Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aipoonana na Maelfu ya Wananchi wa Qum Chapa
08/01/2013

Ifuatayo hapa nchini ni matini kamili ya hotuba ya Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa alipokutana na maelfu ya wat wanamapinduzi na wenye kushikamana na dini wa mjini Qum, tarehe 08/01/2013.

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

Ninatumia fursa hii adhimu kkukaribisheni nyinyi nyote makaka, madada, vijana azizi wa Qum, masheikh, matalaba (wanafunzi wa masomo ya dini) waheshimiwa na maulamaa wenye shani ambapo kwa mnasaba huu muhimu, kwa mara nyingine tena wameifanya Husseiniya yetu hii itawaliwe na anga ya hamasa, shauku, huba na hisia. Kumbukumbu ya tukio lile lisilosahaulika la tarehe 19 mwezi Dei ambalo limekuwa ni lenye kubakia katika historia, mumeihuisha tena. Kwa hakika ninatoa shukurani za dhati kutokana na ratiba ilivyoendeshwa na mambo yaliyofanyika hapa; wimbo ulioimbwa hapa na makaka na madada kuukariri ulikuwa umebeba maana ya kadhia ya tarehe 19 mwezi Dei na kumbukumbu ya tukio hili adhimu ambapo kwa hakika tukio hili sio la kukariri au la kawaida; bali ni suala la kimsingi na muhimu sana. Minasaba yetu yote mikubwa ya kihistoria iko namna hii. Kwanza kizazi kipya na kijana ambacho kimechukua jukumu na masuuliya ya vijana wa zama zile hutambua chimbuko la historia yao kwa kuadhimisha kumbukumbu kama hii na hulihisi kabisa jambo hilo; Pili, jambo hili hupelekea kutambuliwa thamani ya mapambano yaliyoendeshwa kwa ajili ya kulifanya taifa hili lifikie katika hatua hii sambamba na magumu yaliyopatikana katika njia hii pamoja na hatari ambazo wananchi wa wakati huo walisimama na kukabiliana nazo kwa vifua vyao; mambo haya hubainishwa na kuwekwa wazi kwamba, kile ambacho leo taifa la Iran inacho, neema na ujazi ambao haukupatikana kirahisil sio tukio la sadfa. Taifa la Iran lilijihatarisha, lilifanya hima, likakubali kuwa tayari kutoa roho, likasimama kidete mkabala na polisi majabari na wajeuri wa utawala wa Kitaghuti (utawala wa kifalme wa Shah).
Wananchi wakauawa katika harakati hizo za kupigania mapinduzi, wakatoa mashahidi, na wengine wakajeruhiwa na hatimaye kafila na masafara huu adhimu uliokuwa na azma na irada thabiti ukafanikiwa kufika hapa ulipo. Hii nayo ni nukta ya pili.
Nukta ya tatu ni darsa na funzo tunalopata siisi hii leo. Vijana wetu azizi hawajaishuhudia siku ile na kipindi kile, hawafahamu nini kilitokea siku ile. Wale ambao walikuweko katika zama zile wanafahamu; katika siku ile kidhahiri ilikuwa inaonekana kuwa, ni jambo lisiloyumkinika kabisa kwa taifa la Iran kuushinda utawala uliojaa ghururi na majigambo wa kitaghuti. Ilikuwa ikisemwa kwa kustaajabu kwamba, taifa la Iran - wakitolewa mfano wananchi wa Qum - linataka kusimama mkabala na mfumo wa kitaghuti wa Kipahlavi na kuusambaratisha. Watu walikuwa wakisema jambo hili linawezekana kweli? Lakini lile jambo ambalo lilikuwa likionekana kuwa ni muhali, liliwezekana na kutokea. Hivyo jambo hili limetokea (na kubakia katika historia).
Hii leo pia taifa la Iran lina malego makuu (matukufu), lina madai na lina maneno makubwa; kwa ajili ya nchi yake, kwa ajili ya ulimwengu wa Kiislamu na kwa ajili ya mwanaadamu kwa ujumla. Mkabala na taifa la Iran kuna mbwa mwitu wenye njaa, wanyama hatari, makampuni haya ya utumiaji mabavu, majimui hii ya wataka makuu duniani na waabudu dunia ambao wamepanga safu; wanatengeneza silaha, wanauza silaha, wanataka vita, wanaupeleka Umoja wa Mataifa kwa matakwa yao; wanapeleka wanajeshi popote watakapo; wanafanya khiyana na usaliti, wanaunga mkono dhulma , wanatoa himaya na uungaji mkono kwa utawala ghasibu wa Israel; wanafanya dhulma katika jamii ya mwanadamu na wamekuwa wakitumia nguvu za kidhahiri kama zile tulizokuwa tukizishuhudia katika kipindi cha utawala wa kitaghuti hapa Iran. Hii leo pia kuna watu wanauliza, ee Bwana! Kwa inawezekana kusimama mkabala na safu hii iliyoungana ya maadui wenye silaha, mabavu, vyombo vya habari, uchumi, siasa na kila kitu? Kwani itawezekana kusonga mbele? Hii leo pia maneno yale yale ya wakati ule yanakaririwa tena. Hii ni tajiriba.
Ndio, haya sio maneno yetu; bali haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kiabu kitakatifu cha Qur'ani. Endapo watu wataingia uwanjani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu SWT na kusimama kidete basi bila shaka kupata kwao ushindi ni jambo ambalo halina shaka. Mwenyezi Mungu SWT anasema:
"Na lau makafiri wangelipigana nanyi basi bila ya shaka wangeligeuza migongo, kisha wasingelipata mlinzi wala msaidizi. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu ulio kwishapita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu." ( Al-Fat'h 48:22-23).
Kwa hakika jambo hili halihusiana tu na tukio la vita mwanzoni mwa Uislamu yaani hii "bila ya shaka wangeligeuza migongo" ( Al-Fat'h 48:22); la hasha, bali hii ni "Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu uliokwisha pita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu." ( Al-Fat'h 48:23).
Ndio, wakati ambao sisi maneno yetu wenyewe tutakuwa hatuyajui, au tukawa hatufahamu kusema, kuandaa mipango, au tusisimame kidete kutetea msimamo wetu, au aada yakufika katikati ya njia tukakumbwa na vishawishi vya shetani au vishawishi vya nafsi au tukaingiwa na hali ya uvivu na hali ya kutetereka, basi ni jambo lililo wazi kwamba, mapambano yetu hayawezi kufikia popote yaani hayatakuwa na natija. Suala hapa ni kwamba kama anavyosema Mwenyezi Mungu: "Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayemsaidia Yeye." (Al-Haj 22;40).
Kwa hakika hakuna sisitizo zaidi ya hili. Kama tutamsaidia Mwenyezi Mungu - kumsaidia Mwenyezi Mungu kwa kufikiri, kuchimbua fikra na kuzitoa zile ambazo ni za asili na sahihi, kusimama kidete kuzitetea, kuwa na tadbiri kwa ajili ya kuifanya kazi hiyo isonge mbele na kuwa na natija na wakati huo huo kusimama kidete na kuwa ngangari kwa ajili ya kukabiliana kwa vit vyote na hatari vilivyopo - bila shaka Mwenyezi Mungu atatoa auni na msaada Wake na atatupa nusra na ushindi. Maana ya «لينصرنّ» iliyokuja katika aya iliyotangulia ina maana kwamba, nusra na msaada huo hauna shaka. Mwenyezi Mungu SWT anasema:
"Na nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu." (An-Nisaai 4:122). Taifa la Iran limepata tajiriba ya haya katika vitendo. Endapo nyinyi wananchi wetu azizi, nyinyi vijana wenye moyo, ari, azma na irada mtasimama kidete katika njia hii mnayokwenda, basi msiwe na shaka kwamba, bila ya shaka yoyote sunna hiyo ya Mwenyezi Mungu inalijumuisha pia taifa (lenu) hili kwa wakati unaofaa na kupelekea kufanikiwa malengo, matumaini na kaulimbiu zao zote za kitaifa, Kiislamu na kimataifa. Kila kazi ina zama na wakati wake; haya yatafanikiwa katika zama mwafaka. Taifa la Iran limezingatia na kutoa umuhimu kwa jambo ambalo inalo na limefanya harakati kwa ajili ya hilo na hivyo bila shaka litafanikiwa katika njia hii, lakini njia ya kufikia hilo ni muqawama, kuwa ngangari na kusimama kidete.
Katika mazingira kama hayo nini kitatokea? Mkondo wa historia ya dunia utabadilika; muelekeo wa historia utageuka. Hii leo njia ya historia ni njia ya kidhulma; ni njia ya kibeberu na kukubali ubeberu; kuna baadhi ya watu ni mabeberu duniani na watu wengine wanakubali ubeberu. Kama maneno yenu nyinyi wananchi wa Iran yameweza kusonga mbele, kama nyinyi mumeweza kupata ushindi na kama mtaweza kufikia ile nukta iliyoahidiwa, basi bila shaka wakati huo mkondo wa historia utabadilika; na hivyo kuandaa mazingira ya kudhihiri Imam wa Zama, (Imam Mahdi AS), Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake; na kwa muktadha huo ulimwengu utaingia katika hatua na marhala jadidi. Hii inafungamana na azma yangu na nyinyi hii leo na hii inafungamana na maarifa yangu na nyinyi hii leo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa na lengo la kuzifanya nyoyo ziwe imara na madhubuti kwa ajili ya kufikia ahadi, hutekeleza baadhi ya ahadi hizo katika kipindi cha muda mfupi. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwambia mama yake Nabii Mussa AS kwamba: Na utakapomkhofia basi mtie mtoni, (Al-Qasas 28-07). Kisha akamwambia: Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume. (Al-Qasas 28-07).
Mwenyezi Mungu hapa alitoa ahadi mbili pale alipomwambia mama yake Nabii Mussa AS: Mtie mtoni - usikhofu - ahadi ya kwanza ni hii, "tutamrudisha kwako" na ahadi ya pili ni "tutamfanya miongoni mwa Mitume'. Utume wenyewe ni ule ambao Bani Israili kwa miaka mingi - yumkini karne nyingi - walikuwa wakiusubiri. Baadaye Nabii Mussa AS alirejea kwa mama yake katika kasri ya Firauni. Mwenyezi Mungu anasema:
"Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui". (Al-Qasas 28-13).
Katika aya hii Mwenyezi Mungu anaonesha kwamba, ametekeleza ahadi ya kwanza ili atambue kwamba, ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli; na ile ahadi ya pili itatimia.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamiliana hivi na taifa la Iran; ametimiza ahadi nyingi mno na kuna kazi kubwa sana ambazo zimefanyika. Enyi Vijana azizi! Tambueni kwamba, katika zama zile hakuna mtu ambaye alikuwa akiamini kwamba, mfumo wa kitaghuti unaweza kutetereka seuze mtu atake kuusambaratisha na kuutokomeza?
Hii leo nyinyi mnaona kuwa, mfumo wa kitaghuti ndio mfumo unaochukiwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu; nchini Iran (mfumo huu) umesambaratishwa kabisa na - kwa kauli maarufu - umetupwa katika shimo la taka la historia. Katika zama hili kama ingetokea watu wakasema kwamba, yamkini Iran ikaondoka katika makucha ya ubeberu, kwa wale ambao walikuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya nchi, bila shaka wangesema kwa yakini na uhakika kabisa kwamba, kitu kama hiki hakiwezekani. Masuala yote ya nchi, sera zote kubwa za nchi zilikuwa katika udhibiti na mamlaka ya Marekani; wakati mwingine Marekani ilikuwa ikiingilia na kutoa uamuzi hata katika masuala madogo kabisa ya Iran; kwa mfano ni mtu gani awe waziri wa wizara fulani, au mathalani nani asiwepo, au ongezeni bei ya mafuta kwa kiwango fulani au msiongeze na masuala mengine mfano wa hayo.
Kwa udhibiti kama huu wa Wamarekani na waliokuwa wakiwazunguka Wamarekani kwa nchi yetu, kwa taifa letu na kwa heshima yetu ni nani ambaye alikuwa akiamini kwamba, mambo hayo yangekwisha na kuja kutokomea kabisa? Hii leo duniani mnaona nyinyi, taifa fulani likitaka kutaja jina la nchi ambayo inajitegemea na sio tegemezi kwa siasa za kibeberu za Marekani na mfano wa Marekani basi hutaja jina la Iran; (Iran imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na kusimama kwake kidete na kutokubali kunyongeshwa). Mataifa mengine yanaitazama Iran, hupata hamasa kutokana na kusimama huku kidete, hii hali ya kuwa wazi na kutoogopa, huu ushujaa na msimamo thabiti uliooneshwa na taifa la Iran; yote haya yanalifanya taifa hili la Kiislamu kuwa kigezo cha mataifa mengine yanayopigania kujitegemea na kuondoka chini ya makucha ya mabeberu). Waistikbari wote na madola ya kibeberu duniani yamekusanya pamoja nguvu zao ili yaliwekee vikwazo taifa la Iran; ili wawachoshe wananchi wa Iran kupitia vikwazo hivi na hivyo kuwafanya wabadilishe msimamo msimamo wao. Tofauti na huko nyuma, hivi sasa waistikbari wanakiri wazi wazi kuwa malengo ya vikwazo vyao ni kulichosha taifa la Iran, kuwachochea wananchi kukabiliana na mfumo wao wa utawala wa Jamhuri ya Kiislamu, kuongeza mashinikizo dhidi ya viongozi wa Iran na mwishowe kuwafanya wabadilishe misimamo yao. Kwa hakika haya ni mambo ambayo leo yanasemwa wazi tena bila kificho na madui wa Iran.
Awali huko nyuma wakati sisi tulipokuwa tukitoa uchambuzi, walikuwa hawayasemi haya kwa wazi na bayana kiasi hiki; lakini hivi sasa wanayasema haya bayana na dhahiri. Natija yake imekuwa hii ambayo leo nyinyi mnaishuhudia ambayo ni wananchi wa Iran kuzidi kuelekea katika misingi ya Uislamu siku baada ya siku, wananchi wa Iran kuzidi kuelekea katika misingi ya mapinduzi, wananchi wa taifa hili kuzidi kusimama kidete, wananchi Waislamu wa Iran kuzidi kuelekea upande wa izza ya nchi hii ambayo imepatiwa na Mwenyezi Mungu na mambo haya yanazidi kuongezeka siku baada ya siku; mambo yaliyotokea katika nchi hii ni kinyume kabisa na yale ambayo yalikuwa yakitakiwa na maadui. Yaani mambo yamekweda kinyume kabisa na matarajio ya maadui wa taifa hili.
Hizi ni ibra na mafunzo makubwa ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia; na moja ya nukta za darsa na mafunzo haya ni hili tukio la tarehe 19 Dei ambalo fakhari yake mnayo nyinyi wananchi wa Qum. Tab'an, Qum haina fakhari hii tu; kuna fakhari nyingi katika historia ya wananchi wa Qum. Katika kipindi hiki cha miaka 90 au mia moja ya hivi karibuni, kuliibuka chemchemu nyingi za fakhari zilizotiririka katika mji Mtakatifu wa Qum. Walikuwa ni watu wa Qum ambao walimpokea kwa mikono miwili marhumu Al-haj Sheikh (radhiallah anhu) na wakamleta na kuasisi Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) hii kubwa ya kelimu. Haya malezi ya Mwenyezi Mungu na yasiyotarajiwa yamefanyika katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) hii na ambayo kwa kweli ni kwa baraka za hima ya wananchi wa Qum; Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) ambayo mtu kama Imam wetu mwenye shani (Imam Khomeini MA) alitokea hapo na hili tukio hili adhimu duniani ambalo hatupaswi kusema kuwa ni tukio muhimu na adhimu hapa nchini bali ni la dunia nzima, yaani ni la kimataifa.
Katika matukio ya mwaka 1342 Hijria Shamsiya na matukio ya mwaka 1341 Hijria Shamsiya, katika matukio ya mapinduzi na katika matukio ya vita vya kulazimishwa (vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na dikteta wa wakati huo wa Iraq Saddan Hussain), wananchi wa Qum walionesha sura na haiba mahiri na kubwa ambapo Inshallah tunataraji kwamba, daima hali iwe namna hii.
Kuna nukta muhimu - ambayo ninataka kuwaambia nyinyi vijana azizi wa Qum - katika harakati hii ambayo ni mtu kuwa makini na mjanja, azifuatilie kwa makini nyendo za adui, amtazame adui na kuzifuatilia kwa karibu harakati zake na kugundua malengo ya adui; kwa hakika hili ni jambo muhimu sana. Endapo wewe katika mapambano yako na mtu (hasimu wako) utaweza kutabiri harakati anayotaka kuchukua hasimu wako huyo, bila shaka huwezi kupata pigo kwani tayari unafahamu adui anataka kufanya nini. Lakini kama utakuwa hauko makini, fikra zako hazipo, utakuwa katika mghafala (hali ya kughafilika) na kutokuwa na umakini na utulivu unaotakiwa, au kama utakuwa umeshughulishwa na kitu kingine na hivyo kushindwa kutabiri kwamba, mwenzako anataka kufanya nini, bila shaka utachezea kipigo. Hii inatokana na kuwa, adui yuko macho na hajalala.
Amirul Muminin Ali bin Abi Talib (Alayihs Swalaat Wassalaam) anasema: Mwenye kulala, adui yake hajalala." Kwa maana kwamba, kama mtu yuko vitani na kisha akazubaa au kupitiwa na usingizi, basi atambue kwamba, adui yake hajalala, yaani haina maana kwamba, wewe ukilala basi na adui yako naye amelala; hapana, yamkini wewe ukawa umelala lakini adui yako akawa yuko macho; wakati huo atakudhuru. Hivyo haipaswi kughafilika na kukumbwa na mghafala hata kidogo; bali daima na wakati wote mtu anapaswa kuwa macho na makini mno. Hii kwamba, sisi tumekuwa tukikokoteza na kutilia mkazo na kuwasisitizia maafisa wa serikali na wananchi pia kwamba, wasijishughulishe na masuala madogo madogo, sababu yake ni hii. Hii kwamba, tumekuwa tukiyausia majarida, vyombo vya habari, magazeti na mitandao ya intaneti ambayo leo imeenea na tumekuwa tukisisitiza kwamba, ijiepushe na suala la kuingiza maneno yasiyo sahihi katika fikra za wananchi na kuwashughulisha, sababu yake ni hii.
Hivyo wananchi wa taifa hili wanapaswa kuwa macho na makini kabisa na watambue wanapiga hatua kuelekea wapi - kujipamba na taqwa ya wote ndio huku -, taifa hili linapasa kutambua litaka kufanya nini na liwe macho na makini na kufahamu linadhurika na kupata pigo kutoka wapi. Katika amali na matendo ya mtu binafsi, kama sisi tutajipamba na taqwa na uchaji Mungu, tukawa ni wenye kuchunga amali zetu, tukajichunga katika kila jambo tunalofanya; kwa mfano mtu hatii mguu mahala ambapo panateleza; mahala ambapo kuna khofu basi mtu haii mguu wake hapo na anakuwa makini; hivyo kuna haja ya kuwa macho na makini. Kwa hakika hiki ni kitu cha lazima.
Hii leo kile ambacho mimi ninakiainisha - ambacho kinabainisha harakati ya adui - ni hiki: Licha ya kuwa uchaguzi muhimu unatarajiwa kufanyika nchini Iran takribani miezi mitano ijayo yaani mwezi Khordad 1391 (Juni, 2013) uko mbele yetu, lakini adui tayari ameshughulishwa na uchaguzi wetu. Kwa hakika kwa mtazamo wetu uchaguzi ambao utafanyika hapa nchini mwezi Juni ni muhimu na kwa mtazamo wa adui ni muhimu pia; adui ameelekeza fikra zake katika uchaguzi huu. Laiti maadui wa taifa hili wangelikuwa wanaweza, basi wangelihakikisha kwamba, uchaguzi huu haufanyiki. Vizuri, hawawezi kufanya hilo, hawana uwezo wa kufa; wamekata tamaa kama wanaweza kufanya kazi hii. : Kuna wakati baadhi yao walijaribu kadiri walivyoweza kuhakikisha uchaguzi wa Bunge hapa nchini Iran unaakhirishwa angalau kwa wiki mbili, lakini sisi tulisisitiza kuwa uchaguzi hauwezi kuakhirishwa hata kwa siku moja na hivyo njia ya kuakhirisha uchaguzi ikafungwa kama ilivyofungwa kikamilifu njia ya kuzuia kabisa kufanyika uchaguzi. Hivyo hawakuweza kufikia popote. Hivyo wamepata tajiriba na wanafahamu kwamba, uchaguzi (hapa nchini sio wa kuakhirishwa); na ndio maana sasa wanatafuta njia nyingine. Moja ya malengo yao ni kutaka kuhakikisha uchaguzi unafanyika lakini bila ya kuweko mahudhurio makubwa yalioambatana na hamasa; yaani uchaguzi ufanyike lakini kusiweko na maudhurio makubwa yaliyoambatana na hamasa.
Kwa hakika watu wote wanapaswa kutambua kuanzia sasa ya kwamba: Watu ambao yumkini kutokana na kuguswa na kuwakwao na uchungu wakatoa nasaha jumla kuhusiana na uchaguzi ya kwamba, bwana ee uchaguzi uwe hivi au usiwe hivi, watu hawa wanapaswa kuwa makini mno wasije katika mazungumzo yao wakamsaidia adui; wawe makini katika mazungumzo yao wasiwakatishe tamaa wananchi kuhusiana na uchaguzi, wasing'ang'anie kupiga kelele kwamba, uchaguzi unapaswa kuwa huru. Vizuri, inaelewea wazi kwamba, uchaguzi unapaswa kuwa huru. Kuanzia mwanzoni wa mapinduzi hadi leo, sisi tumefanya chaguzi thelathini na ushei; ni uchaguzi gani kati ya chaguzi hizi ambao haukuwa huru? Ni katika nchi gani duniani ambako kunafanyika uchaguzi huru zaidi ya Iran? Ni wapi ambapo ustahiki na sifa za wagombea unazingatiwa na kuchambuliwa namna hii? Hata wata wafikie kushikia bango hili hapa nchini, wasisitize na kulikaririkariri wakidhani kwamba, kwa kufanya hivyo taratibu taratibu watie katika fikra za wananchi kwamba, uchaguzi huu hauna faida? Kwa hakika hili ni moja kati ya matakwa ya adui. Wale watu ambao wanazungumza maneno haya hapa ndani, yumkini wakawa katika mghafala. Mimi nasema, wasighafilike, wawe makini, kazi yenu hii isiwe ni kumsaidia adui kujaza jedwali la mafumbo; msimsaidie adui kufikia na kukamilisha malengo yake. Hii ni moja ya njia za kuufanya uchaguzi hapa nchini usiwe na hamasa na msisimko.
Jambo jingine ni kuwabebesha wananchi kwamba, uchaguzi si salama wa kutosha na kama inavyotakiwa. Tab'an, binafsi ninasisitiza kwamba, uchaguzi unapaswa kufanyika katika mazingira salama; isipokuwa hili lina njia yake. Katika Jamhuri ya Kiisamu, katika sheria zetu, kuna njia nyingi na nzuri za sheria ambazo zimeainishwa kwa ajili ya kulinda usalama wa uchaguzi. Tab'an, kama watajitokeza watu na kutaka kufanya mambo kinyume na sheria, bila shaka hatua hiyo itakuwa ni kwa madhara ya nchi. Iwapo watu wote wataheshimu na kutekeleza vizuri sheria hizo na kama inavyotakiwa, basi bila ya shaka yoyote uchaguzi utakuwa wa salama, isipokuwa kama watu watataka kufanya mambo kinyume cha sheria kama ambavyo baadhi ya watu ambao hawakuheshimu sheria walivyosababisha fitna ya mwaka 2009 na kuwasababishia usumbufu wananchi na nchi, na kujisababishia wenyewe madhara makubwa sana na kuporomoka kabisa. Hivyo basi kuna njia nzuri za kisheria. Ndio, mimi ninasisitiza na kutilia mkazo suala la kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa salama na wenye uaminifu na kwamba viongozi wa serikali na wasio wa serikali wanatakiwa kuchunga na kuheshimu kikamilifu sheria, taqwa na usafi wa nafsi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa salama na kwa yakini hivyo ndivyo itakavyokuwa. Moja ya njia zinazoweaa kumsaidia adui kufanikisha lengo lake kuu katika uchaguzi (hapa nchini Iran) ni kuwashughulisha wananchi na kitu kingine. Yumkini baadhi ya watu wakajaribu kuwashughulisha wananchi na masuala mengine kwa kuzusha jambo fulani au kadhia fulani ya kiuchumi, kisiasa na kiusalama ambapo jambo hilo nalo ni katika mbinu za kuwasaidia maadui, lakini mimi nina yakini kuwa wananchi wa Iran wana muono wa mbali sana na ni werevu mno kiasi kwamba hawawezi kuhadaiwa na mambo kama hayo ya kiuadui ya maadui na vibaraka wao. Inshallah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nguvu, tawfiki na fadhila Zake uchaguzi ujao (wa Juni mwaka huu) utakuwa uchaguz mzuri na wenye hamasa.
Tab'an, nina mengi ya kusema kuhusiana na suala la uchaguzi. Inshallah, endapo Allah atanipa uhai nitalizungumzia tena suala la uchaguzi hapo mbeleni. Kuna nasaha na nukta za kubainisha kuhusiana na hili; hata hivyo kwa leo natosheka na haya. Tambueni kwamba, kushiriki katika uchaguzi ni haki na ni jukumu kwa kila mtu. Sisi kila mmoja wetu tukiwa miongoni mwa watu katika jamii tuna haki ya kushiriki katika uchaguzi na vile vile hilo ni jukumu letu kufanya hivyo. Kila mtu ambaye ana imani na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na anaikubali Katiba anataka kutumia haki yake hiyo na wakati huo huo anataka kutekeleza jukumu lake katika suala hilo na wako watu wengine ambao wanataka kuwathibitishia wananchi ustahiki wao. Sote tunapaswa kutekeleza jukumu hili. Moja ya majukumu hayo ni kuwaonesha wananchi kwamba kweli wanastahiki. Kila mtu ambaye anahisi ana ustahiki na sifa na anafahau kazi ya utekelezaji anakuja na kujitoeza mbele za watu akitaka achaguliwe. Kuongoza nchi ni kazi nzito na wala sio kazi lelemama hata kidogo. Kuna kazi kubwa na mizigo mizito katika mabega ya viongozi wa ngazi za juu. Yumkini kukawa kuna watu wanaofanya kazi katika daraja nyingine ambao wasiweze kuainisha kiwango cha uzito na ukubwa wa kazi hii ya uongozi. Hivyo basi watu wanaojitokeza kwa ajili ya kugombea wanapaswa ndani ya nafsi zao wahisi kwamba, wana uwezo wa kubeba jukumu hilo zito; watu wanaojitokeza kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu kwa hakika wanapaswa kushikamana kikamilifu na mfumo unaotawala nchini na washikamane vilivyo pia na Katiba, na watake ndani ya dhati ya nafsi zao kwamba Katiba itekelezwe kwani Rais hula kiapo cha kuheshimu jambo hilo na mtu hawezi kula kiapo cha uongo.Suala la ustahiki limetiliwa mkazo katika Katiba na katika Baraza a Kulinda Katiba. Watu ambao wana hisia hii huja uwanjani; na watu ambao hapana hawana nia ya kujitokeza na kugombea kiti cha Urais basi na wajitokeze katika uwanja wa kusaidia ili uchaguzi huu uwe wa hamasa kubwa.
Napenda kuwaambia kwamba, kutokana na imani yetu kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu - ahadi ya Allah ni ya kweli na ya haki - hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atalifanya taifa hili limshinde adui katika marhala (hatua) hii na katika hatua zote katika mustakbali, Inshallah. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutotufanya tumdhanie dhana mbaya. Allah anasema:
"wanao mdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya" (Al-Fat'h 48:06). Mwenyezi Mungu hajatuweka katika kundi hili. Hakika sisi tuna dhana nzuri na ahadi ya Mwenyezi Mungu. Katika upande mwingine tunaona kuwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametoa ahadi ya msaada na nusra na katika upande mwingine mtu anashuhudia kuna mahudhurio, mapenzi, hima na ikhlasi hii ya vijana, utakasifu huu wa vijana, baba na akina mama hawa waumini. Haya ni mambo ambayo mtu anayashuhudia wazi katika matabaka yote ya wananchi pamoja na dhahiri yao kuwa tofauti. Mtu anashuhudia kwamba, wananchi wa taifa hili ni wananchi ambao, Alhamdulilahi wako katika medani.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu akushushieni rehma, mapenzi, tawfiki na afya nyinyi wananchi azizi wa Qum na Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) yenye shani ya Qum. Aifufue roho takasifu ya Imam Khomeini MA pamoja na mawalii Wake, Imam ambaye kwa hakika ndiye aliyetufungulia njia hii. Ewe Mola, zijumuishe katika baraka na fadhila Zako roho takasifu za mahahidi azizi waliojotolea katika njia hii na vile vile wanamapambano ambao walipigana jihadi katika njia hii ya haki na utufanye sisi tuwe imara na madhubuti katika njia hii.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabaakaatuh.

 
< Nyuma   Mbele >

^