Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Wasimamiaji wa Amali ya Hija Chapa
11/11/2013
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Wasimamiaji wa Amali ya HijaAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumatatu ameonana na maafisa na wasimamiaji wa amali ya Hija ya mwaka huu na kusema kuwa, ibada ya Hija ni atia na hadia kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni ibada ambayo ina upeo mkubwa usio na kifani kwa ajili ya kuleta maelewano kwenye ulimwengu wa Kiislamu katika mahitaji ya pamoja ya ulimwengu huo.
Amebainisha kuwa, moja ya matatizo makubwa uliyo nayo ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa ni matatizo ya kutwishwa, ya makusudi, ya kikhabithi na yenye lengo la kuwasha moto wa hitilafu na mizozo katika umma wa Kiislamu na kushadidisha ugomvi wa kimadhehebu kati ya Waislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia pia ulazima wa kuzingatiwa unyeti na mahitaji ya wakati tulio nao kwa ajili ya kutumia nafasi adhimu ya Hija na kuongeza kuwa, vyombo vya kibeberu na kikoloni vina historia ndefu ya kuchochea moto wa mizozo ya kimadhehebu kati ya Waislamu na hivi sasa inabidi fursa ya ibada ya Hija itumiwe vizuri kukabiliana na njama hizo.
Vile vile amesema, ugomvi wa vikundi vya kimadhehebu hautaishia tu baina ya Waislamu wa Kishia na Kisunni na kama maadui wa Uislamu wataweza kueneza na kuimarisha wanavyotaka chuki baina ya Waislamu hao, watakwenda mbali zaidi na kuchochea chuki na ugomvi ndani ya safu za Wasunni na Washia wao kwa wao.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha ameitaja fursa inayopatikana kwa ajili ya kuleta maelewano katika matakwa na mahitaji ya pamoja ya ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni uwezo mwingine wa kipekee uliomo kwenye ibada tukufu ya Hija na kusisitiza kwamba, kuna fursa nyingine nyingi zinazopakatikana katika Hija ambazo hazijajulikana na kwamba wasomi na wanafikra wana jukumu la kuzitafuta na kuzitangaza fursa hizo mpya.
Vile vile amewashukuru maafisa na wasimamiaji wa amali ya Hija wa Iran kwa kazi kubwa waliyoifanya mwaka huu katika kutoa huduma sahihi na za kimantiki kwa mahujaji na kuelezea matumaini yake kwamba neema kubwa na fursa zisizo na kikomo za ibada tukufu ya Hija zitaweza kutumiwa vizuri kuutumikia ulimwengu wa Kiislamu.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Hujjatul Islam Walmuslimin Qadhi Askari, mwakilishi wa Fakihi Mtawala na msimamiaji wa mahujaji wa Kiirani ametoa ripoti fupi kuhusu hatua mbali mbali zilizochukuliwa na Biitha ya Hija ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kustafidi na ibada ya Hija kwenye upande wa kiutamaduni, kimaanawi na kimataifa.
Kwa upande wake, Bw. Awhadi, Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran ametoa ripoti kuhusu kazi za kiutendaji na kiutekelezaji za Hija zilizofanywa na taasisi yake na jinsi taasisi hiyo ilivyofanya kazi za kuihudumia misafara ya Hija ya Kiirani mwaka huu.

 

 
< Nyuma   Mbele >

^