Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Waziri Mkuu wa Uturuki Chapa
29/01/2014
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Waziri Mkuu wa UturukiKiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, leo jioni (Jumatano) ameonana na Waziri Mkuu wa Uturuki na kusisitiza kuwa, uhusiano wa kiudugu, kimapenzi na kiurafiki ulioimarika zaidi katika karne za hivi karibuni baina ya Iran na Uturuki ni uhusiano wa aina yake kabisa na kuongeza kuwa: Nchi hizi mbili zina maeneo mengi sana ya kuweza kuimarisha ushirikiano baina yao na kwamba jambo hilo limezidi kuandaa uwanja mzuri wa kuweza kutia nguvu na kupanua ushirikiano wa pande hizo mbili kwa kiwango kikubwa sana.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, ni jambo la dharura sana kwa Tehran na Ankara kulipa uzito wa hali ya juu suala la utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika safari ya Bwana Ordogan mjini Tehran na kusisitiza kuwa: Kupewa uzito wa aina hiyo jambo hilo kutapelekea kuimarika zaidi uhusiano na kuongezeka kasi ya ushirikiano baina ya pande mbili.
Vile vile amekumbushia mielekeo na mfungamano wa ndani ya nyoyo uliopo baina ya mataifa mawili ya Iran na Uturuki na kuongeza kuwa: Inabidi fursa na nafasi muhimu zinazotokea mara kwa mara zitumike vizuri na kwa njia sahihi.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Uturuki, Bw. Recep Tayyip Erdogan sambamba na kuwasilisha salamu nyingi za Rais na wananchi wa Uturuki amesema kuwa, anaihesabu Iran kuwa ni nyumbani kwake kwa pili.
Aidha Waziri Mkuu wa Uturuki amesema kuwa, mazungumzo yake ya leo na Rais Hassan Rouhani na viongozi wengine wa Iran yalikuwa mazuri na yenye faida nyingi na huku akiashiria kutiwa saini hati kadhaa za maelewano baina ya nchi mbili amesema: Ni matumaini yangu kuwa uhusiano wa nchi hizi mbili utazidi kustawi na kuimarika na kuwa kigezo kizuri kwa ajili ya eneo hili na dunia nzima kiujumla.
Vile vile Bw. Ordogan amelitaja suala la kutiwa saini hati ya Baraza Kuu la Ushirikiano wa Iran na Uturuki kuwa ni hatua muhimu sana na kuongeza kwa kusema kuwa: Tutatumia vikao vya mara kwa mara vya pande mbili kuimarisha uhusiano wetu na kuufikisha katika kiwango ambacho itaonekana kana kwamba mawaziri wa nchi hizo mbili wanafanya kazi na kujadiliana mambo yao katika baraza moja la pamoja la mawaziri.
 
< Nyuma   Mbele >

^