Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Tanzia Kufuatia Kufariki Dunia Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mujtaba Musawi Lari Chapa
09/03/2013

Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Alasiri ya leo (Jumamosi) ametoa ujumbe maalumu wa tanzia kufuatia kufariki dunia mwanachuoni na mwandishi mujahid, Hujjatul Islam Walmuslimin Alhaj Sayyid Mujtaba Musawi Lari ambaye pia alikuwa mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) huko Lorestan.
Matini kamili ya ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Nimeipokea kwa masikitiko makubwa habari ya kufariki dunia mwanachuoni mkubwa na mwandishi mujahid, marhum Hujjatul Islam Walmuslimin, Alhaj Sayyid Mujtaba Musawi Lari.
Kazi zilizofanywa na Aalimu huyu mkubwa na mwenye thamani kubwa katika kueneza elimu na mafundisho ya Kiislamu na ya chuo cha Ahlul Bayt Alayhimus Salaam katika pembe zote za dunia katika miongo kadhaa ya hivi karibuni, kwa hakika ilikuwa ni kazi ya aina yake kabisa na kwamba maelfu ya watu wenye insafu na kiu ya kutafuta elimu na kujua ukweli, waliweza kutambua chemchemu isiyo na mwisho ya haki na kuutambua Uislamu na kuuamini kupitia maandishi yaliyojaa mantiki na upana wa kielimu ya mwanachuoni huyo (yaliyofasiriwa kwa lugha tofauti) na kusambazwa katika mabara yote matano ya dunia.
Aalimu huyu mkubwa na ambaye kamwe hakuwa na riya wala majigambo alijitolea kikamilifu na bila ya kumtegemea huyu wala yule na kutumia umri na uwezo wake wote katika jihadi hiyo kubwa na alitia hima kubwa katika kutekeleza vilivyo jukumu lake kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu.
Ninaitumia fursa hii kutoa mkono wangu wa pole kwa dhati ya moyo wangu kwa wananchi wa Lorestan na mkoa wa Fars na kwa wapenzi na wanafunzi wote wa mwanachuoni huyu waliofaidika na vitabu vyake na vile vile kwa familia na wafiwa wote kufuatia kifo cha aalim huyu na namuomba Mwenyezi Mungu ampandishe daraja za juu na ammimie rehema na maghufira Yake.
Sayyid Ali Khamenei,
Esfand 19, 1391
(Machi 9, 2013).

 
< Nyuma   Mbele >

^