Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kumbukumbu za Maombolezo ya Arubaini ya Imam Husain AS Zilizohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu Chapa
23/12/2013
Kumbukumbu za Maombolezo ya Arubaini ya Imam Husain AS Zilizohudhuriwa na Kiongozi MuadhamuWawakilishi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka kona zote za Iran leo wameshiriki katika kumbukumbu za maombolezo ya arubaini ya Bwana wa Mashahidi, Imam Husain AS na wafuasi wake watiifu, kumbukumbu ambazo zimefanyika katika Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) mjini Tehran na kuhudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Kumbukumbu hizo zimejaa hisia za hamasa na mapenzi makubwa kwa Imam Husain AS.
Katika kumbukumbu hizo, Hujjatul Islam Walmuslimin Qasimiyan, amebainisha vipengee mbali mbali vilivyojaa nuru ya mwamko na mapambano yaliyojenga historia - ya Imam Husain AS - katika jangwa la Karbala liliko katika Iraq ya leo na namna msafara wa mtukufu huyo wa kuelekea Karbala ulivyoweza kuwaamsha watu na kutoa somo lililobakia milele hadi leo hii.
Aidha katika kumbukumbu hizo za kimaanawi, Bw. Moti'i - msomaji wa mashairi na kasida za Ahlul Bayt AS - amesoma mashairi yaliyoelezea masaibu ya Bwana wa Mashahidi Imam Husain AS na msafara wake pamoja na namna watu wa Nyumba ya Bwana Mtume Muhammad SAW alivyofanywa mateka baada ya mapambano ya Karbala. Mashairi hayo yameambatana na maombolezo yaliyofanywa kwa huzuni na hamasa kubwa na hadhirina katika kumbukumbu hizo.
Mwishoni mwa kumbukumbu hizo, wanafunzi hao wa Vyuo Vikuu kutoka kona zote za Iran wamesali sala za Adhuhuri na Laasiri zilizosalishwa na Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mwishoni mwa kumbukumbu hizo pia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa hotuba fupi mbele ya mjumuiko huo mkubwa na uliojaa hamasa wa wanachuo waombolezaji katika Arubaini ya Imam Husain AS, akiwashukuru wanachuo hao kwa kuhudhuria kwenye kumbukumbu hizo.
Amesema kuwa kumbukumbu hizo zilikuwa moja ya kumbukumbu za aina yake kabisa kutokana na kuhudhuria ndani yake watu wenye vipaji vya kila namna wakiwa wamejaa mapenzi, hamasa na ikhlasi.
Vile vile amewaombea dua vijana wote nchini na kusema kuwa, Iran ni nchi ambayo mustakbali wake ni mali ya vijana na kwamba vijana nchini wanapaswa kubeba jukumu hilo zito kwa ufakhari mkubwa na kulifikisha salama kulikokusudiwa jukumu hilo.
 
< Nyuma   Mbele >

^