Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Miongozo ya Kiongozi Muadhamu Nyumbani kwa Marhum Ayatullah Khushvaqt Chapa
20/02/2013
Ifuatayo ni hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa nyumbani kwa marehemu Ayatullah Khushvaqt mbele ya hadhara ya jamaa na wapenzi wake.


Ninatoa mkono wa pole kwa watoto, familia, kwenu nyinyi nyote na kwa watu wote wa masuala ya kimaanawi, ya maarifa na ya kujikurubisha na kumjua Mwenyezi Mungu kutokana na kuaga dunia Janabi Bwana Khushvaqt. Kwa kweli kama mtu ataathirika, atalia na ataungulika inapasa iwe ni kwa sababu ya (kufikiria) hali yake mwenyewe. Yeye (Ayatullah Khushvaqt) ni mtu ambaye aliishi umri mrefu na wenye baraka na wote huo katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; maisha safi na yenye nuru. Tangu mwanzo wa ujana yeye alikuwa katika njia hii ya tauhidi, njia ya maarifa (ya kumjua Mwenyezi Mungu) na njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Hadi mwisho wa umri huu mrefu hakusimama hata kwa lahadha ndogo katika njia hii bali alipiga hatua mbele. Inshallah Mwenyezi Mungu Mtukufu atajaalia amali zake na yeye mwenyewe wawe pamoja na amali za waja wema na amali za mawalii inshallah. Ndipo tukaambiwa: Basi jifanyieni maombolezo wenyewe enyi mlioko usingizini!
Ni matumaini yangu kuwa inshallah baraka za janabi Khushvaqt hazitotukatikia sisi na nyinyi bali zitaendelea. Baada ya kujivua na pingu za kimaada na umaada, roho za waja wema wa Mwenyezi Mungu huwa na uwezo mkubwa zaidi; zinaombea dua, zinaombea msaada na zinaombea uongofu. Kama tutaweza kudumisha na kuutunza uhusiano nao ni kwa manufaa yetu. Tuweze kudumisha uhusiano wetu na wao (waja wema) ili tunufaike na dua zao na baraka zao inshallah. Inshallah Mwenyezi Mungu aiinue daraja yake, na kwa kweli kuondoka kwake kunahisika mno ndani ya chumba hiki.
Ahsanteni sana!
 
< Nyuma   Mbele >

^