Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu apanda mche wa mti katika kukaribia siku ya upandaji miti nchini Iran Chapa
05/03/2014
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu leo mchana (Jumatano) amepanda mche mmoja wa mti Katika wiki ya maliasili na wakati wa kukaribia siku ya kupanda miti nchini Iran.
Baada ya kupanda mche huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amezungumza machache akiwashukuru wale wote wanajishughulisha na kazi ya kueneza maeneo kijani nchini Iran na kuongeza kuwa: Wakuu na matabaka yote ya wananchi wa Iran wanataka suala la maeneo kijani lipewe umuhimu mkubwa ili nchi na maisha ya wananchi yaweze kufaidika na neema hiyo kubwa ya Mwenyezi Mungu.
Amesema, suala la kulinda mazingira ni muhimu sana na huku akiashiria matukio kama ya kuingia hewa ya vumbi na mchanga nchini Iran kutoka nchi jirani amesisitiza kuwa: Ili kuondoa madhara hayo, sekta zote za serikali zinapaswa kulipa umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na madhara hayo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa, kuzungumza na nchi husika na kushirikiana na pande mbali mbali kwa ajili ya kuzuia madhara hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile ametaka lipewe umuhimu mkubwa zaidi suala la kuzuia kuharibiwa mazingira na maeneo kijani akisema: Kaulimbiu ya "Kila Muirani, mti mmoja" ni nara na kaulimbiu nzuri sana na ni ya dharura kwa ajili ya kupambana na kugeuzwa vyanzo hivyo muhimu vya kimaumbile kuwa vyuma na saruji kama ambavyo pia jambo hilo ni la dharura kuwa nalo maafisa husika wote kama wenzo wa kupambana kisheria na watu wote wanaotumia vibaya jambo hilo.
Katika zoezi hilo, wamehudhuria pia Waziri wa Jihadi ya Kilimo, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala katika Wizara ya Jihadi ya Kilimo na meya wa jiji la Tehran.
 
< Nyuma   Mbele >

^