Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba Mbele yua Wajumbe wa Tume ya Maandilizi ya Semina ya Kumuenzi Allama Ni'matullah Jazayiri Chapa
25/02/2013
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mkutano na wajumbe wa tume ya maandalizi ya semina ya kumuenzi Allamah Sayyid Ni'matullah Jazayiri uliofanyika asubuhi ya Alkhamisi ya tarehe 10 Esfand ulisomwa katika mkutano huo uliofanyika mjini Shushtar na Ayatullah Sayyid Muhammad Ali Musawi Jazayiri, mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika mkoa wa Khuzestan na Imamu wa Ijumaa wa Ahwaz
Bismillahir Rahmanir Rahim
Ninamshukuru sana janabi bwana Jazayiri na mabwana wengine waliosalia ambao wamefikiria kumuarifisha shakhsia huyu mkubwa na asiyejulikana. Ni asiyejulikana kwa sababu japokuwa marehemu Sayyid Ni'matullah Jazayiri ni maarufu kwa vitabu viwili: Zahrur Rabi'i na Anwarun Nu'maniyyah (Al Anwarun Nu'maaniyyah Fii Bayaani Ma'rifatin Nash - atil Insaniyyah) lakini hadhi yake ni kubwa zaidi ya hiyo. Yeye alikuwa faqihi pia - marehemu Sayyid Ni'matullah ni faqihi mahiri - na vilevile alikuwa mpokezi wa hadithi mwenye mapokezi mengi na ya uwanja mpana katika vitabu vya Akhbariyyun lakini pia alikuwa mwanafasihi. Ajabu ni kwamba familia yao ni familia ambayo mbali na kutabahari kwenye fiqhi na hadithi ni watu wa fasihi pia, isimu n.k. Marehemu Sayyid Nuruddin - mwanawe (Sayyid Ni'matullah) - ameandika kitabu mashuhuri cha Furuqul Lughat (Furuuqul Lughaat Fiit Tamyiz baynal Mufradaat) ambacho si kitabu cha isimu tu, bali kinaonyesha kutabahari kwake kikamilifu katika isimu ya Kiarabu. Mjukuu wake pia ni marehemu Sayyid Abdullah Jazayiri; yaani vizazi vitatu, kimoja baada ya kingine, ni miongoni mwa maulamaa wakubwa na mashuhuri na wanaojulikana barabara katika hawza za elimu (vyuo vikuu vya kidini). Tab'an shakhsia hao wote watatu wakubwa walikuwa Akhbariyyun; marehemu Sayyid Abdullah kwa kiwango kikubwa na Sayyid Ni'matullah na Sayyid Nuruddin kwa kiwango kidogo; lakini licha ya marehemu Sayyid Ni'matullah kuwa mwanazuoni wa Akhbariyyun lakini anazipa uzito pia rai na maoni ya wanazuoni wa Usuliyyun na anacho kitabu pia - kwa sasa silikumbuki jina lake - kuhusu ulazima wa kurejea kwenye vitabu vya mafaqihi; na tab'an makusudio yake kuhusu mafaqihi ni mafaqihi wa Usuliyyun. Yeye ni mtu mkubwa. Athari na maandishi yake ni mengi. Janabi wewe umeeleza ni karibu maandishi sitini; lakini kwa ninavyokumbuka akilini mwangu nilikuwa nikijua kwamba yeye ana maandishi yapatayo arubaini; na kati ya hayo ni sherehe muhimu za vitabu vyetu vinne - yaani yeye ameandika sherehe za Tahdhib, sherehe ya Istibsar, na nadhani ana sherehe ya Al Kafi pia - ana sherehe za vitabu vingi vya (Sheikh) Sadduq - kama Tauhidi ya Sadduq na mfano wa hicho. Yaani yeye ni shakhsia mmoja mkubwa sana aliyetabahari na kubobea kwenye hadithi za Shia pamoja na kuwa na mtazamo makini wa kifiqhi na si hadithi tu. Yeye ni mwanafunzi wa Allamah Majlisi. Na Allamah Majlisi ni mtu mkubwa sana, yaani mtu anapoangalia maelezo yake ndani ya Bihar katika kiambatisho cha hadithi ataelewa kwamba mtu huyu ni faqihi, mtaalamu wa Ilmul - kalam na vievile ni mtu wa elimu ya mantiki. Majilisi ni (mtu) mkubwa sana lakini amekuwa mashuhuri zaidi kwa hadithi hali ya kuwa hayuko hivyo tu. Yeye ni mpokezi wa hadithi - na kitabu chake cha hadithi, Biharul Anwar, ni kitabu kikubwa - lakini pia ni faqihi wa Ilmul kalam mwenye rai; baadhi ya rai zake alizotoa ni za kipekee katika masuala ya Ilmul kalam na mantiki katika viambatisho vya hadithi. Hizo zinaonyesha jinsi alivyo shakhsia mkubwa. Marehemu Sayyid Ni'matullah ni mwanafunzi wa mtu kama huyu, ni mwanafunzi wa marehemu Allamah Majlisi. Inavyoonekana ni mwanafunzi wa Faidh pia, nadhani alikuwa mwanafunzi wa Faidh pia. Alaa kulli hal yeye ni shakhsia mkubwa.
Kitabu cha Zahrur Rabi'i japokuwa ni kitabu ambacho katika hawza za elimu ni maarufu zaidi kama kitabu cha vichekesho na masuala kama hayo lakini ni kitabu kinachoonyesha kuwa mafakihi wetu, shakhsia wetu wakubwa na maulamaa wetu, wakati walipokuwa wakifanya kazi kubwa za kielimu na kifiqhi, walikuwa wakiyazingatia pia masuala kama haya. Yaani mwanzoni mwa Zahrur Rabi'i - huenda sisi tangu miaka hamsini hadi sitini nyuma tumekuwa tukiiangalia Zahrur Rab'i - anasema nimehisi wanafunzi wa kidini wanahitaji kitu cha kuburudisha na kuchekesha kwa hivyo nimekiandika kitabu hiki kwa ajili yao; yaani yeye ameandika kitabu ili mwanafunzi wa kidini, ambaye amezama kwenye kazi za kielimu katika madrasa na chumbani mwake na sehemu kama hizi, awe na kitu cha kumburudisha na kumchekesha; yaani yeye hakughafilika na vitu hivi. Sasa sisi na tukae hapa kirasmi tu hata akitokea mtu pale akafanya mzaha kidogo mara tushakereka! Maulamaa wetu hawakuwa hivi, tena basi kwa mtu aalim kama Sayyid Ni'matullah ambaye tena alikuwa mtu wa Akhbariyyun mwenye misimamo migumu na masuala kama hayo; lakini pamoja na hayo alikuwa na mambo haya pia. Kwa maoni yangu hivi vitu vya burudani (vya kujishughulisha na mambo ya ziada ya kielimu mbali na yale ya asili) vya maulamaa wetu waliopita vina umuhimu sana; na mfano wake mmoja ni hiki kitabu cha Furuqul lughaat ambacho nilisema kwamba Sayyid Nuruddin - mwanawe yeye - pamoja na kwamba ni faqihi, pamoja na kwamba ni mpokezi wa hadithi, ni mwanafuzi wa baba yake lakini wakati huohuo aliandika pia kitu kama hiki katika uwanja wa isimu. Alaa kulii hal kwa maoni yangu marehemu Sayydi Ni'matullah ni shakhsia mkubwa.
Na ukoo wenyewe pia ni ukoo wa elimu. Alhamdulillah hadi leo hii pia ukoo huu ni ukoo wa elimu, na tunatumai kwamba utaendelea kuwa hivi daima. Na kumuenzi yeye ni kuienzi elimu na kuenzi mafundisho ya kidini; ni jambo zuri sana kuwaarifisha shakhsia hawa adhimu. Na hasa kama mtaweza kuvihakiki na kuvichapisha vitabu vyake. Tab'an Anwarun Nu'maaniyyah kimesharudiwa kuchapishwa mara kadha wa kadha, kitabu kile ni kitabu maarufu lakini vitabu vyake vyengine havipatikani, yaani vitabu vyake vya hadithi na sherehe alizoandika kuhusu hadithi hazijapewa umuhimu mkubwa. Inshallah mpate taufiki na mafanikio. Ninamshukuru pia janabi Hussaini (Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu ambaye alihudhuria kikao hicho) ambaye anatoa msaada katika kazi hizi.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullah.
 
< Nyuma   Mbele >

^