Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Waandaaji wa Kongamano la Taifa la “Mabadiliko ya Idadi ya Watu” Chapa
31/10/2013
Kiongozi Muadhamu Aonana na Waandaaji wa Kongamano la Taifa la “Mabadiliko ya Idadi ya Watu”Wasimamiaji na waandaaji wa "Kongamano la Taifa la Mabidiliko ya Jamii ya Watu na Nafasi yake katika Mabadiliko Mbali Mbali ya Jamii" wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
Katika mazungumzo hayo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria umuhimu wa suala la idadi ya watu na udharura wa kutengenezwa utamaduni wa kuwakinaisha watu wenye vipaji na wenye ushawishi na kuwafanya waone umuhimu wa mahitaji ya nchi katika suala zima la kuongeza idadi ya watu.
Vile vile amesema: Suala la sura ya ujana inayoonekana katika jamii ya nchi ni suala la kimsingi, la dharura na lenye umuhimu kubwa sana na kwamba nchi ambazo katika dunia hii zimekumbwa na mgogoro wa jamii ya watu vizee zina matatizo mazito ya kutatua migogoro inayotokana na jambo hilo na kuna udharura na wajibu wa kufanyika kazi kubwa, za kimsingi na muhimu kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
Mwanzoni mwa mkutano huo Hujjatul Islam Walmuslimin Agha Tehrani, mmoja wa wasimamiaji na waandaaji wa kongamano hilo ametoa ripoti fupi na kusema kuwa baada ya kupasishwa siasa na mikakati mikuu kuhusu kadhia ya idadi ya watu katika Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni, hivi sasa siasa na mikakati hiyo inajadiliwa katika Kamisheni ya Utamaduni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ili baada ya kujadiliwa na kuandaliwa muswada wake, muswada huo uweze kujadiliwa katika vikao vya wazi vya Bunge na kupasishwa kuwa sheria.
Kongamano hilo litafanyika tarehe 31 Oktoba, 2013, kwa hima ya kitengo cha utafiti cha Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini, (Quddisa Sirruh).
 
< Nyuma   Mbele >

^