Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mkutano wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya Chapa
13/01/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kufanyika mkutano wa arubaini na saba wa kila mwaka wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Ulaya.
Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Wanachuo azizi
Nyinyi vijana ndio viongozi wa baadaye wa nchi (ya Iran). Iran ya kesho, yenye utajiri adhimu wa fikra za kielimu na kivitendo, inabidi iendeshwe na viongozi wakubwa wenye ustahiki ili iweze kupiga hatua kubwa na zenye kasi kubwa kuelekea kwenye malengo yaliyoainishwa kwa hima na imani na tabasuri (muono wa mbali) na ushujaa kama wenu nyinyi. Nyinyi na vijana wote, na wana wote azizi wa taifa la Iran popote walipo duniani, wana jukumu la kujiweka tayari kutoa michango yao katika jambo hili muhimu sana. Ninakuombeeni dua za kheri wakati wote. Mwenyezi Mungu akusaidieni na akupeni taufiki katika kazi zenu.

Sayyid Ali Khamenei.
 
< Nyuma   Mbele >

^