Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika Chuo Kikuu cha Jeshi la Majini cha Imam Khomeini mjini Nowshahr Chapa
17/09/2012

Ifuatayo hapa chini ni matini kamili ya Hotuba ya Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa katika hafla ya kuapishwa na kupatiwa nishani wanachuo wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alipotembelea Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Imam Khomeini MA mjini Nowshahr tarehe 17/09/2012

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

Natoa pongezi zangu za dhati kwenu ninyi vijana azizi na maafisa wenye nishati na shauku kubwa wa vikosi vya ulinzi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ninapenda kuwapongeza pia vijana ambao leo wameingia katika njia hii na wanaanza mafunzo katika Vyo Vikuu vya Kijeshi.
Njia yenu hii imejaa fakhari; njia yenu hii ni njia ambayo inasifiwa na kila mtu mwenye dhamira huru ambaye hufanya hivyo baada ya kuiona njia hii na kuwa na ufahamu na welewa nayo; kwa hakika njia ya kutetea malengo matukufu na aali ya Kiislamu ni hitajio la lazima na la dharura kwa mwanaadamu. Nyinyi mumeingia katika njia hii tena katika sekta na uga ambao ni nyeti na wenye hatari mno. Vikosi vya ulinzi ni kiungo muhimu katika Mfumo wa Kiislamu, wa Kimwenyezi Mungu na ustaarabu wa Kimwenyezi Mungu na wa Kiislamu katika kukabiliana na maadui, wenye chuki na wasioutakia mema mfumo huu (adhimu). Vijana wetu azizi wanapita katika medani hii wakiwac na hamu, shauku, mapenzi, ufahamu na welewa wa hali ya juu na hivyo kupata fakhari za dunia pamoja na ujira (thawabu) wa Akhera na wa Mwenyezi Mungu.
Ndugu zanguni wapendwa! Hii ni njia yenye nuru na baraka tele; tambueni thamani ya (kushikamana na) njia hii; mnajishughulisha na utoaji huduma au mtajishughulisha na utoaji huduma katika sehemu yoyote ya vikosi vya ulinzi na Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu, litambueni hili kwamba, ni jambo zuri, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakupeni ujira na hivyo kuzifanya sura zenu zing'are hapa duniani na huko Akhera. Vile vile ni lazima niwapongeze na kuwataka wasichoke hawa maafisa wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na Wakurugenzi wa Chuo Kikuu hiki kutokana na hima na idili kubwa waliofanya ya kuwalea ninyi vijana. Hii leo pia ratiba katika uwanja huu nazo naona ziliambatana na ubunifu na mandhari ya kuvutia. Nakutakieni mafanikio mema Inshallah, na kila hatua moja mtakayopiga kwa ajili ya nchi na taifa hili ambalo linakuungeni mkono iwe ni hatua ya kulifanya taifa hili lisonge mbele. Kwa hakika hii leo katika nchi yetu kuna wimbi la mapenzi na shauku ya maendeleo, shauku ya kutaka kufanya harakati, ubunifu na kuleta mambo mapya. Katika kila sekta mbalimbali - katika sekta ya elimu, utaalamu, ubunifu, masuala ya kisiasa na masuala ya kijamii - watu wote wanafikiria kufanya ubinifu na kuleta mambo mapya - wanachuo wapendwa na maafisa wanajeshi vijana katika jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na katika vikosi vyote vya ulinzi - hivyo basi medani hii iko wazi. Vijana wana kipawa na nishati na uchangamfu wa ujana, wanafanya hima katika mazingira ya kielimu na vile vile mna fakhari kubwa ya kuwa katika vikosi vya ulinzi - ambapo kama alivyosema Imam Ali AS "ni husuni imara ya nchi na wananchi - nyote mko katika hali ya kutekeleza majukumu.
Kadiri siku na muda unavyopita, ndivyo thamani ya hima na juhudi katika jengo la Jamhuri ya Kiislamu na uimara wake unavyodhihirika na kuonekana zaidi. Maadui wa Uislamu na umma wa Kiislamu, wanahisi wameshindwa na kubakia nyuma katika kukabiliana na kupambana pamoja na harakati hii kubwa na yenye kuchemka na yenye kudhihiri kwa nguvu (ya mwamko wa Kiislamu); na ndio maana sasa wanafanya mambo ya kiuwendawazimu. Tukio la hivi karibuni la kuvunjia heshima sura inayong'ara ya Mtume wa mwisho Muhammad SAW (kwa kuenezwa filamu iliyotengenezwa nchini Marekani) ni miongoni mwa ibra za historia yetu na bila shaka ibra ni yenye kubakia. Wakuu wa mifumo ya kiistikbari na kibeberu wanakwepa kulaani jinai hiyo katika hali ambayo hawatekelezi pia majukumu yao ya kukabiliana na uhalifu huo mkubwa kama ambavyo pia wanadai kuwa, hawakuhusika na jinai hiyo kubwa. Sisi hatung'ang'anii suala la kuthibitisha kuhusika kwao katika jinai hiyo, bali tunachosema sisi ni kuwa sera na mbinu za kisiasa zinazotumiwa na wanasiasa wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya ndizo zinazowafanya walimwengu wawanyooshee kidole na kuwaona kuwa ndio wakosa wakuu, hivyo wanachopaswa kufanya wanasiasa hao ni kuonyesha kivitendo kuwa hawahusiki na uhalifu huo mkubwa sana na wasiishie tu kusema kwa maneno matupu. Wanapaswa kuzuia uhalifu huu; tab'ani, hawatofanya hivyo. Sababu ya hilo iko wazi nayo ni kuwa kuna misukumo katika vyombo vya waistikbari na mabeberu ya kuvunjia heshima Uislamu na matukufu yake. Kile kinachowafanya wafanye matendo kama haya ya kipunguani na kiuwendawazimu ni harakati kubwa ya mwamko wa Kiislamu. Kisha wanakuja na kutoa visingizo kwambam, wao hawawezi kuzuia hayo kutokana na kuheshimu uhuru wa kusema na kujieleza. Nani atawaamini hawa? Nani atayaaamini hayo ilhali moja ya mifano ya wazi inayothibitisha uongo wa madai hayo ya viongozi wa Magharibi ni kuweko mistari myekundu iliyo wazi kabisa katika nchi za Magharibi ambayo inapiga marufuku suala la kupinga kwa namna yoyote ile misingi ya uistikbari katika nchi hizo. Hivi kuna mtu anaweza kukubaliana na madai ya madola ambayo yanafanya ukandamizaji mkubwa mno dhidi ya watu wanaopinga na kulalamikia misingi ya uistikbari inayotawala katika nchi hizo, ya kwamba eti kuzuia kuvunjiwa heshima thamani takatifu za Uislamu ni kinyume na uhuru wa kusema?
Hii leo katika nchi nyingi za Magharibi mtu hathubutu hata kutilia shaka tu tukio lenye utata mwingi na ambalo uhakika wake haujulikani yaani tukio la Holocaust, au kuandika kitu dhidi ya siasa chafu za kimaadili za mabeberu kama vile mahusiano machafu ya watu wa jinsia moja. Vipi watu kama hawa wanaweza kudai kwamba, wanaheshimu uhuru wa kusema? Vipi inawezekana kukosoa na kutilia shaka masuala kama hayo kwa nchi hizo yawe ni kitu kiovu na iwe marufuku kabisa kufanyika katika nchi hizo; lakini linapofika suala la kuvunjiwa heshima Uislamu na matukufu ya Kiislamu iwe ni huru kufanya hivyo kwa kutegemea madai ya uongo ya kulindwa uhuru wa kusema kwenye nchi hizo?
Ukweli wa mambo ni kuwa, linapojitokeza siasa khabithi za Wazayuni, suala la maadili ya mataifa na kizazi cha vijana au suala la uhuru wa kusema huwa halina maana na mtu huwa haki na wala hathubutu kuzungumzia hilo - au kuhusiana na suala kama la Holocaust - lakini kuhusiana na kutusiwa na kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu hali ni kinyume kabisa! Kwa nini?
Mtu hawezi kuamini haya. Hivi kweli mtu anaweza kuamini kwamba, utawala kama wa Marekani unapigania demokrasia na kuunga mkono uhuru, wakati ambapo ulimuunga mkono kwa miaka 30 dikteta kama Hosni Mubarak (Rais aliyeng'olewa madarakani na mapindiz ya wananchi) au hatua yake ya kumuunga mkono kwa miaka 35 mtu kama Muhammad Reza Pahlavi (aliyekuwa mfalme wa Iran) licha ya jinai zote alizofanya; kwa hakika mtu hawezi kuamini kama mashambulio yao dhidi ya Iraq na utawala wa dikteta (wa zamani wa Iraq) Saddam Husain lengo lake lilikuwa ni kupambana na udikteta. Wao wenyewe ni walezi wa madikteta na ndio wanaowalea na kusaidia madikteta. Madikteta wa eneo letu la Kiislamu waliweza na wanaendelea kuwakandamiza, kuwadhulumu wananchi wao na kuwabagua kwa kuwategemea viongozi wa madola hayo ya kibeberu. Vipi watu kama hao wanaweza kudai kwamba, wanataka demokrasia? Kwa hakika mtu hawezi kuwaamini watu kama hawa. Hii leo duniani, fikra za waliowengi za wananchi ziko dhidi ya siasa za Kimarekani na Kizayuni. Ndio, tawala za nchi hizo hazifanyi hilo kutokana na maslahi yao ya kisiasa, lakini wananchi wamechoshwa na siasa za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wakati anapojitokeza mtekelezaji, kukajitokeza jambo fulani - kama hili lililotokea - mnaona harakati za wananchi kuelekea katika vituo vinavyofungamana na Marekani; katika vituo vya kisiasa, katika vituo vya kijamii vya Kimarekani katika nchi mbalimbali duniani. Madola haya yanachukiwa, ili ni jambo ambalo linaonekaa na kuhuhudiwa kwa uwazi kabsa katika kila kona ya dunia.
Ukweli wa mambo ni kuwa, nuru ya Uislamu itang'ara zaidi na zaidi kuliko wakati mwingne wowote ule katika kukabiliana na mashambulizi ya Waistikbari dhidi ya dini hii ya Mwenyezi Mungu, na bila ya shaka yoyote ushindi utakuwa ni wa umma wa Kiislamu; hili ni jambo ambalo haalina cheme ya shaka. Mfumo wa Kiislamu una jukumu zito na kubwa katika uwanja huu na nyinyi vijana azizi na wapendwa ambao mko katika uwanja huu na ambao mmekusanyika katika vikosi vya ulinzi, bila shaka mna sehemu nyeti kabisa ya jukumu hili.
Tuna matarajio kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakupeni nyote tawfiqi; atazing'arisha nyuso za mashahidi wa miaka 32 na 33 ambao walifidia roho zao katika uwanja huu na atazifufua roho zao pamoja na mawalii wake; atamfufua na mawalii wake Imam wetu mwenye shani (Imam Khomeini MA) ambaye alitufungulia sisi sote njia hii.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 
< Nyuma   Mbele >

^