Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Amirijeshi Mkuu wa VikosiVyote vya Ulinzi vya Iran Aonana na Makamanda wa Jeshi la Majini Chapa
24/11/2013
Jagora Imam Khamenei Ya Gana Da Manyan Kwamandojin Sojojin Ruwa Na IranAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) ameonana na makamanda na maafisa wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu na huku akiashiria nafasi muhimu sana ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, ya taifa na ya jeshi la Iran amesema kuwa, kuwepo nguvu na maendeleo ya kweli kunaashiria kuwepo watu weledi wa mambo, wenye imani thabiti na wenye ushujaa unaotakiwa na kuongeza kwamba, lengo kuu la Jeshi la Majini linapaswa liwe ni kuunda jeshi lenye hadhi ya taifa la Iran na lenye hadhi ya malengo matukufu ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Katika mkutano huo uliofanyika wakati huu wa kukaribia tarehe 7 Azar (Novemba 28) ambayo ni Siku ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameitaja tarehe 7 Azar kuwa ni siku ya kuwaenzi wanajeshi mashujaa wa Jeshi la Majini na kuongeza kuwa, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kumepatikana maendeleo makubwa katika Jeshi la Majini lakini inabidi izingatiwe kuwa, maendeleo ya zana na vifaa vya kisasa tu vya kijeshi, si dalili ya kuwa na nguvu.
Amesema, jambo lililopelekea madola makubwa yatambue utambulisho, shakhsia, uadhama na utukufu wa jeshi la Iran ni kuweko watu wenye maarifa, wenye imani thabiti na wenye ushujaa unaotakiwa na kuongeza kuwa, kwa bahati nzuri hivi sasa muundo wa nguvu kazi ya Jeshi la Majini ni mzuri huku mkabala wa hali hiyo kukionekana kitu ambacho watu waliopita ambao hawakuwa na sifa zinazotakiwa, kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, walikuwa wamekipanga kitokee.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia vipengee tofauti vya umuhimu wa kielimu, kijeshi, kimataifa na kisiasa wa Jeshi la Majini na kuongeza kuwa, Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina umuhimu mkubwa katika upande wa kielimu na zana za kijeshi kama ambavyo pia lina nafasi ya kipekee ya kisiasa na kijeshi kwa kuzingatia siasa zinazotawala hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuwepo baadhi ya vitisho katika eneo hili.
Vile vile ameashiria kuwepo Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu katika fukwe za Bahari ya Oman na taathira zake nzuri katika ustawi wa taifa na kuongeza kuwa, iwapo serikali italizingatia jambo hilo, basi Jeshi la Majini linaweza kuandaa mazingira mazuri ya kuwepo maendeleo makubwa na ustawi wa kimapinduzi katika eneo hili.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Admirali Habibullah Sayyari, Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sambamba na kutoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Basiji na maadhimisho ya tarehe 7 Azar (28 Novemba, Siku ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) amesema kuwa, inabidi juhudi zaidi zifanyike za kuliimarisha zaidi na zaidi Jeshi la Majini kwa ajili ya kuitia nguvu na kuiongezea kasi harakati inayozidi kunawiri wa maendeleo ya nchi na kupata nguvu, hadhi na utukufu baharini na inabidi Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran liwe kigezo na litoe ilhamu na matumaini kwa mataifa mengine.
 
< Nyuma   Mbele >

^