Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe kwa Mnasaba wa Kushiriki kwa Hamasa Kubwa Wananchi katika Uchaguzi wa 11 wa Rais Chapa
15/06/2013
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Khamenei ametoa ujumbe muhimu wa kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa hamasa kubwa katika duru ya 11 ya uchaguzi wa kihistoria wa Rais wa Iran na duru ya 4 ya mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji.
Katika ujumbe wake huo, Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria jinsi wananchi waumini na wenye ghera wa Iran walivyojitokeza kwa wingi mno na kwa sura ya kustaajabisha katika hamasa ya kisiasa ya uchaguzi huo na kukutaja kushiriki huko kwa wananchi kuwa kunaonesha jinsi wananchi wa Iran wanavyozidi kupevuka kisiasa na kuzidi kutia nguvu misingi ya demokrasia yao ya kidini sambamba na kubatilisha njama mbaya za maadui wanaolifanyia husda na kulionea choyo taifa hili.
Amesisitiza kuwa: Mshindi mkuu na halisi katika uchaguzi huo ni taifa kubwa la Iran ambalo kwa uwezo na msaada wa Mwenyezi Mungu limefanikiwa kupiga hatua kubwa madhubuti na kuwaonyesha walimwengu jinsi taifa hili lilivyo mithili ya kito kisichopenyeka na kuwaonesha pia walimwengu sura iliyojaa uchangamfu na isiyotetereka ya taifa hili na moyo wake uliosheheni matumaini na imani.
Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
Bisimillahir Rahmanir Rahim
Taifa azizi la Iran!
Medani ya hamasa iliyojaa hisia nzuri ya uchaguzi wa siku ya Ijumaa ya Khordad 24 (Juni 14) ulikuwa ni mtihani mwingine wenye maajabu mengi ambao umewaonyesha marafiki na maadui sura isiyotetereka na iliyojaa matumaini ya Iran ya Kiislamu. Kupevuka kisiasa kunakozidi kuongezeka na kuzidi kutiwaa nguvu kiukweli misingi ya demokrasia ya kidini nchini Iran ni uhakika unaomeremeta ambao umetimia kwa kujitokeza kwenu kwa wingi mkubwa na kwa mshikamano wa hali ya juu katika masanduku ya kupigia kura na kwa mara nyingine kumebatilisha uchawi potofu na ulioongezwa chumvi wa maadui wenye tamaa, choyo na husda.
Hamasa yenu hii kubwa imewaonyesha maadui mfungamano madhubuti uliopo baina ya Iran na Muirani na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu licha ya maadui hao kufanya mamia ya njama za kisiasa, kiuchumi na kiusalama ili kutaka kufifiliza au kupunguza kasi ya mfungamano huo mtakatifu.
Muirani muumini na mwenye ghera katika uchaguzi wa jana alionyesha uwezo wake mkubwa wa kukabiliana vilivyo na kwa hekima ya hali ya juu na vita vya kisaikolojia na waendeshaji wa siasa za kibeberu na kiistikbari. Ameonyesha uwezo wake huo adhimu kwa sura nzuri kabisa na kwa namna ya kipekee na kwa njia hiyo ameweza kuiwekea kinga nchi yake, manufaa yake ya kitaifa na mustakbali wake uliojaa juhudi na matumaini.
Mshindi halisi wa uchaguzi wa jana ni taifa kubwa la Iran ambalo kwa uwezo na taufiki wa Mwenyezi Mungu limeweza kupiga hatua madhubiri na kuwaonyesha walimwengu kito kisichopenyeka na sura yake iliyojaa harakati na iliyo imara na moyo wake uliosheheni matumaini na imani.
Mimi kwa unyenyekevu, adabu na utii mkubwa, ninanyenyekea mbele ya Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mjuzi na Mwingi wa hekima, na ninatoa mwito kwenu kuweka pembeni kambi za kisiasa na sote kwa pamoja tushirikiane katika kumtaja na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake hii kubwa aliyotuneemesha na ninatuma salamu zangu zilizojaa ikhlasi kwa Imam wa Zama, Imam Mahdi (Roho yangu iwe fidia kwake) na ninatoa mkono wa baraka kwa taifa azizi la Iran na kwa Rais mteule Janab Hujjatul Islam Walmuslimin Alhaj Sheikh Hasan Rohani na hapa ninapenda kumueleza yeye na matabaka yote ya wananchi masuala yafuatayo:
1 - Sasa hamasa ya kisiasa ambayo ilifikia kileleni siku ya Ijumaa ya Khordad ishirini na nne (Juni 14) imemalizika kwa ushindi wa taifa la Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Hamasa, moto na mchuano uliokuwepo katika siku na wiki za ushindani wa kisiasa na kampeni za uchaguzi ni vitu ambavyo inabidi viwekwe pembeni na mahala pake pachukuliwe na ushirikiano na urafiki, na wafuasi wa wagombea waliochuana kwenye mtihani huo mgumu waonyeshe hekima zao kwa kujipamba kwa hekima, welewa na maelewano. Hisia za namna yoyote ile, ziwe za furaha au zisizo za furaha hazipaswi kuwa sababu ya mtu kutoa maneno au kufanya kitendo kilicho nje ya hekima, busara na uungwana. Msiruhusu watu wasiolitakia mema taifa hili kutumia hisia za wananchi, kama wenzo wa kufanikisha malengo yao machafu. Umoja wa kitaifa, urafiki na kustahamiliana ndiyo ngao ya usalama wa nchi na ndio unaoweza kubatilisha njama zote za maadui.
2 - Rais aliyechaguliwa, ni Rais wa wananchi wote wa Iran. Watu wote wanapaswa kumsaidia na kushirikiana na Rais na wenzake katika serikali ili kufanikisha malengo makuu waliyoahidi kuyatekeleza.
3 - Hivi sasa na baada ya kupita wiki kadhaa za kuzungumza na kusikiliza, umefika wakati wa kazi na kutekeleza kivitendo ahadi zilizotolewa. Rais mteule, hadi kufikia siku ya kuchukua rasmi jukumu hilo, ana muda wenye thamani kubwa, na ni jambo la busara mno kustafidi na fursa hiyo kadiri inavyowezekana na kuanza mara moja kufanya kazi ambazo zinapaswa kufanya kwa ajili ya kuanza kubeba jukumu zito na hatari la Urais.
4 - Hamasa ya kisiasa ya uchaguzi isingeliweza kufanikiwa bila ya kushiriki, kushindana na kufanya juhudi wagombea wengine wa Urais. Ni wajibu wangu kuwashukuru kwa udhati wa moyo wangu, shakhsia wote wapendwa ambao wameingia kwenye medani hii na kuufanya uga wa ushindani katika uchaguzi huu kuwa na hamasa kubwa kutokana na jitihada zao kubwa zisizojua kuchoka na ninatoa mwito kwao wendelee kutoa michango yao katika nyanja tofauti za Mapinduzi na mfumo wa Kiislamu nchini.
6 - Vile vile ni wajibu wangu kutoa shukrani za dhati kwa matabaka yote ya wananchi ambao mara hii pia wameunda tukio jengine kubwa la kubakia milele, hususan marajii muadhamu na maulamaa wakubwa na watu wenye vipawa kutoka wa Vyuo Vikuu, na watu wenye ushawishi wa kisaisa na kiutamaduni ambao wametoa mchango wenye thamani kubwa katika kuwashajisha na kuwahamasisha wananchi wajitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo. Vile vile ninawashukuru kwa dhati maafisa wote waliosimamia na kuendesha uchaguzi wa rais na mabaraza ya miji na vijiji hususan Wizara ya Mambo ya Ndani na Baraza tukufu la Kulinda Katiba ambao wamefanya jitihada kubwa katika kipindi cha wiki kadhaa zilizojaa kazi za usiku na mchana na kutokana na uaminifu wao mkubwa hadi walipoutua mzigo huu mzito. Aidha ninawashukuru kwa dhati maafisa wote wachapa kazi waliodhamini usalama wa tukio hili nyeti lililofanyika kwenye nchi hii kubwa na pana sana na kuweza kudhamini usalama katika kila kona ya nchi. Vile vile ninazishukuru kwa dhati taasisi na vyombo vyote vilivyoshiriki katika kufanikisha jambo hili muhimu sana nikimuomba Mwenyezi Mungu awalipe wote ujira mwema.
6 - Ni wajibu wangu pia kuishukuru kwa dhati kabisa, taasisi ya utangazaji ya taifa na wahusika wote wapendwa kwa kuweza kuleta hamasa ya uchaguzi kwa mbinu zao za kisanii za ubunifu wa kila namna na kwa kuakisi kiukweli na kwa uwazi kabisa kwa walimwengu mirengo na fikra tofauti pamoja na malengo ya wagombea wa urais na namna uongozi unavyopatikana katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Ninaishukuru sana kabisa taasisi ya taifa ya utangazaji nikiwaombea malipo mema kwa Mwenyezi Mungu, wale wote waliochangia kufanikiwa suala hili.
Mwisho ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa utii na unyenyekevu kutokana na neema Zake kubwa kwetu na ninamtaja kwa wema Imam wetu mtukufu (Imam Khomeini - quddisa sirruh) na mashahidi na watu wanaojitolea kwenye njia ya haki, na ninamuomba Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu za utukufu mbele Yake nikimuomba pia Mwenyezi Mungu kwa heshima na matumaini, alipe taifa letu na nchi yetu mustakbali ulio bora kabisa.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullah.
Sayyid Ali Khamenei
25/ Khordad/1392
(15/Juni/2013).

 
< Nyuma   Mbele >

^