Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Kikao Kikuu cha Nane cha Walimu wa Hawza ya Qum Chapa
13/02/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma risala maalumu kwa kongamano la Baraza la Walimu wa Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) ya Qum linalofanyika chini ya anwani: "Nusu Karne ya Mahudhurio" kwa lengo la kukumbuka na kuadhimisha miaka 50 ya jitihada na idili za kielimu, kiutamaduni na kisiasa za Baraza la Walimu wa Hawza ya Qum. Huku akisisitiza juu ya udharura wa kushukuriwa na kuthaminiwa nusu karne ya jitihada zilizojaa ikhlasi za baraza hilo lenye baraka la Hawza, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwenye ujumbe wake huo kuwa, Baraza la Walimu wa Hawza ya Qum ni dhihirisho la wazi la miaka 50 ya jitihada kubwa ambazo zimepitia kwenye vipindi vigumu vya kupambana na utawala wa taghuti na kufikisha kishujaa sauti ya Hawza ya Qum kwa watu wote kwa uwazi na bila ya kificho na kwamba vitisho, mashinikizo, kufungwa jela na kubaidishwa hakukuwazuia maulamaa wapigania jihadi kutetereka na wala kurudi nyuma katika misimamo na kazi za baraza hilo la watu wa dini.
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umesomwa leo asubuhi (Alkhamisi) na Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammadi Golpeygani, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kongamano hilo huko mjini Qum. Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Kulitukuza Baraza la Walimu wa Hawza ya Qum ni hatua nzuri na ya mahala pake kwa ajili ya kuthamini nusu karne ya jitihada zilizojaa ikhlasi za chombo hicho chenye baraka cha Hawza kinachoundwa na maulamaa wakubwa wenye tabasuri na muono wa mbali. Baraza hilo liliundwa katika kipindi kigumu cha maisha ya Hawza hiyo adhimu kutokana na kuweko haja kubwa mno ya kuwa na chombo hicho na limefanya jitihada iliyotukuka na nzito sana katika mazingira na vipindi tofauti iwe ni kwenye kile kipindi kilichojaa mateso na shida kubwa au katika kipindi cha kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na limeifanya Hawza (ya Qum) kuendelea kuimarika na kusonga mbele vizuri na kazi zake.
Baraza la Walimu wa Hawza ya Qum ni dhihirisho la wazi la jitihada, idili na kazi za miaka khamsini.
Kaatika kipindi kizito cha mapambano dhidi ya utawala wa taghuti, baraza hili liliweza kufikisha sauti ya Hawza ya Qum bila ya woga wala kificho kwa watu wote na kwamba vitisho, mashinikizo, kufungwa na kubaidishwa hakukuwazuia maulamaa wapigania jihadi wa baraza hilo la watu wa dini kuendelea na mapambano yao bila ya kusita wala kurudi nyuma ambapo kwa kutia saini waziwazi taarifa na matamko mbali mbali ya wazi waliweza kukipa heshima na itibari chombo hicho kitukufu. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu (nchini Iran) aidha, kushiriki wajumbe wa baraza hilo katika masuala mengi ya kisiasa, kijihadi, kielimu na kiutafiti na hivyo kutoa fursa kwa Hawza kutoa mchango wake mkubwa katika nyuga hizo na wakati huo huo kuonyesha sura bora na tukufu inayong'ara ya majimui hiyo iliyobarikiwa; katika nafasi ya juu ya "umarja'a" na majukumu mengineyo makubwa yanayohusu masuala ya dini na kisiasa na kupelekea sehemu adhimu ya taifa la Iran kulifanya baraza hilo kuwa marejeo yao ya kisiasa na kidini na kulifuata kwa moyo wa dhati likiwa ni hoja ya kisheria na yenye kuaminika kisiasa kwao.
Hivi sasa majimui hiyo yenye uaminifu na uzoefu wa nusu karne wa kazi za kisiasa na kimapinduzi linakabiliwa na mahitaji mapya na nyuga jadidi.
Moyo wa kufanya idili na ubunifu na kuchukua hatua za kishujaa katika nyanja zote sambamba na kujipamba kwa sifa za ikhlasi na unyofu wa moyo sifa ambazo zimekuwa zikionekana wazi siku zote kwenye baraza hilo, kutalisaidia baraza hilo kupiga hatua madhubuti zaidi ya hizi lilizozipiga katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.
Hivi leo vijana wapya na bora ambao ni matunda ya mti huu mwema uliojaa baraka wa Hawza, wamekodolea macho na kuangalia kwa umakini upeo wa mbali na wa juu sana. Malengo makubwa ni yenye kufikiwa na hima nazo ni kubwa na makini.
Fursa na matumaini ni hazina kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambapo jihadi nzito ya taifa la Iran imelipelekea taifa hili kustahiki kupata fadhila na baraka hizo kubwa za Mwenyezi Mungu. Kipaji kikubwa cha watu wakubwa na walioko mstari wa mbele wa Hawza kikiwemo chombo hiki kikongwe na chenye mizizi madhubiti cha Baraza la Walimu wa Hawza ambacho kinaonekana wazi katika rasilimali hii yenye thamani kubwa, inabidi kitumiwe vizuri na kufaidisha mirengo ya kidini na kimapinduzi katika nchi hii ya Mwenyezi Mungu. Yaliyopo leo hii yatumike vizuri kujenga kesho iliyo bora na kwa njia hiyo iweze kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu aliposema:

أَلَمْ تَرَ كَیْفَ ضَرَبَ اللّهُ مَثَلاً كَلِمَةً طَیِّبَةً كَشَجَرةٍ طَیِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِی السَّمَاء، تُؤْتِی أُكُلَهَا كُلَّ حِینٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ...
Je, hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi... (Surat Ibrahim 14: 24-25).

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Sayyid Ali Khamenei,
Bahman 25, 1391 (Hijria Shamsia)
(Februari 13, 2013 Milaadia).
 
< Nyuma   Mbele >

^