Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi MuadhamuAwasilisha Siasa kuu za Mabadiliko katika Mfumo wa Elimu na Malezi Nchini Iran Chapa
30/04/2013
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika kutekeleza kipengee cha kwanza cha kifungu cha 110 cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewasilisha siasa kuu za kuleta mapinduzi na mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu na malezi wa Iran siasa kuu ambazo amezitoa baada ya kushauriana na Halmashauri ya Kulinda Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Matini kamili ya siasa kuu za "Kuleta Mabadiliko katika Mfumo wa Elimu na Malezi Nchini (Iran)" na ambazo wamepelekewa wakuu wa mihimili mitatu mikuu wa dola (Serikali, Bunge na Mahakama) pamoja na Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Siasa Kuu za Kuleta Mabadiliko katika Mfumo wa Elimu na Malezi Nchini
1 - Mabadiliko katika mfumo wa elimu na malezi yaliyosimama juu ya msingi wa falsafa ya utoaji elimu na malezi ya Kiislamu kwa shabaha ya kufikia kwenye maisha sahihi na bora (maisha yanayotakiwa na Uislamu ya watu binafsi na ya jamii nzima) na kukuza na kustawisha vipaji vya kimaumbile pamoja na kuimarishwa kiubora maeneo ya umaizi, elimu, umahiri na ustadi, malezi na usalama wa kiroho na kimwili wa wanafunzi sambamba na kusisitizia wajibu wa kupambana kikamilifu na kutojua kusoma na kuandika, kujali majukumu, kuheshimu sheria, kupigania uadilifu, kujipamba kwa hekima, busara, ubunifu, kupenda nchi, kupambana na dhulma, kupenda kazi za pamoja, kuwa tayari kujitolea wakati wote na kujiamini.
2 - Kunyanyua nafasi na ubora wa Wizara ya Elimu na Malezi kikiwa ni chombo muhimu cha kulea nguvu kazi na mzalishaji wa rasilimali ya kijamii na ambacho ndicho chenye jukumu la kutekeleza siasa zilizopasishwa, kuziongoza na kuzisimamia (kuanzia chekechea, shule za msingi hadi Vyuo Vikuu) likiwa ni suala la kiutawala na kwa kupitia kupanua wigo wa ushirikiano kati ya asasi mbali mbali husika.
3 - Uboreshaji na Uimarishaji wa vyanzo vya Wizara ya Elimu na Malezi ukiwa ni mhimili mkuu wa mfumo wa elimu na malezi nchini Iran na kuboresha uendeshaji wa vyanzo vya kibinaadamu kwa kusisitiza mambo yafuatayo:
3 - 1 - Kuongeza ubora wa mfumo wa malezi ya walimu na kuzidisha mtawalia ustahiki na uwezo wao wa kielimu, ustadi na malezi ya walimu na kuifanya ya kisasa mipango ya elimu ya taasisi na vyuo vya walimu na mbinu za usomeshaji na usomaji kwa ajili ya kulea walimu wenye mori, wanaofaa, waliopambika kwa dini, wabunifu na wenye taathira kubwa.
3 - 2 - Kuangalia upya mbinu za kuvutia watu, za malezi na kulinda nguvu kazi pamoja na kutumia vizuri nguvu kazi inayohitajika katika Wizara ya Elimu na Malezi na kuandaa mazingira mazuri ya kuvutia walimu bora na wenye ustahiki unaotakiwa kwa ajili ya kufundisha na kulea vizuri wanafunzi huku wakiwa wamepambika kwa maadili mazuri baada ya kupitisha masomo ya kiufundi na kiustadi.
3 - 3 - Kunyanyua nafasi na heshima ya walimu katika jamii na kuongeza hamu na mori wao wa kufanya kazi inavyotakiwa kupitia kazi za kiutamaduni, kitablighi na huduma bora pamoja na suhula za ustawi na kuwaondolea walimu matatizo yao ya kimaada na kimaisha.
3 - 4 - Kupanua umahiri wa kiutaalamu na uwezo wa kielimu na kimalezi wa walimu kupitia kuongeza ubora wa mafunzo sambamba na huduma na mipango mizuri ya kusasisha mara kwa mara taarifa za kitaalamu na za kumaliza masomo walimu kulingana na mahitaji ya Wizara ya Elimu na Malezi.
3 - 5 - Kuanzisha mfumo wa kutathmini na kuchunguza watu wanostahiki kuwa walimu katika jamii, kutathmini utaalamu na umahiri wa walimu kwa kuangalia vielelezo vya kielimu, kiutafiti, kiualimu na kimalezi kwa ajili ya ustawi mkubwa zaidi.
3 - 6 - Kupanua wigo wa kushirikishwa walimu katika kubuni na kuboresha mipango ya elimu, utafiti, malezi na utamaduni.
3 - 7 - Kuanzisha mfumo wa malipo kwa msingi wa utaalamu, ustahiki na utendaji wa kiushindani chini ya mfumo wa kuainisha kiutaalamu daraja za walimu.
4 - Kuleta mabadiliko katika mfumo wa kupanga mipango ya masomo na ufundishaji kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
4 - 1 - Kufanywa vya kisasa vitu vinavyotumika katika malezi na ufundishaji na kuandaliwa mpango wa kitaifa wa usomeshaji utakaosimama juu ya falsafa ya ufundishaji na malezi ya Kiislamu na ambao unakidhi mahitaji ya nchi na kutabikiana vitu hivyo na maendeleo ya kisayansi na kiteknoloji na kutilia hima suala la kuimarishwa utamaduni na utambulisho wa Kiislamu-Kiirani.
4 - 2 - Kuimarishwa na kustawisha utamaduni wa kutafakari, kufanya uhakiki, ubunifu na kuvumbua mambo mapya pamoja na kutumiwa mbinu za kila namna na bora za ufundishaji na usomaji na kuleta fikra ya kimantiki na yenye uratibu wa pamja kwa ajili ya kufanya utafiti, uhakiki na uchunguzi wa kimaudhui.
4 - 3 - Kubainisha fikra za kidini na kisiasa za Imam Khomeini (quddisa sirruh), misingi ya Jamhuri ya Kiislamu na Utawala wa Fakihi (Wilayatul Faqih) na misingi thabiti ya katiba katika mihula mbali mbali ya masomo.
4 - 4 - Kustawishwa na kutiwa nguvu utamaduni na maarifa ya Kiislamu na kujifunza Qur'ani (kuweza kuisoma, kusoma kwa kasi na kuelewa maana ya aya zake) na kuwatia hima na nguvu wanafuzni za kuipenda Qur'ani Tukufu pamoja na kupenda kusoma sira ya Bwana Mtume Muhammad (SAW) na Ahlul Bayt AS na kustawisha utamaduni wa kusimamisha sala.
4 - 5 - Kuleta Mapinduzi na mabadiliko makubwa na ya kimsingi katika mbinu za kutafuta thamani na matukufu ya wanafunzi kwa ajili ya kujua nukta zenye nguvu na nukta dhaifu na kulea vipaji, atia na vipawa vya wanafunzi.
4 - 6 - Kuzingatiwa na kupewa umuhimu mkubwa fikra ya kiutamaduni na kimalezi katika kupanga mipango mbali mbali ya masomo na ufundishaji.
4 - 7 - Kuimarisha mila na umahiri wa kuendesha maisha pamoja na uwezo wa kutatua masuala mbali mbali na kutekeleza mafundisho yanayotolewa kwa ajili ya kuwafanya wanafunzi waweze kujiimarisha kimaisha kila mmoja wao na kwa ujumla wao katika jamii.
4 - 8 - Kutiwa nguvu masomo ya ufundi na utaalamu.
5 - Kutilia hima malezi na mafunzo kwa kuzingatia falsafa ya usomeshaji na malezi ya Kiislamu hususan katika mambo yafuatayo:-
5 - 1 - Kunyanyua kiwango cha welewa na tabasuri ya kidini kwa ajili ya ukuzaji na uimarishaji wa kimaanawi na kimaadili wa walimu na wanafunzi na kufanya jitihada za kuziimarisha na kuzinyanyua familia kimaanawi.
5 - 2 - Kunyanyua kiwango cha usalama wa kimwili na kiroho kwa walimu na wanafunzi na kuzuia kutokea madhara ya kijamii.
5 - 3 - Kunyanyua daraja ya malezi ya kimantiki na kuongeza kiwango cha welewa wa kidini, kisiasa na kijamii wa wanafunzi na kutilia hima suala la kukubalika kijamii kwa ajili ya kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa, kupenda nchi na kukabiliana kwa busara na mashambulizi ya kiutamaduni, istikilali, uhuru, demokrasia ya kidini na manufaa ya taifa.
5 - 4 - Kukuza na kufanya zichanue dhuku na vipawa vya kiutamaduni na kisanii na kutia nguvu moyo wa nishati, uchangamfu, na furaha kwa wanafunzi.
5 - 5 - Kustawisha michezo na kujenga mwili mashuleni.
5 - 6 - Kulea na kudhamini nguvu kazi yenye uwezo mkubwa na iliyotimiza sifa za kuweza kufanikisha malengo na mipango ya malezi na mafunzo.
6 - Mabadiliko katika muundo wa kifedha, kiidara na mfumo wa uongozi kwa kusisitizia mambo yafuatayo:-
6 - 1 - Kujengwa upya muundo wa kiidara katika daraja zake zote kwa kujenga fikra ya kufanya mambo kwa haraka na kwa usafi sambamba na kuongeza uwezo, kujenga utamaduni na kuweka misingi imara kwa ajili ya kutia nguvu ushiriki wa wananchi na asasi zisizo za kiserikali kulingana na Katiba na siasa kuu za mfumo wa kiidara na wa elimu na malezi hususan kuandaa uwanja wa kushiriki walimu, familia, Hawza, Vyuo Vikuu, vituo vya kielimu na utafiti na asasi nyinginezo za umma na taasisi za utendaji katika suala zima la elimu na malezi.
6 - 2 - Kuzingatia vipaumbele katika bajeti inayohitajiwa na Wizara ya Elimu na Malezi katika bajeti za kila mwaka kwa shabaha ya kufanikisha malengo ya kazi zilizoainishwa katika Siasa Kuu za nchi.
6 - 3 - Kuimarisha usimamiaji wa vyanzo, masurufu na matumizi kwa shabaha ya kuongeza ubora na kutumiwa vizuri mfumo wa elimu na malezi.
7 - Kutumia vizuri anga, miundombinu majengo na vifaa vya shule katika kufanikisha malengo ya mfumo wa elimu na malezi ya Kiislamu kwa kutilia mkazo masuala yafuatayo:-
7 - 1 - Kuwekewa misingi mizuri, kuboresha, kupambwa na kuimarishwa na kuwekewa kinga mashule kwa kutumia misingi mizuri ya ujenzi wenye sura ya Kiislamu Kiirani, kutenga maeneo na kugawa maeneo hayo kulingana na mahitaji, kubuni na kujenga maeneo makubwa ya elimu na malezi na kupanua wigo wa kushiriki wananchi na asasi za uendeshaji wa miji katika kujenga na kutunza mashule.
7 - 2 - Kuanzisha vituo vipya maalumu kwa ajili ya elimu na malezi kulingana na ongezeko la watu na kuwawajibisha wajengaji wa vijiji na vitongoji kujenga maeneo yanayohitajika kwa ajili ya elimu na malezi.
7 - 3 - Kutoa kigezo na kielelezo kilicho wajibu kutekelezwa na Wizara ya Elimu na Malezi kwa ajili ya kujenga shule mpya.
7 - 4 - Kupatiwa mashule teknolojia ya upashaji habari na mawasiliano na kuandaliwa uwanja wa kutumiwa vizuri usomeshaji kwa kutumia teknolojia mpya mashuleni.
8 - Kuongezwa nafasi na uwezo wa shule wa kufanikisha shabaha na kazi zilizoanishwa kwenye kifungu cha kwanza cha siasa kuu na kutiwa nguvu inavyotakiwa na kwa njia sahihi na ya maana, Wizara ya Elimu na Malezi, familia, vyombo vya habari na jamii.
9 - Kutiwa nguvu kazi za Wizara ya Elimu na Malezi katika maeneo ya mipakani kupitia kuwapa nguvu walimu na wanafunzi wa maeneo hayo.
10 - Kudhaminiwa utulivu katika uongozi kwenye Wizara ya Elimu na Malezi kwa kutumia fikra bora na za kimapinduzi na kuyaepusha mazingira ya elimu na malezi kuathiriwa na mirengo ya kisiasa.
11 - Kuwepo utaratibu mzuri na wa pamoja baina ya malengo, sera, mipango na masuala ya utoaji elimu na malezi katika Wizara ya Elimu na Malezi, Wizara ya Elimu ya Juu na vyombo vingine husika.
12 - Kunyanyua nafasi ya Wizara ya Elimu na Malezi katika upande wa vielelezo vya kiidadi na kiviwango katika upeo wa kieneo na kimataifa kwa shabaha ya kufanikisha hati ya malengo ya miaka ishirini ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
13 - Kuweka mfumo mkubwa na mpana wa kuweza kuangalia, kusimamia, kutathmini na kudhamini ubora katika mfumo wa elimu na malezi.
 
< Nyuma   Mbele >

^