Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mnasaba wa Kufariki Dunia Dk. Hasan Habibi Chapa
31/01/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa risala na ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kufariki dunia Dk. Hasan Habibi, mmoja wa shakhsia mashuhuri wa Iran aliyetunga vitabu vingi aliyetoa huduma kubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kufanya kazi za siasa miaka mingi na aliyewahi pia kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa miaka mingi. Huku akiashiria historia ya utumishi wa Dk. Hasan Habibi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemtaja marhum Dk. Habibi kwamba alikuwa muumini mkweli, msafi na mwaminifu na ambaye hakuonesha kuchoka katika kuitumikia Jamhuri ya Kiislamu.
Ifuatayo ni matini kamili ya ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Nimeipokea kwa majonzi na huzuni kubwa, taarifa ya kufariki dunia mfuasi na sahibu wa muda mrefu wa Mapinduzi (ya Kiislamu) na ambaye alikuwa msomi, mwaminifu marhum na maghfur, Dk. Hasan Habibi (Mwenyezi Mungu amrehemu). Dk. Habibi alikuwa muumini mkweli, msafi na mwaminifu ambaye alikuwa yuko tayari kuihudumia Jamhuri ya Kiislamu wakati wote. Historia ya utumishi wake kwa Jamhuri ya Kiislamu ilianza kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na wakati wa kutungwa muswada wa Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na kuendelea kwa miaka mingi baadaye akiwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi (ya Kiislamu) na baadaye kuchukua nyadhifa na majukumu mengine makubwa. Maradhi yake mazito na ya muda mrefu yaliyohitajia subira, kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu na kutawakali Kwake, yaliongeza ubora wa shakhsia yake na matumaini ya kuongezekewa na rehema, maghufira na radhi za Mwenyezi Mungu. Ni wajibu wangu hapa kutoa mkono wa pole kwa mke wake mwaminifu na wafiwa wote pamoja na kwa wafanyakazi wenzake wote na wapenzi wa mtu huyu muhimu nikimuomba Mwenyezi Mungu ampandishe daraja za juu mbele Yake.
Sayyid Ali Khamenei,
Bahman 12, 1391 (Hijria Shamsia)
(Januari 31, 2013 Milaadia).
 
< Nyuma   Mbele >

^