Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Mwanamichezo wa Kike wa Iran, Bingwa wa Wushu Chapa
11/11/2013
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Mwanamichezo wa Kike wa Iran, Bingwa wa WushuBi Maryam Hashemi, mwanamichezo kutoka Kermanshah nchini Iran ambaye ni bingwa wa dunia wa mchezo wa Wushu katika mashindano yaliyofanyika nchini Malaysia, leo (Jumatatu) ameonana na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumkabidhi medali yake ya dhahabu aliyoipata kwenye mashindano hayo.
Akizungumza na bingwa huyo wa dunia wa mchezo wa Wushu, Ayatullah Udhma Khamenei amemwambia: Umefanikiwa kuonesha shakhsia na utambulisho wa mwanamke Muislamu Muirani na kuthibitisha kwamba katika medani za michezo pia, mwanamke Muislamu anaweza kuhifadhi na kulinda vizuri Hijabu yake na mipaka ya dini yake ni kutwaa ubingwa na ushindi wa kila namna kwenye medani hizo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, faida nyingine kubwa inayopatikana kwenye kushiriki wanamichezo wa kike wa Iran kwenye medani mbali mbali za mashindano ya michezo, ni kuihami, kuilinda na kutangaza ukweli kuhusu Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, moja ya vita vya daima na vya kila siku vya kisaikolojia vya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kueneza madai ya uongo kwamba watu wenye vipaji katika nyuga tofauti hawakubaliani na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, lakini kwa hatua yenu hii ya kushiriki kwenye medani mbali mbali za michezo mnathibitisha uaminifu wenu kwa Jamhuri ya Kiislamu kwa kutumia jukwaa moja la kimataifa.
Amesema, asili ya hatua ya vijana wanamichezo wa Iran ya Kiislamu, kushiriki kwenye mashindano ya michezo mbali mbali katika medani za kimataifa ni jambo lenye umuhimu na thamani kubwa na kuongeza kuwa: Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuwa na vijana kama wewe.
 
< Nyuma   Mbele >

^