Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Alipokutana na Washairi Chapa
04/08/2012
Ifuatayo ni matini kamili ya hotuba ya Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa tarehe 04/08/2012 wakati alipokutana na malengo, magwiji wa lugha na fasihi ya Kifarsi na washairi vijana, katika hafla iliyofanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa "Karimu Ahlul Bayt" Imam Hasan bin Ali al Mujtaba AS.

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

Kama ilivyo daima, ndugu wapendwa malenga na washairi mumeifanya sikukuu yetu hii kuwa nzuri na yenye kuvutia zaidi; Inshallah Mwenyezi Mungu akujaalieni mafanikio mema. Mashairi yaliyosomwa, aghalabu yalikuwa mashairi mazuri na ya kutua moyoni; baadhi ya beti za mashairi hayo zilikuwa zimebeba maana kubwa mno. Tuna matumaini Inshallah, kafila (msafara) ya mashairi hususan mashairi ya rubaiyat (tungo za mashairi yenye mistari minne minne katika kila ubeti) itakwenda kwa kasi, kwa umakini na kwa muelekeo sahihi hapa nchini na kwa baraka za mashairi yenu nchi yetu azizi na lugha ya Kifarsi kwa mara nyingine tena iweze kutoa zawadi na adia yake yenye thamani kwa ustaarabu ulimwenguni hususan utamaduni wa dunia na hususan utamaduni wa kieneo. Napenda kutumia fursa hii kusema nukta mbili tatu hapa. Nukta ya kwanza ni kuwa, mashairi katika nchi yetu yamesonga mbele vizuri; isipokuwa kuna nukta moja muhimu na ya kimsingi; mashairi yanapaswa kuhudumia thamani na matukufu. Mimi sipingi wala kukanusha kwamba, mashairi ni hisia za mshairi, na mshairi ana haki ya kubainisha hisia zake, hisia zake za kimashairi na udiriki wake wa kishairi katika kalibu ya mashairi kwa mujibu wa kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu - mimi ninakubaliana na hili kikamilifu - isipokuwa fani ya mashairi ikiwa taaluma na sanaa ya juu na ikiwa neema na ujazi mkubwa wa Mwenyezi Mungu ina majukumu na ina masuuliya. Mbali na kubainisha hisia, mashairi yana majukumu na masuuliya. Kwa uoni na mtazamo wangu ni kuwa, masuuliya na majukumu haya katika mashairi ni kwamba, ni lazima mashairi yawe ni kwa ajili ya kuhudumia dini, mapinduzi, (thamani za) maadili na maarifa. Kama mashairi haya yatatekekeza jukumu hii, haki hupatikana; yaani hufanyika kazi ambayo ni ya haki, yaani kutakuwa kumefanyika kazi ambayo ni ya kiadilifu. Malenga na washairi wetu wanapaswa kuelekea upande huu, wafanye hima na idili na kuzivuta dhuku na hisia zao za ndani za kishairi katika upande huu. Tab'an, hii leo hususan katika kikao chetu hiki, kwa bahati nzuri vitu hivi vipo na sio vidogo; lakini mimi ninasisitiza na kutilia mkazo kwamba, kiujumla harakati ya kimashairi hapa nchini inapaswa kuhisiwa zaidi na mtu.
Tazameni, ni lazima jukumu la mashairi ikiwa kama sanaa na jukumu la mshairi (malenga) akiwa kama msanii lieleweke mkabala na ulimwengu, mkabala na Mwenyezi Mungu Mtukufu, mkabala na kufungamana na Uislamu na mapinduzi na jukumu hili litekelezwe kikamilifu. Jukumu hili ni kuwapeleka (kuwaongoza) waja wa Mwenyezi Mungu upande wa Mola Muumba na kuongeza kiwango cha maadili na maarifa ya jamii. Tab'an, mashairi yana jukumu jengine, lakini hilo ndilo la msingi na muhimu. Mashairi yanapaswa kuwa na uwezo wa kuhudumia maarifa ya wananchi, maadili ya watu na harakati ya mapinduzi ya taifa letu ambalo ni tukio tukufu, lenye thamani na la nadra kutokea. Kwa hakika haya ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika mashairi.
Tab'an, mimi ninaegemea katika mashairi ya rubaiyat (tungo za mashairi yenye mistari minne minne katika kila ubeti). Hii inatokana na kuwa, mashairi ya rubaiyat ni tungo za mashairi ambazo zina taathira kubwa, kwa msingi huo basi haya mafuhumu na maana ambazo tunataka kuzieneza katika jamii kupitia tungo za kishairi, basi ni bora kuzieneza kupitia mashairi ya rubaiyat (tungo za mashairi yenye mistari minne minne katika kila ubeti). Yamkini mtu akadhani kwamba, ni vizuri kama sisi tutakuja na kutunga beti za kishairi ambapo kuanzia mwanzo hadi mwisho tukazungumzia suala la akhlaqi (maadili) hii ni aina gani ya mashairi ya rubaiyat (mashairi ya mistari minne minne katika kila ubeti)? Sasa hisia zetu zitakwenda wapi? Kwa hakika mimi sisemi kwamba, nyinyi muwe kama mashairi ya Bidel, yaani kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mashairi ya rubaiyat mzungumzie irfani; au muwe kama yalivyo mashairi ya kiaklhaqi ya Saeb yaani katika beti kumi za mashairi ya rubaiyat, beti nane kati ya hizo mujaze mafuhumu za kiakhlaqi - tab'an, hii sio kazi ndogo ambayo mtu anaweza kuifanya - mimi ninasema kuwa, kama nyinyi mtaweza katika mashairi ya rubaiyat ya beti saba, mkaweka katika kila beti maana na madhumuni ya kiaklhlaqi au kimapinduzi au maarifa, mashairi haya ya rubaiyat yatakuwa ni rubaiyat (tungo za mashairi yenye mistari minne minne katika kila ubeti) ya kimapinduzi; rubaiyat hii itakuwa ni ya kiaklhaqi na itaacha athari zake. Jaalieni kwamba, kama mwalimu wa soma la hisabati wakati anaendelea kufunduisha atazungumzia katikati ya somo suala la Tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), uumbaji na umaasumu wa Mitume, mimi ninadhani kwamba, wakati mwingine athari ya hili huwa ni kubwa kuliko saa moja ya ufundishaji katika somo la dini. Mimi ninataka kutoka kwenu kuweko na hizi nukta na ugusiaji wa jambo katika mashairi yenu ya rubaiyat. Tungeni tungo zenu za mashairi ya aina hii, na bainisheni kila hisia yenu, huba, nishati na hamasa ambayo mnayo katika mashairi yenu haya yaani mwageni na wekeni kila mlichonacho katika beti zenu hizi za mashairi; isipokuwa katika mashairi yenu haya ya rubaiyat ya beti saba kwa mfano, chagueni beti mbili ambazo mtazungumzia humo madhumuni asili ya Uislamu, mapinduzi na maadili. Hii ni nukta moja, ambayo ni nukta muhimu sana.
Nukta nyingine ni hii kwamba, kwa hakika mashairi ya rubaiyat yanaegemea katika makole matatu: lafudhi, madhumuni na hisia. Haipaswi kudhoofishwa moja kati ya mambo haya matatu. Usiku wa leo ambapo makaka na madada wapendwa wamesoma mashairi yao ya rubaiyat, (tungo za mashairi yenye mistari minne minne katika kila ubeti) nimeona kwamba, kwa bahati nzuri lafudhi zimekuwa nzuri. Baadhi ya tungo za mashairi zinazotolewa na kusomwa na vijana wetu kwa upande wa lafudhi hayana uwezo (wa kilugha) unaotakiwa. Wakati mwingine watungaji wa tungo za mashairi hayo huwa na maana na madhumuni nzuri katika fikra zao, lakini hukosea katika maana ya lafudhi kilugha; yaani sio tu kwanza sio nzuri, bali ni makosa pia; yaani kitenzi kinapaswa kutabikishwa lakini hawatabikishi hilo kama inavyotakiwa. Wakati mwingine ishkali (mapungufu) iko namna hii. Hivyo basi, ni lazima mfanye hima katika mashairi ya rubaiyat - na mashairi kiujumla ingawa kwa sasa maudhui yetu hapa ni mashairi ya rubaiyat - yawe sahihi kilafudhi na vile vile vina na urari na vile vile mashairi hayo yawe imara na madhubuti katika maneno; yaani yawe na uimara na umadhubuti wa kilugha; na vizuri vile vile yawe na uzuri na hali ya kuvutia; kwani kwa vyovyote itakavyokuwa hii ni sanaa. Sanaa ya mashairi ndio hii. Hii ni kuhusiana na lafudhi.
Madhumuni nayo ni jambo muhimu. Kwa mtazamo wetu madhumuni ni jambo ambalo katu haliishi. Kwa hakika madhumuni si jambo ambalo linaisha; kwa sababu akili na fikra za mwanaadamu si zenye kwisha. Sisi tunafanya uvivu; tunafungamana na madhumuni ambayo watu wengine wameyabainisha na hivyo tunakariri haya haya; lakini ukweli wa mambo ni kuwa madhumuni na maana si jambo la kwisha na kumalizika. Wakati mwingine mtu anashuhudia katika mashairi ya vijana madhumuni na maana ambayo kwa hakika haina uzoefu wa hapo kabla; bila shaka hili ni jambo lenye thamani sana. Kwa muktadha huo maana na madhumuni haya yanapaswa kupewa uzito; yaani tuwe na hali ya kufuatilia maana na madhumuni. Inawezekana kupata na kuchukua maana na madhumuni katika maisha. Sasa kwa mfano katika zama za kale kulikuweko na vitu kwa mfano katika zama hizo kulikuweko na mshumaa, lakini leo kuna taa. Watu wa kale walikuwa wakitoa maana mia moja kuhusiana na mshumaa; nyinyi mnaweza leo kwa kufikiri na kutaamali mkatoa maana nyingi kuhusiana na mwanga na taa ya umeme. Tab'ani, mutwalaa wa ndani na wa kifikra una nafasi muhimu sana.
Jingine ni suala la hisia. Katika mashairi ya rubaiyat (mashairi ya mistari minne minne katika kila ubeti wa mashairi) suala la hisia ni muhimu; sasa hisia hiyo tunaipa jina la huba na mapenzi; lakini sio mapenzi; wakati mwingine ni huba na mapenzi na wakati mwingine ni kitu ambacho kiko dhidi ya huba na mapenzi; kwa mfano jaalieni kwamba, ni chuki; lakini ni hisia. Kwa hakika mashairi ya rubaiyat hayawezi kuwa ni mashairi ya rubaiyat bila ya kuweko hisia. Chungeni mielekeo hii mitatu. Wakati huo mafahimu - kama tulivyosema - yawe kwa ajili ya kuhudumia nguzo hizi tatu; yaani mapinduzi, akhladi (maadili) na maarifa.
Kuna masuala muhimu katika nchi yetu ambayo tungo za mashairi zinaweza kustafidi nayo na hivyo kuwa kwa ajili ya kuhudumia mafahimu (maana) haya. Mafahimu (maana) hayo nayo sio mafahimu ya kibinafsi; bali ni mafahimu ya kitaifa. Jaalieni kwamba, kuna dhulma kubwa ya nishati ya nyuklia ambayo tunafanyiwa. Ni kweli kwamba, hawatuui kwa umati mathalani kama (inavyofanyika) kule Myanmar; kutokana na kuwa hawezi kufanya hivyo; lau kama wangelikuwa wanaweza (wangekuwa na ubavu wa) kufanya hivyo basi wangelifanya; lakini hawana ubavu wa kufanya hilo; lakini mambo ambayo wanaweza kuyafanya katika kulidhulumu taifa hili na nchi hii (wamekuwa) wanayafanya. Vizuri, hii ni moja ya maudhui muhimu. Au jaalieni kwamba, wanawauwa shahidi wanasayansi (wataalamu) wetu wa nyuklia; kwa hakika hili sio tukio dogo, ni tukio muhimu sana. Hivyo basi hili ni suala la kitaifa na suala kubwa mno; haya ni mambo ambayo yanapaswa kuakisiwa vizuri (kubainishwa vizuri) katika tungo za mashairi. Kama ambavyo inawajia katika fikra zenu kwamba, ni lazima kwa mfano kuzungumzia katika tungo za mashairi suala la Myamnar au Misri au suala la mwamko wa Kiislamu au Palestina au vita vya siku 33 - ambapo mumekuwa mukiyazungumzia haya katika tungo zenu za mashairi hili ni jambo zuri na la lazima - masuala ambayo yako katika nchi yenu pia ni mambo ambayo hamuwezi kuyafumbia macho; haya ni masuala ambayo hayawezi kufumbiwa macho katika ulimwengu wa mashairi.
Vizuri, kuna baadhi ya watu ambao hawayapi umuhimu kabisa masuala ya nchi hii. Kuna watu ambao mimi nimewashuhudia ambao wanadai kuwa ni wazalendo na kwamba, wanaipenda nchi hii, lakini wakati huo huo hawayapi umuhimu masuala yanayohusiana na nchi hii. Nchi hii ilikuwa katika vita kwa muda wa miaka minane (vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na utawala wa dikteta Saddam); kwa hakika Iran haikuanzisha vita hivi (bali ilitwishwa na kubebeshwa vita hivi); yaani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ililazimishwa kupigana vita hivi. Vizuri, watu ambao wanapingana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, walipaswa kuchukua msimamo gani kuhusiana na vita hivi? Walipaswa kufanya nini? Serikali ni serikali ya Jamhuri ya Kiislamu; lakini taifa ni taifa la Iran; mji wa Dezful, Khorramshar, Tehran; kwa nini hili halikuwashughulisha? Kwa nini malenga na washairi mahiri, wasanii stadi, waandishi wa riwaya watajika, waandishi mashuhuri wa makala na wanafikra waliotabahari katika uga wa fikra na mitazamo hawakushughulishwa na haya? Kwa hakika haya ni mapungufu makubwa mno. Iran ni Iran; kwani adui hakuvamia na kuishambulia nchi hii? Kwa hakika watu hawa hawana la kujitetea. Utetezi pekee wanaoweza kuutoa na kujitetea ni kusema kwamba, wao ni wabaya kwa Jamhuri ya Kiislamu; na kwamba, taasubu hiyo ndio ambayo haikuwaruhusu kuizungumzia Iran, Tehran, Khorramshahr na vijana wa nchi hii katika mashairi yao au katika nathari zao. Kwa hakika huku kujitetea kwenyewe - ambalo ndilo jambo pekee wanaloweza kulifanya wahusika - ni aibu kubwa kabisa kwao ya kwamba, kuna taasubi kama hii ambayo imeganda na kutawala katika fikra, roho, nyoyo na kalamu zao.
Hii leo pia hali iko namna hii. Hii leo ninyi mnaona kwamba, kambi ya kiistikbari imesimama na kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na taifa la Iran kwa nguvu zake zote za kipropaganda, kisiasa na ukhabithi wa kila namna - sasa ni kwa kiwango gani propaganda zao hizo zina taathira au hazina taathira hiyo ni kadhia nyingine - lakini la msingi ni kuwa adui anafanya ukhabithi wake; na katu hazembei katika hili. Kwa hakika adui amesimama kukabiliana na taifa la Iran na nchi ya Iran na hivyo kuiridhisha roho yake khabithi na chafu; lakini taifa la Iran nalo linaendelea kupambana kiume na linaendelea na muqawama wake mbele ya uadui huo wa mabeberu. Vizuri hili ni tukio la kitaifa; je hili tukio la kitaifa inawezekana mkaliacha mbali na kulifumbia macho? Haya ni mambo ambayo yanapaswa kuakisiwa katika mashairi. Nimesema kwamba, mimi singang'aniii kwamba, mtunge beti hamsini za mashairi kuhusiana na kadhia hii; hapana hilo linawezekana hata kwa beti moja au mbili tu za shairi la kimapinduzi, kiakhlaki, kimaadili na lililobeba madhumuni na maana kubwa iliyojaa mafunzo, mazingatio na maarifa. Yaani tungeni kwa mfano mashairi ya beti saba au nane na katika mashairi yenu hayo muainishe ubeti mmoja au beti mbili kwa ajili ya kubainisha suala hilo. Haya ni mambo ya lazima. Vyovyote itakavyokuwa, katika suala la haki na batili bila shaka kuna haja ya kuchukua msimamo; haiwezekani mtu akakaa bila ya kuwa na msimamo wowote ule.
Suala la maadili nalo ni miongoni mwa masuala haya ambayo ni muhimu sana. Watu hao ambao wanafanya propaganda za kueneza fikra za kujihusisha na mambo ya kipuuzi, dharau na kutojali mafundisho ya kidini wala kimaadili na wala masuala ya kimsingi na ya kimapinduzi nchini, ndio hao hao ambao hawaonyeshi hisia zozote mbele ya adui wa kigeni anapoivamia nchi. Sasa katika mashairi ya Bwana Amiri, tumeshuhudia nukta hii, watu hawa ni watu ambao hawapingi suala la kutofungamana na matakwa ya wageni na mabeberu bali wanafungamana nalo.
Kwa muktadha huo kuna suala la kufungana lakini mfungamano huu ni mfungamano na adui. Mfungamano wa dini, maadili, maarifa na masuala ya nchi na mapinduzi kama vile ni nukta hasi ambayo ni lazima kuikwepa; hivyo basi wanaelekea katika mambo ya kipuuzi na kuita watu katika mambo hayo yasiyo na maana wala msingi wowote. Kuna haja ya kuwa na msimamo mkabala na haya na ni lazima watu wasimame kukabiliana na tishio dhidi ya dini, utamaduni na maadili ya jamii.
Niseme jambo jingine. Washairi wetu vijana - Inshallah Mwenyezi Mungu akulindeni na kukuhifadhini nyote na mimi ninasisitiza na kutilia mkazo kwamba, Inshallah endeleeni katika njia hii - kuweni makini na msije mkavutwa na kambi hasi na zenye madhara. Hivi sasa kuna juhudi zinafanyika katika hili. Baadhi ya hawa hawa watu ambao ni wenye mielekeo ya mambo ya kipuuzi na ambao hawana mfungano mzuri na mapinduzi, dini na utaifa - ambao linalojitokeza suala la kukabiliana na adui wa mapinduzi na adui wa nchi hii sio wabaya kiasi hicho; bali huwa na muelekeo wa kuwa pamoja na adui! - yamkini kimuonekana wakaonekana hawako hivyo.
Ala kulli haal, jichungeni na muwe makini mno na mhakikishe kwamba, mnalinda mistari, mipaka na viwango. Nyinyi ni kambi kubwa ambayo inatetea haki na maanawi; nyinyi mnafanya hima na idili kwa ajili ya kuuwekea mtaji haki na umaanawi; mnatumia mtaji wenu wa sanaa (fani ya mashairi); na baadhi yenu wanasema kuwa, wako tayari kutoa rasimali ya uhai wao. Kuweni makini na kuhakikisha kwamba, mnadumu katika kambi hii na bila shaka kusimama kidete ni jambo lenye umuhimu mkubwa na Inshallah mtafanikiwa kufikia natija maridhawa. Tuna matarajio kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuhifadhini na kukulindeni nyinyi nyote.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 
< Nyuma   Mbele >

^