wetu azizi, mashahidi wa elimu na mashahidi wa sayansi ya nyuklia pamoja na mawalii Wako.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabakaatuh.

 
< Nyuma   Mbele >

^