Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Katika Darsa ya Khariji ya Fikihi Chapa
11/02/2013
Ifuatayo ni matini kamili ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei aliyoitoa katika darsa ya Khariji ya Fikihi katika siku ya tarehe 11/02/2013.

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

Hamdu zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe pia. Na rehema za Allah na salamu Zake zimfikie Bwana wetu Mtume Mtukufu Muhammad SAW pamoja na Aali zake watoharifu, wateule hususan baqiyatullah (Imam Mahdi Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) katika ardhi.
Na miongoni mwa maneno yake SAW: " Watu ni mfano wa madini, kama yalivyo madini ya dhahabu na fedha."
Kile ambacho kiko katika hadithi hii tukufu, fupi lakini iliyobeba maana kubwa ni uwepo wa vipaji vilivyojificha katika kila mtu miongoni mwa watu katika jamii. Sasa kuna baadhi ya watu wanaunganisha suala hili na mjadala wa Hiyari na Kutokuwa na Kutokuwa na Hiyar (Al-Jabr-Watafwidh); kwa hakika kufanya hivyo ni kujiweka mbali na muhtawa pamoa na maana wadhiha na ya kidhahiri kabisa ya hadithi hii tukufu. Kwa hakika hadithi hii inataka kusema kwamba: Kama ambavyo katika madini yaliyopo kuna (madini ya aina tofauti tofauti yaliyopo leo) dhahabu na fedha - sasa hapa yametajwa mawili kama mfano tu; kuna madini tofauti tofauti na anuwai kwa anuwai - na dhahiri ya kazi, ni jiwe, udongo, ardhi.
Ukitazama kijuujuu (kidhahiri) hakuna kitu kinachohisika na kuonekana wazi lakini kama utafanya uchunguzi, kama utakuwa unafahamu na kujua thamani chini ya jiwe hjli hili (unaloliona) na udongo huu wa kawaida, bila shaka utapata kito chenye thamani kubwa ambacho thamani yake kidhahiri haiwezi kulinganishwa na kile ambacho kinaonekana kidhahiri. Wanaadamu pia nao wako namna hii; kuna hali ya kidhahiri ambayo inaonekana katika harakati, maneno, muamala na vitendo vya wanadamu, haya ni mambo ambayo mtu anayashuhudia; lakini wakati huo huo, kuna hali ya kibatini ambayo ni mrundikano wa vipaji ambavyo Mwenyezi Mungu amempatia mwanaadamu. Tab'an, vipaji hivi haviko sawa na havilingani - kama ambavyo madini pia hayalingani - lakini kuna mshabaha kutokana na kuwa, kile ambacho kiko katika batini ya mwanadamu kina thamani kuliko kile ambacho mtu unakishuhudia kidhahiri.
Vile vile kama utafanya kazi katika madini, ukafanya hima na kufanya idili, unaweza kufikia kile kito chenye thamani, katika suala la mwanaadamu pia hali iko namna hii pia; kuna haja ya kuweko hima na juhudi; kuna haja ya kuweko watu ambao watafanya juhudi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, vipaji hivi vinafanyiwa kazi. Sharti la lazima katika hili ni nyinyi kuijua mada hii. Mtu ambaye yeye hajui dhahabu au fedha ni nini, endapo atapata dhahabu katika madini haya, kwa kuwa hafahamu, hatoyapa umuhimu na kuyazingatia madini hayo ya dhahabu. Ni lazima mjue dhahabu ni nini na ina thamani gani, kisha muende kuchimba migodi kwa ajili ya kuitafuta, mfanye hima na kujituma katika uwanja huo kwa ajili ya kupata dhahabu. Kwa mwanadamu pia hali iko namna hii. Walezi wa wanadamu, walezi wa watoto hususan vijana ambao wanataka kustafidi na vipaji hivi vilivyoko katika ujudi wa watu ambavyo ni tunu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wanapaswa kufahamu vipaji hivi, watambue thamani ya vipaji hivi na kisha baadaye wachukue hatua za kuviendea na kuvifuatilia. Kama ambavyo sisi tunakwenda katika uga wa masuala ya utambuzi wa ardhi na kufanya utafiti ili tuone je ardhi hii ina madini au haina, madini yake ni yapi (ya aina gani), ukubwa wake, pesa, yake, kiwango na thamani yake ikoje na njia ya kuyapata madini hayo ni ipi, kuhusiana na wanadamu pia hali iko namna hii. Baadhi ya vipaji ni mahiri na ni vingi na vikubwa; lakini baadhi yake ni vidogo na vichache. Aina ya vijana pia nayo ina tofauti; kuna mahala dhahabu ni lazima (yaani inahitajika na hali yake ya kuhitajika ni ya lazima) na yenye kuhitajika na mahala pengine (hapana) panahitajika fedha; mahala ambapo mnapaswa kutumia fedha mnapaswa kutumia na kustafidi na madini hayo na endapo hapa mtatumia dhahabu hamuwezi kufikia natija; mahala ambapo ni lazima mtumie chuma mnapaswa kufanya hivyo; kwani kama mtatumia dhahabu hamuwezi kufikia natija maridhawa na matulubu; hivyo basi kila moja (kati ya madini haya) yana kazi yake.
Wanaadamu nao kwa upande wao wana vipaji vinavyotofautiana yaani vya anuwai kwa anuwai na kwa vipaji vyao hivyo, wanaadamu hao hudhamini mahitaji na hawaiji za jamii ya mwanaadamu kwa ajili ya kuelekea katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuelekea katika njia ya ukamilifu; vipawa vyote hivi vinapaswa kuchimbuliwa. Kwa hakika hili ni jambo ambalo linalifanya jukumu la walezi wa jamii kuwa zito; linayafanya majukumu ya tawala kuwa mazito na magumu. Kuchimbua vipaji, kulea vipawa, kutambua vipaji, kutambua thamani ya vipawa, njia ya kuvitoa na kuvichumbua vipaji hivyo na kujua namna ya kuvitumia na kisha kuvifuatilia kwa nguvu zote, hiki ni kitu ambacho kitakuwa na natija kwa kudhihiri na kujitokeza vipaji; kwa hakika Mitume wa Mwenyezi Mungu waliifanya kazi hii. Kwa hakika Mitume wa Mwenyezi Mungu walikuwa wakichimbua vipaji vya watu. Kwa msingi huo basi: " Watu ni mfano wa madini, kama yalivyo madini ya dhahabu na fedha." Hivyo basi haipasi kumtazama mtu kwa jicho la kumdhalilisha na kumdunisha; kwani ana kipaji ambacho jamii ya mwanadamu inakihitajia.
Ndio, kuna baadhi ya watu wanakuja duniani na kuishi kwa muda wa miaka sabini au themanini na kisha kwenda zao (kufariki dunia), lakini vipaji vyao havigunduliwi; kimsingi ni kuwa, watu hawa hudhulumiwa, yaani watu hawa huwa wamedhulumiwa. Kama vipaji vyake vingegunduliwa, yamkini angeondokea kuwa mtu stadi mwenye kipaji na mahiri. Hili ni jukumu la walezi wa jamii wakiwemo masheikh, walimu, vyombo vya serikali na tasisi pamoja na vituo mbalimbali na tofauti vya malezi. Isije vipaji hivyo vikadharauliwa na kupuuzwa.
Kabla ya kuingia katika maudhui, kwa hakika ninaona kuna ulazima wa kuashiria na kutaja tukio hili adhimu lililofanywa na taifa la Iran katika tarehe 22 Bahman (siku ya kumbukumu ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu) ambayo ni Bahman ya 35 na kwa hakika nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa ujazi na neema hii kubwa; kwa hakika ni tukio la kustaajabisha. Nyinyi tazameni na kutupia jicho hizi nchi ambazo zimefanya mapinduzi, muone zinakumbuka vipi maadhimisho ya mapinduzi yao; ni ya kasi sana, baada ya miaka miwili au miaka mitatu huja na kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya mapinduzi, huja baadhi ya watu wakasimama kule, kisha waje watu wengine na kufanya gwaride mbele yao; kama vile vikosi vya kijeshi na kadhalika. Lakini hapa nchini Iran kazi hii iko katika mabega ya wananchi (ni ya wananchi); hapa nchini Iran wananchi wenyewe hujitokeza uwanjani, wananchi ndio wenye mapinduzi; wananchi wanajiona na kujitambua kwamba, nchi ni yao na ni mali yao; na kwa hakika huu ndio ukweli. Hii kwamba, sisi tunamshukuru mwananchi mmoja mmoja - ambapo hili ni jukumu langu na mfano wa watu kama wangu ambao kwa hakika tunapaswa kushukuru - sio kwa maana kamba, sisi tuko karibu zaidi na mapinduzi kuliko wananchi, hivyo ndio maana tunawashukuru wananchi kwamba, mumesaidia mapinduzi; hapana, mapinduzi ni mali ya wananchi, nchi hii ni mali ya wananchi hawa na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mali ya wananchi hawa. Kazi bora na ustadi mkubwa na mahiri ni kwamba, wananchi wanalijua hili; na wamekuwa wakijitokeza kwa ushujaa, kwa kusoma alama za nyakati na kuja kuutetea huu utajiri wao adhimu (mkubwa) ambao ni chimbuko la izza na mamlaka yao ya kujitawala; yaani mahala wanapotakiwa wawepo basi hujitokeza bila kusita na kutangaza uwepo na mahudhurio yao; bila shaka mumeona jana mjini Tehran na katika miji mbalimbali ya nchi hii jinsi wananchi walivyojitokeza kwa kwa wingi; kwa hakika hili ni tukio muhimu sana, na mliona jana jinsi walivyojitokeza uwanjani; kwa hakika hili ni tukio la kustaajabisha, hili ni tukio muhimu sana. Kwa hakika sisi kuna matukio mengi ambayo tumeyazoea; kama ambavyo tumezoea kuchomozwa kwa jua na tunadhani kwamba, hili ni jambo la lazima na hivyo hatulizingatii na kulipa umuhimu. Bila shaka kuna umuhimu mkubwa kwamba, baada ya kupita miaka thelathini na nne ya hii tarehe 22 Bahman, (katika maandamano ya kumbukumbu ya tarehe 22 Bahman siku ya kukumbuka ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran) bado wananchi wanajitokeza namna hii katika medani, wake kwa waume, wazee kwa vijana tena kutoka katika maeneo mbalimbali, wakiwa ni watu wa matabaka tofauti, watu wa kila aina na kila namna na kutoka kila sehemu, watu wote hujitokeza (katika maandamano ya kumbukumbu ya tarehe 22 Bahman siku ya kukumbuka ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran); kwa hakika hii ni neema kubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu. Kama mtu atajitahidi na kufanya hima ya kulishukuru hili katika umri wake wote, bado atakuwa hajaweza kumshukuru Mwenyezi Mungu kama inavyotakiwa. Na vile vile tunapaswa kuwashukuru wananchi mmoja mmoja; kwa hakika wamefanya kazi kubwa sana, tena wa wakati (unaofaa na mwafaka) na mahala pake. Kwa hakika wananchi wamejitokeza katika wakati mwafaka na unaofaa yaani katika kipindi ambacho maadui wa taifa hili (Marekani na witifaki wake), maadui wa mamlaka ya kujitawala nchi hii, maadui wa izza na heshima ya nchi hii walikuwa wakitaraji kwamba, wananchi wa Iran hawatoitikia (kwa sauti moja ya ndio) wito wa mapinduzi na wito wa Jamhuri ya Kiislamu na hivyo washuhudie hali ya mtengano baina ya wananchi, mfumo wa Kiislamu na Uislamu, wananchi walijitiokeza kwa wingi na kuwa na mahudhurio yasiyo kifani na hivyo kumkwamisha adui na kumkatisha tamaa. Tab'an, katika propaganda, maadui wanajikakamua na kujitahidi kutolionesha hilo (ya kwamba, wamekwama katika mipango yao) lakini wanafahamu vyema. Hiki ndicho kitu ambacho nyinyi muliokiona na kukishuhudia katika mahudhurio makubwa ya wananchi yaliyoleta hamasa kubwa, (katika maandamano ya kumbukumbu ya tarehe 22 Bahman siku ya kukumbuka ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran); wao pia wanaona, wanafahamu na wanatoa uchambuzi (kuhusiana na hili); hivyo wanafikia natija hii kwamba, haiwezekani kukabiliana na taifa la Iran.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa baraka Zake alishushie na kulimimnia taifa hili, rehma, fadhila na afya zaidi na zaidi na kuyaongeza haya siku baada ya siku.
 
< Nyuma   Mbele >

^