Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu Alipokutana na Vikosi vya Ulinzi vya Mkoa wa Khorasan Kaskazini Chapa
12/10/2012
Ifuatayo ni matini kamili ya hotuba ya Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alipokutana na vikozi vya ulinzi vya mkoa wa Khorasan Kaskazini 12/10/2012
Bismillahir Rahmanir Rahim
Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote na kisha Sala na Salamu zimwendee Mtume SAW pamoja na aali zake wema na watoharifu.
Kwa hakika yaliyofanywa na nyinyi vijana hapa yalikuwa ni mazuri na mambo yaliyojaa umaanawi wa hali ya juu. Nyoyo safi za vijana na zenye nishati na uchangamfu wa unaja zinapoingia katika uga miongoni mwa nyuga - uwe ni uga wa kimaanawi au uga wa kidunia - hueneza umaanawi, vuguvugu na nishati ya umaanawi katika anga husika. Kijana aliyesoma Qur'ani hapa amesoma vizuri mno. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na Yeye kutupa tawfiki ya kuja hapa na kuweko katika mkusanyiko wenu huu nyinyi wapendwa na vijana wa jeshi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Jeshi la Polisi na Mabasiji wa eneo hili muhimu na nyeti katika nchi yetu.
Jukumu la Vikosi vya Ulinzi katika eneo hili kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi, ni masuuliya hatari, mazito na yenye kuainisha mambo. Katika kila nchi na baina ya kila taifa, kuna kikosi cha ulinzi chenye nguvu ambacho kimeandaliwa na kupata mafunzo ambapo kwa upande mmoja huwa ni nguzo na mtaji muhimu wa usalama wa taifa husika na kwa upande mwingine ni kinga na ngao ya usalama dhidi ya wageni ambao wana fikra ya kuvamia. Pindi taifa fulani linapokuwa na mikono imara na madhubuti ambapo likiwa ndani ya vazi la kikosi cha ulinzi likawa linaonyesha bila woga nguvu na uwezo lilionao, fikra potofu na tamaa ya taifa lile lenye uchu na kutaka makuu hudhoofika na adui huwa makini na kutochukua hatua za pupa.
Bila shaka nyinyi vijana azizi mnafahamu na mnapaswa kufahamu ya kwamba, tuko katika dunia ambayo imetawaliwa na siasa za kupenda vita na uvamizi. Kutaka vita ni moja ya kazi ambazo tangu kale zilikuwa ada na mazoea ya madola yenye nguvu, vamizi na yanayopenda kujitanua na kuvamia ardhi za wengine na katika zama zetu hizi - yaani zama za maendeleo ya ustaarabu wa kimaada - shauku ya hayo imeongezeka maradufu kutokana na tamaa ya kutaka kuuza silaha sambamba na kuboresha sanaa ya viwanda ambayo inategemewa na mabepari. Watu wenye nguvu iwe ni wanasiasa, au mabepari ambao wako nyuma ya viwanda vinavyotengeneza na kuzalisha silaha duniani, fikra zao ni kuanzisha vita na machafuko duniani; kupandikisha na kuyatwisha mataifa na nchi nyingine vita na migogoro. Kile ambacho kinaweza kusambaratisha shauku hii kabla ya kudhihiri na kujitokeza au kuitokomeza kabisa ni maandalizi ya taifa; ambapo maandalizi haya yanapatikana katika maandalizi jumla ya wananchi na vile vile maandalizi na utayarifu pamoja na uwepo wa vikosi vya ulinzi.
Hii leo Alhamdulilahi wananchi wetu azizi katika kila kona ya nchi, vijana wetu na wananchi wetu wanahisi kuwa na maandalizi ya kulinda na kutetea nchi yao; na wanahisi kuwa tayari kwa ajili ya kusukuma mbele gurudumu la nchi yao. Vikosi vyetu vya ulinzi navyo viko katika safu ya mbele ya kulinda na kutetea ardhi ya nchi, Alhamdulilahi hii leo vikosi vya ulinzi vina maandalizi ya kutosha na vina uwezo zaidi ikilinganishwa na huko nyuma.
Ndugu zanguni wapendwa! Amir al-Muminina Imam Ali bin Abi Talib (Alayhis Swalaat Wassalaam) anavitaja vikosi vya ulinzi kuwa ni husuni na ngao ya raia yaani anaviona vikosi hivyo kuwa ni ngome ya kuaminika kwa ajili ya wananchi; lakini anasema katika Nahaj al-Balagha kwamba, "kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, askari ni husuni ya raia." Katika maneno haya ya Imam Ali kuna ibara isemayo "kwa idhini ya Mwenyezi Mungu" jambo ambalo bila shaka kile ambacho kinaainisha mambo ni irada ya Mwenyezi Mungu. Kadiri vikosi vya ulinzi vitakavyosafisha nafsi zake na kumtaja Mwenyezi Mungu sambamba na kushikamana zaidi na mambo ya kimaanawi, ndivyo ambavyo uwezo wao utakavyoongezeka na ndivyo vitakapokuwa na uwezo zaidi wa kukabiliana na adui.
Nyinyi tazameni katika vita vya hivi karibuni katika eneo (Mashariki ya Kati), katika vita vya siku 33, katika vita vya siku 22 huko Gaza, Palestina, makundi madogo ya wapiganaji yalifanikiwa kulishinda jeshi ambalo kidhahiri linaonekana lina nguvu na ambalo nguvu zake zikizungumziwa. Wanajeshi wa jeshi hilo hawakuwa watu wanaomtambua Mwenyezi Mungu na kumzingatia katika mambo yao; bali wao walikuwa watu wa maada mia kwa mia; lakini wapiganaji na wanamujahidi walikuwa watu wa maanawi na watu ambao walikuwa na mahusiano na mawasiliano na Mwenyezi Mungu. Ushahidi wa wazi ni vijana na wapiganaji wetu wakati walipokuwa vitani; kwa hakika wao ni mfano wa wazi kabisa wa umaanawi na kumzingatia Mwenyezi Mungu ambao ulionyeshwa na vijana wa taifa hili katika vita. Katika ngome zetu, katika mstari wetu wa mbele vitani, katika nyusiku za kukabiliwa na hujuma na mashambulio na katika mashambulio ya kijeshi ya maadui dhidi yetu, kusoma dua na kunong'ona na Mwenyezi Mungu ni moja ya mambo ambayo yamebakia katika historia yetu, na miongoni mwa mambo ya taifa hili ambayo hayana mfano wala mithili; kwa hakika mambo haya yatabakia milele katika historia ya taifa letu.
Waheshimiwa maafisa wa jeshi wa vikosi vya kijeshi wana jukumu la kuwalea vijana hawa azizi, kuwandaa wapiganaji hawa kwa ajili ya kazi na kuwatayarisha kwa ajili ya kutetea heshima, izza, utambulisho pamoja na mipaka ya nchi. Hii leo taifa la Iran linahisi kuwa na nguvu mbele ya maaduzi zake. Hii hali ya kuhisi kuwa na nguvu, sio hisia ya uongo (ya kujidanganya), bali ni hisia ya kweli ambayo inaegemea na kutazama mambo kwa ukweli na uhalisia wake. Hili ni jambo ambalo hata maadui zetu wanalifahamu. Kwa hakika sisi ni wafuasi wa mafundishio ya Kiislamu na sio watu wa kuvamia au kumshambulia kijeshi huyu na yule; hata hivyo, sisi sio watu wa kulegeza kamba mbele ya mvamizi wa aina yoyote yule.Taifa la Iran na vikosi vya kijeshi hapa nchini vimejiandaa kwa namna ambayo havitoa idhini kwa maadui kuwa na fikra au dhana ya kutaka kuvamia nchi hii na vikosi hivyo viko katika maandalizi ya hali ya juu tayari kwa ajili ya kufanya kile ambacho ni jukumu lao. Utayarifu na maandalizi haya yanapaswa kulindwa na kuhifadhiwa. Maandalizi haya yanapaswa kuimarishwa siku baada ya siku na tambueni kwamba, kila harakati ambayo mnafanya kwa ajili ya kukifanya kikosi hiki kuwa na nguvu na uwezo, kuwa na umaanawi na kuwa na mipangilio ni jambo ambalo linahesabiwa kuwa jeja na zuri mbele ya Mwenyezi Mungu. Eneo hili ni eneo ambalo ni la watu mashujaa ambapo utajo wao ni kumbukumbu ya wapiganaji katika medani ya vita na daima hili limekuwa hai katika kumbukumbu zao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akupeni tawfiki na kukukirimuni. Tunamuomba Allah akupeni tawfiki ya kuhudumia na kuwa na hatima njema.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
 
< Nyuma   Mbele >

^