Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Majibu ya Kiongozi Muadhamu kwa Barua ya Rais wa Iran kuhusu Mchakato wa Mazungumzo ya Nyuklia Chapa
24/11/2013
 Majibu ya Kiongozi Muadhamu kwa Barua ya Rais wa Iran kuhusu Mchakato wa Mazungumzo ya NyukliaMajibu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Barua ya Rais wa Iran kuhusu Mchakato wa Mazungumzo ya Nyuklia
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Hujjatul Islam Walmuslimin Dk Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na mchakato wa mazungumzo ya nyuklia na sambamba na kuipongeza na kuishukuru timu ya Iran inayoshiriki kwenye mazungumzo hayo amesisitiza kuwa: Ni jambo lisilo na shaka kwamba taufiki ya Mwenyezi Mungu, dua na uungaji mkono wa wananchi wa Iran ndiyo mambo yaliyopelekea kupatikana mafanikio hayo na kwamba kusimama kidete mbele ya madola yanayopenda makuu inabidi kiwe ndicho kielelezo cha njia iliyonyoka kwa viongozi wanaohusika kwenye suala hilo.
Matini kamili ya barua ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majibu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Janabi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Ayatullah Udhma Khamenei (damat barakaatuh)
Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Ambaye amewajaalia wana wa Mapinduzi ya Kiislamu katika miezi ya awali kabisa ya kuanza kazi za serikali ya tadibiri na matumaini (serikali ya 11 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) kuthibitisha katika uga wa kimataifa, haki ya taifa la Iran ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia, kupitia mazungumzo, na hivyo kupiga hatua ya kwanza kwa namna ambayo imeyafanya madola makubwa ya dunia - ambayo kwa miaka mingi yalikuwa yanaikana haki hiyo - yatambue haki ya taifa la Iran ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia na kurutubisha urani na kuandaa mazingira ya kupigwa hatua kubwa zaidi katika siku za usoni za kulinda maendeleo ya kiteknolojia na kiuchumi ya taifa la Iran.
Taufiki iliyopatikana katika mazungumzo hayo inaonesha kuwa, inawezekana kuchunga misingi na mistari myekundu ya Jamhuri ya Kiislamu na wakati huo huio kuonyesha misimamo ya taifa la Iran kwa hoja za kimantiki na kuzitimizia hoja fikra za walio wengi duniani na kuyafanya madola makubwa duniani yaheshimu haki ya taifa la Iran na kupiga hatua madhubuti zaidi katika jitihada za baadaye za kuzipatia ufumbuzi wa kudumu hitilafu zilizopo.
Ni jambo lisilo na shaka kwamba, mafanikio haya yamepatikana kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na miongozo ya busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na uungaji mkono wa kila upande wa wananchi wa Iran na Inshaallah mafanikio ya mwisho katika njia hii nayo yataweza kupatikana kwa kuendelea kuwepo miongozo yako ya busara na hekima na msaada na uungaji mkono wa wananchi watukufu na wenye subira wa Iran.
Mafanikio muhimu na ya msingi yaliyopatikana kwenye makubaliano haya ya awali ni kutambuliwa rasmi haki ya Iran ya kustafidi na nishati ya nyuklia sambamba na kulindwa mafanikio ya nyuklia ya wana wa ardhi na nchi hii, ambapo pembeni mwa hayo, kusimamishwa mwenendo wa kuiwekea vikwazo vya dhulma taifa la Iran kutapelekea kuondolewa baadhi ya mashinikizo yasiyo ya kisheria na vikwazo vya upande mmoja na kama ambavyo pia itaanza kuporomoka ile taasisi ya vikwazo. Hatimaye ubunifu huu wa Iran ya Kiislamu na kusimama kidete taifa kubwa la Iran kumeyafanya madola makubwa yalazimike kukukubaliana na ukweli kwamba vikwazo na mashinikizo hayawezi kusaidia chochote na kama ambavyo Iran ilisema tangu awali, hakuwezi kupatikana makubaliano yoyote bila kuheshimiana na kufanyika mazungumzo ya kweli ambayo kila upande utakuwa unamstahi mwenzake. Kwa bahati mbaya upande wa pili unaofanya mazungumzo na Iran umeona umuhimu wa jambo hilo kwa kuchelewa. Ni jambo lisilo na shaka kuwa, kufikiwa mwafaka huu usio na mshindi wala mshindwa ni kwa manufaa ya nchi zote za eneo la Mashariki ya Kati kama ambavyo pia ni kwa manufaa ya usalama na maendeleo ya dunia nzima.
Kwa kupatikana taufiki hii ya Mwenyezi Mungu, ninatumia fursa hii kutoa pongezi zangu kwako Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na miongozo na uungaji mkono wako kama ambavyo ninawashukuru pia wananchi wa taifa kubwa la Iran kwa uungaji mkono wao mkubwa na wa kila upande, nikiwakumbuka kwa wema mashahidi wetu wa nyuklia. Vile vile ninaitumia fursa hii kutangaza kwa mara nyingine tena ahadi iliyojaa ikhlasi ya serikali katika kulihudumia taifa hili linalothamini mambo linayotendewa nikiomba dua zako kwa heshima na taadhima na dua za matabaka yote ya wananchi.

Hassan Rouhani
3 Azar 92.

Majibu ya Kiongozi Muadhamu kwa barua hiyo ya Rais Hassan Rouhani ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Janabi Rais wa Jamhuri ya Kiislamu
Timu inayoshiriki katika mazungumzo ya nyuklia na maafisa wote wanaohusika katika kadhia hiyo wanastahiki kushukuriwa na kupongezwa kutokana na hiki kilichopatikana ambacho kinaweza kuwa msingi wa hatua nyingine za busara na za hekima katika siku za usoni. Ni jambo lisilo na shaka kwamba taufiki ya Mwenyezi Mungu na dua na uungaji mkono wa taifa la Iran ndiyo mambo yaliyopelekea kupatikana mafanikio haya ambayo yatapatikana pia katika siku za usoni Inshaallah. Inabidi suala la kusimama imara mbele ya (madola na watu) wanaopenda makuu liwe ndicho kielelezo cha daima katika njia iliyonyooka ya harakati ya viongozi husika katika suala hilo na Inshaallah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Sayyid Ali Khamenei,
3 Azar, 1392
(Novemba 24, 2013).

 
< Nyuma   Mbele >

^