Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu baada ya Shughuli ya Upandaji Miti Chapa
05/03/2013
Bismillahir Rahmanir Rahim
Inshallah upandaji miti, iwe ni katika siku hii na masiku haya yanayojulikana kama Siku ya Upandaji Miti au katika siku nyinginezo ambazo inawezekana pia kupanda miti, uiletee nchi baraka na ustawi. Na huu ndio ukweli wa kadhia yenyewe kwamba mimea na miti ni chachu ya baraka kwa kila nchi na kwa kila majimui yoyote ile ya watu; na ndiyo maana katika sharia tukufu za Uislamu na katika hadithi zetu limeusiwa suala la upandaji miti, utunzaji miti na kuzuia ukataji miti. Kwa hivyo hivi ndivyo ulivyousia Uislamu. Leo hii watu wote duniani wanalipa umuhimu suala hili na pengine tunaweza kusema watu na jamii za watu wamekuwa daima wakilipa umuhimu suala la upandaji miti. Pamoja na hayo dukuduku na manung'uniko ambayo inapasa niyatoe kwa majimui ya viongozi wanaohusika na suala la miti, upandaji miti, misitu na mfano wa hayo ni kwamba sisi hapa tunapanda mti mmoja mmoja lakini kuna mamia na maelfu kwa maelfu ya miti inakatwa bila ya sababu katika mahala ambako isingepasa kukatwa; hili ni tatizo kubwa sana lililopo. Zaidi ya hayo ni kwamba maeneo ya miti na ya mandhari za kijani zilizopo kandokando ya miji mikubwa yamechukuliwa kimakosa na kuporwa na watu waliotaka kuzitumia vibaya ardhi na ambao wangali wanaendelea kufanya hivyo kwa kuyageuza maeneo ya kijani kuwa ya saruji na vyuma (kujenga majengo) na vitu kama hivyo - na huu ni msiba kwa miji - hali ambayo imehatarisha na inaendelea kuhatarisha mno maeneo ya misitu nchini; na kuna ulazima mkubwa wa kuizuia hali hii. Hili ni jukumu la serikali, ni jukumu la bunge, ni jukumu la mabaraza ya miji na vilevile ni jukumu la idara ya mahakama; kila moja inapaswa kuzuia kwa namna moja au nyengine kuendelea kwa harakati hii isiyo sahihi ambayo kwa masikitiko inashuhudiwa leo hii katika nchi yetu.
Ili kuihifadhi misitu tunahitaji sheria na kanuni - sheria hizi hazipo kwa sasa - na pia tunahitajia irada madhubuti na azma thabiti ya kuzuia na kudhibiti utwaaji wa ardhi kandokando ya miji ya mikubwa ambazo kuna watu wanazichukua na kuzibadilisha kuwa majengo na mafleti ya maghorofa makubwa. Tabia hii mbali na kusababisha matatizo mbalimbali ya kibinadamu na kiutu, madhara yake ya kwanza ni kuangamiza mazingira ya mandhari za kijani kandokando ya miji ambayo ni hewa ya kupumua kwa ajili ya miji. Sasa hata kama nyinyi katika mji mtakwenda kujisumbua kupanda mche mmoja mmoja majumbani kwenu, kufanya hivyo ni wapi na wapi na suala la mji wote kuzungukwa na majimui ya mazingira ya kijani? Hata kama kuna kazi nzuri pia zimefanyika, kandokando ya miji kuna kazi zilizofanywa za uoteshaji misitu - na haifai kulikana hilo - lakini vile vitu ambavyo ndiyo utajiri wa asili wa nchi ambayo ni maeneo ya kijani ya kandokando ya miji, konde na bustani za ndani ya miji na hususan miti, inapasa iendelee kuhifadhiwa. Shirika la Hifadhi ya Mazingira, vyombo vingine husika vya serikali na vilevile wakuu na wawakilishi wa bunge, wakuu wa idara ya mahakama - na kwa upande wa miji na maeneo ya mipaka ya miji, manispaa - nchini kote wana wajibu wa kulifuatilia suala hili. Tunarudia kila mara kulizungumzia suala hili lakini pamoja na hayo hakuna kazi sahihi iliyofanyika! Kwa hivyo inshallah watu wote wafanye hima ili kazi hii ambayo wote wanakubali kuwa ni ya lazima na ya sawa iweze kufanyika.
Kwaherini waheshimiwa.
 
< Nyuma   Mbele >

^