Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mazungumzo ya Kiongozi Muadhamu na Wananchi wa Maeneo Yaliyokumbwa na Zilzala, Azerbaijan Mashariki Chapa
16/08/2012

Yafuatayo ni mazungumzo kati ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi katika kijiji cha cha mkoa wa Azerbaijan Mashariki, wakati alipotembelea maeneo hayo.

Kiongozi Muadhamu: Ni watu wangapi waliopoteza maisha hapa?
Wananchi: Watu wawili.
Kiongozi Muadhamu: Idadi ya watu hapa (katika kijiji hiki) ni kiasi gani?
Wananchi: 450.
Kiongozi Muadhamu: Lakini msongamano ni mkubwa mno?
Wananchi: Ndio, asilimia 99 ya kijiji hiki imeharibika (kabisa).
Kiongozi Muadhamu: Huduma hadi sasa zimekuwaje?
Wananchi: Alhamdulilahi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu. Mheshimiwa! Lakini usimamizi wa ugawaji ni dhaifu; ni dhaifu mno. Mtu mmoja anakuja na kuchukua (vitu na misaada) mara kumi; wakati kuna mtu mwingine ambaye kimsingi anaishi hapa na ni mkazi wa hapa, yeye haambulii chochote.
Kiongozi Muadhamu: Alaa, ajabu!
Wananchi: wananchi wametuma na kuleta vitu hapa kama mafuriko (vingi). Watu wote wako amilifu. Ni usimamizi tu ndio kwa kiwango fulani ni dhaifu; huo nao ni kutokana na hasara kuwa kubwa na kuenea.
Alhamdulilahi, misaada inafika hapa (kutoka katika pembe mbalimbali hapa nchini).
Kiongozi Muadhamu: Wewe ndio Gavana?
Gavana: Ndio.
Kiongozi Muadhamu: Hili suala la usimamizi umelisikia?
Gavana: Ndio, Inshallah, tunaandaa mipango na tutayapatia ufumbuzi matatizo yao (ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi).
Kiongozi Muadhamu: Kwa hakika serikali inajitahidi sana, na wananchi nao wamekuwa wakitoa huduma nyingi. Kwa hakika wananchi wako katika msiba na wako pamoja katika huzuni na msiba huu. Wananchi wote wa kila kona ya nchi, hususan wa maeneo haya wako pamoja na watu waliopata msiba katika mtetemeko huu wa ardhi. Viongozi na maafisa wa serikali nao kwa hakika wanajitahidi na wamefanya kazi kubwa mno. Kama walivyosema ndugu hapa, usimamizi uimarishwe kwa namna fulani ili uadilifu uweze kuenea na kupatikana.
Wananchi: Inshallah.
Kiongozi Muadhamu: Tuna matarajio kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakupeni subira. Watu ambao wamepata hasara hususan wale ambao wamepoteza ndugu zao wapendwa, tunataraji kwamba, Mwenyezi Mungu atawapa subira na ujira. Mimi daima nimekuwa nikiwausia wananchi wa maeneo ambayo wanakumbwa na matukio kama haya - kama tukio la tetemeko la ardhi, au mafuriko katika baadhi ya maeneo - ya kwamba, yafanyeni matukio haya kuwa jukwaa lenu la kupaa; hususan nyinyi vijana. Mashinikizo haya, hii mibinyo ya hali - iwe haya yanatokana na hali ya kawaida au ni hali iliyotiwishwa (kwenu) na watu wengine - yanapaswa kutufanya sisi tujitegee, tufanye kazi zaidi, tufanye hima maradufu; tutambue mapungufu yetu, na kisha tuondoe mapungufu haya; hili ni jukumu letu. Mimi ninaona Inshallah, mustakablai utakuwa mzuri mno; kwani hali ya hewa na tabia nchi ya eneo hili ni nzuri; wananchi wa eneo hili ni wananchi wazuri na wenye hima kubwa; vijana wao pia nao ni vijana ambao kwa hakika ni wazuri mno; Alhamdulilahi. Inshallah, Mwenyezi Mungu akupeni tawfiki nyote. Akupeni uhai. Nakutakieni mafanikio.

 
< Nyuma   Mbele >

^