Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Waziri Mkuu wa Iraq Aonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Chapa
05/12/2013
Waziri Mkuu wa Iraq Aonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ameonana na Bw. Nouri al Maliki, Waziri Mkuu wa Iraq na huku akiashiria umuhimu wa kustawishwa na kutiwa nguvu uhusiano wa kisiasa na wa kiuchumi baina ya Iran na Iraq amesema kuwa, medani ya ushirikiano wa kudumu katika sekta na kada tofauti baina ya nchi hizi mbili ni mpana mno na hakuna kizuizi chochote katika suala la kukuza uhusiano na Iraq pamoja na ustawishaji wa ushirikiano wa kieneo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameunga mkono matamshi ya Waziri Mkuu wa Iraq kwamba mazungumzo yaliyofanyika baina ya serikali za Iran na Iraq kuhusu udharura wa kustawisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kielimu baina ya pande mbili na ameongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Iran imestawi sana kielimu na kwamba suala la kupatiwa Iraq uzoefu na tajiriba ya kielimu ya Iran linaweza kuwa moja ya nyuga muhimu za kustawisha ushirikiano wa pande mbili.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amesifu kazi na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya Iraq na kumkhutubu Waziri Mkuu wa Iraq akimwambia: Jitihada ambazo leo hii mnazifanya kwa ajili ya nchi yenu ni harakati yenye thamani sana, tab'an Iraq ina mahitaji mengi yanayotaka idili na juhudi kubwa zaidi.
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema kuwa, Rais Jalal Talabani wa Iraq ni rafiki mzuri na wa karibu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na amemuomba Mwenyezi Mungu ampe afya ya haraka.
Kwa upande wake, Bw. Nouri al Maliki, Waziri Mkuu wa Iraq ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Kiislamu na kuelezea matumaini yake kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo mbali mbali aliyoyafanya na viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu katika ziara yake nchini Iran yatapelekea kustawishwa zaidi na zaidi ushirikiano wa nchi mbili.
 
< Nyuma   Mbele >

^