Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Amirijeshi Mkuu wa Majeshi Yote ya Iran Aonana na Makamanda na Maafisa wa Jeshi la Anga Chapa
08/02/2014
Supreme Leader Meets with Turkish Prime MinisterAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na majimui ya makamanda na maafisa wa jeshi la anga la Jamhuri ya Kiislamu na kulitaja suala la uhuru, kujitegemea na kupambana na madola ya kibeberu na ya kiistikbari yanayopenda kuingilia masuala ya nchi nyingine kuwa ni moja ya misingi mikuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Matamshi yanayotolewa kijeuri na viongozi wa Marekani ni funzo na ibra kwa watu wote na kwamba wananchi wa Iran wanapaswa kufuatilia kwa kina na kwa weledi wa hali ya juu mazungumzo ya hivi karibuni na matamshi yanayotolewa na Wamarekani.
Vile vile ameashiria kuwa, moja ya mambo ya lazima katika kulinda na kuhifadhi uhuru ni kuwa na misimamo ya wazi iliyo wadhiha bila ya kujifichaficha kuhusiana na misingi na matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu na mistari ya asili ya Imam mtukufu ikiwemo pia kadhia ya Marekani.
Aidha amesisitiza kuwa: Siri ya kudumu, kuwa imara na kuwa na nguvu za ndani mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutokana na mfumo huo kutegemea imani, mapenzi na irada zisizotetereka za wananchi na kwamba taifa la Iran katika maandamano ya Bahman 22 (siku yanapofikia kileleni maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran) ya mwaka huu litatoa kaulimbiu na nara za Mapinduzi ya Kiislamu kwa ukakamavu na uimara zaidi na kwa mara nyingine litawaonesha walimwengu nguvu zake za kitaifa na kusimama kwake imara.
Katika mkutano huo uliotishwa kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kihistoria ambayo makamanda na maafisa wa jeshi la anga la Iran walikwenda kutoa mkono wa baia na kutangaza utiifu wao kwa Imam Khomeini (quddisa sirruh) tarehe kumi na tisa Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsia (Februari 8, 1979), Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja tukio hilo kuwa ni lenye upeo mkubwa wa kila namna na ni hatua iliyojaa baraka.
Ameongeza kuwa, moja ya vipengee muhimu mno vya tukio hilo la tarehe 19 Bahman ni kuhuisha hisia za uhuru za jeshi la anga na baadaye jeshi zima la Iran kwani jambo hilo liliandaa uwanja wa kujitokeza moyo wa kujiamini na kutegemea uwezo mbali mbali wa ndani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amebainisha maana ya neno uhuru kwa kuashiria mbinu mpya zinazotumiwa na ukoloni mamboleo za kuwatumia vibaraka wao badala ya kuingia wao moja kwa moja katika nchi za mataifa mengine duniani na kuongeza kuwa: Katika kupambana na ukoloni mamboleo mbali na kupambana na ukandamizaji na udiktetea uliopo, inabidi kupambana pia na mabeberu wa kigeni na waungaji mkono wa madikteta kwani kupambana na ukandamizaji na wakati huo huo kufanya mapatano na mabeberu hakuwezi kuzaa matunda mazuri.
Ayatullah Udhma Khamenei ameendelea kuzungumzia suala hilo kwa kuashiria hatima ya baadhi ya mapinduzi ya wananchi yaliyotokea katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika na kusema kuwa, mapinduzi yanayoweza kufanikiwa ni yale ambayo yanazitambua nguvu za muistikbari na beberu zilizoko nyuma ya dikteta na badala ya kufanya mapatano na muistikbari huyo, mapinduzi hayo yasimame imara kupambana na nguvu hizo za dola la kibeberu.
Ameongeza kuwa: Ni kwa sababu hiyo ndio maana baada tu ya kutekwa ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Tehran na vijana wanamapinduzi, Imam Khomeini (quddisa sirruh) alilitaja jambo hilo kuwa ni mapinduzi makubwa zaidi kuliko hata mapinduzi ya kwanza (yaliyoung'oa utawala wa kidikteta wa mfalme Shah) kwani harakati hiyo ya vijana wanamapinduzi wa Iran ilionesha kuwa taifa la Iran baada ya kuupindua utawala wa taghuti lilikuwa linautambua pia utando na tabaka linalofuatia la muistikbari na hatari zake na ndio maana liliamua kupambana nalo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, welewa na utambuzi huo pamoja na kuchukua hatua ya kupambana na dola la kibeberu linaloingilia masuala ya ndani ya taifa, ndiyo maana halisi ya uhuru.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Madola ya kigeni yanayopenda kuingilia masuala ya mataifa mengine yanaogopeshwa sana na hisia zozote zile za uhuru wanazokuwa nazo wananchi wa nchi yoyote ile na ndio maana yanajaribu kutumia mbinu za kila namna kuzuia watu wa mataifa hayo wasipane hisia za uhuru na kujikomboa na wakati wote yanahakikisha nchi hizo zinatawaliwa na watu dhaifu.
Ametaja moja ya mbinu na hila zinazotumiwa na mabeberu katika suala hilo kuwa ni kupandikiza fikra ya kwamba uhuru na kujikomboa ni mambo ambayo yanakinzana na maendeleo.
Ameongeza kuwa, vyombo vya kipropaganda vya madola ya kibeberu na vibaraka wao wa ndani mara zote wanajitahidi kuonesha kuwa kutegemea na kuzingatia manufaa na utambulisho wa kitaifa hakuendani na maendeleo kwa maana ya kwamba kama nchi inataka ipate maendeleo basi haina budi kusahau suala la kuwa huru na kujikomboa.
Kiongozi Muadhamu wa Maopinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Maneno hayo ni ghalati na ni makosa kikamilifu, bali ni uongo unaotungwa na watu ambao wanapinga uhuru wa nchi nyingine duniani.
Ayatullah Udhmna Khamenei aidha amesisitiza kwamba, uhuru na kujikomboa hakuna maana ya kuwa na tabia mbaya na kujitenga na mataifa mengine ya dunia bali uhuru maana yake ni ngao na ni kinga ya kukabiliana na ushawishi wa nchi nyingine ambazo zinataka kupora na kukanyaga manufaa ya mataifa mengine kwa faida yao.
Amelitaja suala la kutegemea misingi na matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu kwa uwazi na kwa njia iliyo bayani kuwa ni jambo la lazima katika kulinda na kuhifadhi uhuru wa taifa na huku akiashiria sira ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) katika kubainisha misimamo yake kwa uwazi kabisa bila ya kujificha ficha ameongeza kwamba: Imam (quddisa sirruh) alibainisha msimamo wake kwa uwazi kabisa bila ya kuficha kitu kuhusu utawala wa taghuti wa kurithishana, wa kiimla, wa kiukandamizaji na wa kifalme uliokuwa ukitawala nchini Iran; Imam (quddisa sirruh) alitangaza wazi wazi msimamo wake kuhusiana na ulazima wa kuundwa mfumo wa utawala uliosimama juu ya msingi wa Uislamu na matukufu ya Kiislamu; Imam (quddisa sirruh) alitangaza wazi wazi na bila ya kificho msimamo wake kuhusu wajibu wa kupambana na kanali hatari sana ya Kizayuni inayotawala dunia na pia kusimama thabiti na kupambana vilivyo na utawala pandikizi na ghasibu wa Kizayuni. Alitoa misimamo yake hiyo kwa uwazi kabisa bila ya kumuogopa mtu yeyote.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Imam wetu mtukufu (quddisa sirruh) alipinga wazi wazi na bila ya kificho mfumo wa kibeberu yaani mfumo wa kimataifa ambao unaamini kwamba nchi za dunia lazima zigawanywe sehemu mbili, sehemu moja ni ile ya nchi zilizo nyingi zinazopaswa kufanyiwa ubeberu na sehemu ya pili ni ya nchi chache zinazozifanyia ubeberu na uistikbari nchi nyingine na alichukua msimamo wa wazi ulio wadhiha na usiojificha dhidi ya dola linaloongoza mfumo huo wa kidhulma yaani Marekani.
Vile vile Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Masuala hayo ndiyo misingi na usuli za Mapinduzi ya Kiislamu na kwamba baada ya kupita miaka 35 ya ushindi wa mapinduzi hayo matukufu misingi hiyo bado ipo na malengo yale yale bado yapo hayajabadilika na kwamba mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeweza kwa kushikilia misingi hiyo na kubakia imara katika njia hiyo; kupiga hatua za kustaajabisha za maendeleo katika nyanja na nyuga tofauti na kuwa moja ya madola makubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na moja ya madola yenye taathira katika masuala ya kimataifa.
Ameongeza kuwa: Kusimama imara wazi wazi na bila ya kutetereka taifa la Iran juu ya usuli na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu kumeyafanya hivi sasa mataifa mengine ya dunia na hata watu wenye vipawa na watu muhimu wasio na chuki wa mataifa mengine, kulihesabu taifa la Iran kuwa ni taifa shujaa, aminifu, erevu na lisilotetereka licha ya kuweko propaganda kubwa za vyombo vya kipropaganda vya maadui za kueneza chuki dhidi ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Leo hii si tu kwamba mapenzi na heshima ya taifa la Iran duniani haijapungua bali imeongezeka sana lakini katika upande wa pili hasira na chuki za mataifa ya dunia zinazidi kuongezeka dhidi ya Marekani.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa, siri ya kubaki mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye reli ya Mapinduzi ya Kiislamu na njia za asili za Imam, ni hatua yake ya kuwa muwazi katika kutangaza misingi na misimamo yake na kuongeza kwamba: Si sahihi hata kidogo kuacha kutangaza misimamo wazi wazi na bila ya kuficha kitu mbele ya marafiki na maadui wa taifa la Iran na kwamba misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni lazima ibainishwe kwa uwazi na bila ya kificho.
Amesisitiza pia kuwa, inawezekana kubadilisha mbinu na njia za kutumia lakini usuli na misingi mikuu lazima iwe imara wakati wote na kwamba suala hilo ndiyo siri ya kuwa imara na kupiga hatua za maendeleo nchi ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuwa na utambuzi wa kina kuhusu marafiki na maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni jambo muhimu na kuongeza kwamba: Maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu ni madola machache fasidi na yasiyo na hadhi wala heshima duniani lakini marafiki wa Mapinduzi ya Kiislamu ni mataifa mengine yote ambayo yanaelewa vyema kaulimbiu za Mapinduzi ya Kiislamu na mwito wa kila siku wa taifa la Iran wa kuwataka wanaodhulumiwa wasimame imara kupambana na dhulma.
Ayatullah Udhma Khamenei pia amesema, siri ya kuwa imara na kuwa na nguvu mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni uungaji mkono wa wananchi kwa mfumo huo na kushikamana vilivyo wananchi hao na mfumo wao huo wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa: Viongozi wa Marekani katika mazungumzo yao na viongozi wa Iran wanasema kuwa: Sisi hatuna nia ya kubadilisha mfumo wa utawala nchini Iran wakati ambapo uongo unaonekana wazi katika madai yao hayo kwani kama viongozi hao wangeliweza kubadilisha mfumo wa utawala nchini Iran wasingelisita kufanya hivyo hata kwa sekunde moja.
Ameongeza kwamba: Ushahidi mwingine unaoonesha kuwa viongozi wa Marekani hawawezi kubadilisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unaotawala nchini Iran ni kutokana na mfumo huo kutegemea imani, mapenzi na irada ya wananchi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kushiriki vilivyo wananchi katika nyuga mbali mbali na kuendelea wananchi hao kuyaunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu na kuziunga mkono kaulimbiu na matukufu ya mapinduzi hayo licha kupita makumi ya miaka tangu mapinduzi hayo yalipopata ushindi kuwa ni uungaji mkono wa kipekee na usio na mfano duniani na kusisitiza kwamba: Katika siku ya tarehe 22 Bahman (Februari 11) watu wote duniani wataona namna wananchi wa Iran kwa mara nyingine watakavyojitokeza kwa wingi mno katika miji yote ya Iran katika maandamano ya kuadhimisha siku hiyo na kuonesha uimara na nguvu zao za kitaifa kwa walimwengu wote.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile ameitaja siri ya "mafanikio na maendeleo ya taifa la Iran" kwamba ni kusimama imara na siri ya "kuwa na usalama taifa" kwamba ni kuonesha nguvu za kitaifa na kusisitiza kuwa: Moja ya madhihirisho ya nguvu za kitaifa ni mkusanyiko mkubwa wa wananchi kama ule unaoshuhudiwa kwenye maandamano ya Bahman 22 na vile vile ushiriki wa wananchi katika chaguzi mbali mbali. Amesema kwa kusisitiza kwamba, wakati watu wanapoamua kumuonesha adui nguvu zao za kitaifa, wakati huo tena adui huwa hawezi kulifanya lolote taifa hilo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile ameashiria misimamo ya hivi karibuni ya viongozi wa Marekani na kusema kuwa: Matamshi ya viongozi hao ni somo la ibra kwa wananchi wetu. Wananchi wa Iran wanapaswa kuangalia kwa kina na kwa karibu mazungumzo ya hivi karibuni na matamshi yasiyo na heshima yanayotolewa na Wamarekani ili waweze kuwajua vilivyo maadui wao wote.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria namna baadhi ya watu wanavyojaribu kubadilisha mtazamo wa wananchi wa Iran kuhusu uadui wa Marekani na kuongeza kuwa: Katika matamshi yake haya ya karibuni kabisa, adui ameonesha uadui wake na undumilakuwili wake kwa uwazi kabisa. Katika vikao vyao vya faranga na viongozi wa nchi yetu Wamarekani wanazungumza kwa namna tofauti na wanavyozungumza wanapotoka nje ya vikao hivyo. Yote haya yanaonesha namna viongozi hao wa Marekani walivyo na nyuso mbili na jinsi walivyo na nia mbaya na chafu ya kiuadui na kwamba wananchi wa Iran wanapaswa kuyafuatilia na kuyaangalia kwa kina na kwa kwa karibu sana masuala hayo.
Ameongeza kuwa: Suala hilo na matamshi yanayotolewa na viongozi wa Marekani yanaonesha usahihi wa nasaha ambazo nimekuwa nikizitoa siku zote kwa viongozi wetu nchini yaani ulazima wa kulinda na kuhifadhi nguvu zetu za ndani na kwa bahati nzuri viongozi wetu wanaoshughulikia masuala ya kiuchumi wameelewa kwamba hakuna njia nyingine ya kuweza kukabiliana na matatizo yanayojitokeza isipokuwa kuwa na muundo madhubuti na wa ndani ya nchi na tayari hatua za utangulizi zinazohitajika kwa ajili ya suala hilo zimeshaanza kuchukuliwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwa mara nyingine kwamba: Njia pekee ya kuweza kuondoa matatizo ya kiuchumi nchini ni kuangalia na kutegemea uwezo mkubwa na usio na idadi uliomo nchini na sio kuangalia nje na wala kuwa na tamaa ya kuondolewa vikwazo na mashinikizo na maadui kwani hakuna matumani ya adui kufanya hivyo.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria baadhi ya matamshi ya viongozi wa Marekani wanaodai kuwa ni marafiki na wanalipenda taifa la Iran na kuongeza kwamba: Viongozi hao wanasema uongo pia katika jambo hilo. Kwa upande mmoja wanasema kuwa wanalipenda taifa la Iran lakini kwa upande wa pili wanatoa vitisho dhidi ya taifa hilo na wanadhani kuwa Jamhuri ya Kiislamu itapunguza nguvu na uwezo wake wa kujihami na kujilinda na kwa hakika hiyo ni istihzai iliyo wazi kabisa.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesisitiza kwamba: Taifa la Iran na viongozi katika sekta mbali mbali hususan vikosi vya ulinzi kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, siku baada ya siku watazidi kuimarisha uwezo na nguvu zao za kulilinda taifa hili.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kutegemea nguvu za ndani kuwa ndilo litakaloiokoa nchi na ndilo litakaloandaa uwanja wa kutatuliwa masuala tofauti ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni nchini.
Ameongeza kuwa: Siasa za uchumi wa kimuqawama na kimapambano zitawasilishwa karibuni hivi, na wakati huo hatua na miundo inayotakiwa ya kuwezesha kupatikana uchumi wa kimuqawama zitachukuliwa.
Vile vile ametoa nasaha kadhaa kwa wananchi na viongozi nchini.
Nasaha za kwanza zilikuwa ni kusisitiza kuhusu wajibu wa kulindwa na kuimarishwa umoja na mshikamano katika matabaka yote ya wananchi, viongozi na watu wenye vipawa na kuzuia kutiwa doa mambo ya asili kupitia mambo ya pembeni yasiyo ya asili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Leo hii matini na asili ya harakati ya taifa la Iran ni kuimarisha nguvu za ndani na kusimama kidete mbele ya tufani tofauti zinazolikabili taifa ambapo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu taifa la Iran kama lilivyofanya miaka 35 iliyopita, hivi sasa pia litafanikiwa kushinda tufani zote hizo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Inabidi umoja na mshikamano baina ya wananchi na viongozi uendelee kulindwa kupitia kuongeza uaminifu wa viongozi wa sekta mbali mbali kubwa na ndogo na kwa upande wa wananchi nao inabidi uaminifu wao uongezwe mbele ya viongozi wa sekta hizo tofauti.
Nasaha nyingine za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimehusiana na watu wanaokosoa serikali na viongozi serikalini.
Ayatullah Udhma Khamenei amewataka watu wanaokosoa serikali wawe na insafu wakati wanapokosoa kitu na kuongeza kuwa: Ni miezi michache tu imepita tangu serikali mpya iingie madarakani hivyo inabidi wapewe fursa viongozi serikalini ya kuweza kufanya kazi kwa nguvu zote na wakati huo huo watu wanaokosoa serikali wawe na kifua kipana cha kuangalia na kuamiliana na kazi za serikali kiuadilifu na kwa insafu.
Vile vile amewataka viongozi serikalini nao kuwa na kifua kipana cha kukubali kukosolewa na kusema kuwa: Kila mmoja ana wajibu wa kuchunga heshima ya mwenzake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia kuweko baadhi ya vibaraka wa adui ndani ya nchi na kusisitiza kwamba: Haipasi kughafilika na kuwasahu vibaraka hao na hivyo kutoa mwanya wa kutumia vibaya nukta dhaifu na kuleta matatizo katika harakati kuu ya nchi.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa: Sote tunapaswa kusaidiana katika njia ya Imam (quddisa sirruh) na katika njia ya kuiletea nguvu zinazotakiwa nchi yetu na kwamba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu taifa hili ltafanikiwa kupeleka mbele mambo yote kwa njia iliyo bora kabisa.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa uhakikisho akisema: Taifa la Iran litawashinda maadui katika kadhia ya nyuklia na katika masuala mengineyo.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Brigedia Jenerali, Rubani, Hasan Shah Safi, kamanda wa jeshi la anga cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Imam Hasan Askari AS na maadhimisho ya tarehe kumi na tisa Bahman (Februari 8) siku ya kuadhimisha hatua ya kihistoria ya makamanda na maafisa wa jeshi la anga la Iran ya kutangaza baia na utiifu wao kwa Imam Khomeini (quddisa sirruh) kama ambavyo pia ametoa ripoti fupi kuhusiana na uwezo wa ndani na hatua za maendeleo zililozipigwa na jeshi la anga la Iran akisisitiza kuwa: Hakuna nukta yoyote isiyofikiwa na walinzi wa taifa la Iran kwa ajili ya kumsambaratisha adui na kuvunja haiba yake.
Kamanda wa jeshi la anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vile vile amebainisha namna madola ya Magharibi yalivyofeli katika siasa zao na sasa yanabakia kudai tu kuwa machaguo yote ya kukabiliana na taifa la Iran likiwemo chaguo la kijeshi yako mezani na kuongeza kwamba: Taifa la Iran lilipamba kiume na lilisimama imara katika vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu na hivyo kuidhalilisha kambi ya kiistikbari na kwamba tunawausia wanaopiga makelele ya majigambo yasiyo na mashiko wasome sehemu ya historia yetu hiyo ya pamoja na watambue kuwa kwa yakini majibu yetu tutakapochokozwa yatakuwa makali sana, yatakuwa ya kumfanya adui ajute na yatakuwa ya kuliletea fakhari kubwa taifa letu.
 
< Nyuma   Mbele >

^