Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Kamati ya Kuendesha Kumbukumbu za Mashahidi wa Mazandaran Chapa
16/12/2013
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Kamati ya Kuendesha Kumbukumbu za Mashahidi wa MazandaranKiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana na wasimamiaji na waendeshaji wa kumbukumbu za mashahidi elfu kumi wa mkoa wa Mazandaran na kusema kuwa, mashahidi na wapiganaji jihadi ni watu wanaobakisha kumbukumbu za milele na kufafanua kuwa: Kuadhimisha na kubakisha hai kumbukumbu na sira za mashahidi hao kupitia kufanya kazi za utafiti na kuzalisha athari za kimaandishi na kwa kutumia vyombo mbali mbali vya haabari na vya kuwasiliana na watu wengi katika kuzungumzia sira na maisha ya mashahidi hao ni jambo la dharura sana kama ambavyo ni lazima pia kazi zinazofanyika katika uwanja huo zifanyike kwa kina, kwa umakini wa hali ya juu na kwa kutumia sanaa na utafiti ili athari za kazi hizo ziweze kubakia milele.
Aidha Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, harakati adhimu ya vijana katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane ambavyo Iran ililazimika kupigana baada ya kuvamiwa na utawala wa zamani wa Iraq) ulikuwa ni muujiza wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Vita vya kujihami kutakatifu mbali na kwamba vilikuwa ni mthimani mkubwa kwa taifa la Iran, vilikuwa ni fursa pia ya kujitokeza vipaji vikubwa vya watu wa maeneo tofauti ya Iran na uwanja huo mpana ulipelekea kujitokeza vipaji vingi vilivyokuwa vimejificha, kwa kadiri ilivyowezekana.
Ayatullah Udhma Khamenei amekumbushia pia miongozo iliyokuwa inatolewa na makamanda mashahidi wakiwemo Bakeri, Kharazi, Baqeri na kuchanua kimuujiza na kwa sura ya ajabu vipaji vyao katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu na kusisitiza kuwa, uwanja wa vita vya kujihami kutakatifu uliandaa mazingira ya kuweza vijana hao kuwa makamanda wenye stratijia bora kabisa za kijeshi na kuweza kulizingira kwa kila upande na kulishinda jeshi lililokuwa limejiandaa kwa kila aina ya silaha za kisasa na kuungwa mkono kwa kila namna na madola makubwa ya kibeberu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia namna mkoa wa Mazandaran ulivyo na historia kongwe ya kushikamana na dini, kujitolea, uaminifu, iklhasi na kiujumla historia yake yote inayong'ara na kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kutokana na michango yao mikubwa katika nyuga tofauti za Mapinduzi ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na mchango wao mkubwa katika kipindi cha kujihami kutakatifu na kipindi cha ujenzi wa nchi.
 
< Nyuma   Mbele >

^