Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia Kutokea Mtetemeko wa Ardhi katika Mkoa wa Bushehr wa Iran Chapa
09/04/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kufuatia kutokea tukio chungu la mtetemeko wa ardhi mkoani Bushehr (kusini magharibi mwa Iran) na kuwaombea subira watu waliopata hasara na waliopoteza jamaa zao kwenye tukio hilo.
Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bisimillahir Rahmanir Rahim
Nimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa habari ya kutokea zilizala katika mkoa wa Bushehr na kusababisha hasara za roho, za watu na mali.
Ninawaombea dua za kheri, rehema na maghufira wale wote waliopoteza maisha yao kwenye tukio hilo, na ninamuomba Mwenyezi Mungu awape subira na ujira mwema wale wote waliojeruhiwa na kupoteza mali na jamaa zao kutokana na tukio hilo la kuhuzunisha.
Ninamwomba Mwakilishi mheshimiwa wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih), waheshimiwa viongozi wa mkoa huo na maafisa husika wote mkoani humo na nje yake, wafanye juhudi zao zote ili kuwaokoa watu waliojeruhiwa na kukwama na vile vile wawasaidie katika kuziba pengo la hasara walizopata na ni matumaini yangu kuwa wananchi azizi na wa maeneo yote nchini nao kama ilivyo kawaida yao watajitokeza kwa wingi na kutoa mchango wao mkubwa ili kuwapunguzia majonzi wahanga wa mtetemeko huo wa ardhi.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullah.
Sayyid Ali Khamenei
20 Farvardin 1392 (Hijria Shamsia)
(09/04/2013).
 
< Nyuma   Mbele >

^