Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Nairuzi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Mwaka 1393 Hijria Shamsia Chapa
20/03/2014
Ujumbe wa Nairuzi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Mwaka 1393 Hijria ShamsiaAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kwa wananchi wa Iran kwa mnasaba wa kuingia mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia na kuuita mwaka huo kwa jina la mwaka wa "Uchumi na Utamaduni wenye Azma ya Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."

Matini kamili ya ujumbe wake huo ni kama ifuatayo:

بسم الله الرحمن الرحیم
یا مقلّب القلوب و الابصار، یا مدبّر اللّیل و النّهار، یا محوّل الحول و الاحوال، حوّل حالنا الی احسن الحال
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
Ewe Mgeuzaji wa nyoyo na basari! Ewe Mpangiliaji wa Usiku na Mchana!
Ewe Mbadilishaji wa mwaka na hali! Badilisha hali zetu kuwa bora ya hali.

Ewe Mola wangu mminie rehema Zako Fatima na baba yake, na mumewe na wanawe. Mola wangu, kuwa; kwa ajili ya walii Wako na hujja Wako, mwana wa Hasan (Imam Mahdi AS), rehema ziwe juu yake na wazazi wake, katika saa hii na katika kila saa; (kuwa) Walii wake, na Mlinzi wake, na Kiongozi wake na Mwenye kumnusuru na Mwonyesha njia na jicho lake hadi utakapomfikisha kwenye ardhi Yako akiwa mtiifu kikamilifu Kwako na umneemeshe na umstareheshe humo milele.
Ewe Mola wangu, harakisha faraja zake na utujaalie kuwa wasaidizi wake, na watu wanaomnusuru na utujaalie pia kuwa wafuasi wake wa kweli.
Ninatoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Nairuzi na kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya. Mkono wangu wa baraka uwaendee wananchi wenzangu wote azizi nchini, na Wairani wote walioko katika kila kona ya dunia. Mkono wangu wa baraka hasa hasa nautoa kwa familia azizi za mashahidi, majeruhi wa vita, aila zao, watu wote wanaojitolea katika njia ya haki, na watu wote wanaofanya kazi kwa bidii na idili kubwa katika nyuga tofauti. Kama ambavyo pia mkono wangu wa baraka za Nairuzi nautoa kwa kwa mataifa yote yanayoadhimisha sikukuu hii ya Nairuzi, ulimwenguni.
Mwaka mpya mwaka huu umeingia ukiwa umesadifiana na siku za maadhimisho ya kukumbuka alipokufa shahidi bibi bora zaidi duniani na katika ulimwengu wa Kiislamu, Siddiqatul Kubra (Bibi Fatimatuz Zahra - Salamullahi Alayha). Kusadifiana huku kunaliwajibisha taifa letu Inshaallah liweze kutumia vizuri baraka za nuru za Fatima, kujiidilisha kuingia chini ya miale ya nuru ya mafundisho ya mtukufu huyo na kujinawirisha kwa nuru za uongofu wa Mwenyezi Mungu ambazo wametunukiwa na kupewa hadiya wanadamu wote duniani kupitia kwa Fatimatuz Zahra (Salamullahi Alayha) na Ahlul Bayt wa Mtume (SAW).
Kupita miaka na kuingia miaka mingine kunapaswa kuwe sababu ya sisi sote ya kupata tajiriba na uzoefu wa busuri na muono wa mbali, tujifunze kutokana na yaliyopita na kuuangalia mustakbali wetu kwa jicho la wazi na kwa moyo wenye welewa mpana na hatimaye tuweze kuchukua maamuzi sahihi kuhusu mustakbali wetu. Ninamuomba Mwenyezi Mungu awape Wairani wote azizi afya njema katika mwaka huu mpya na awape nyoyo za furaha na awape watu wote wa nchi yetu wanaume kwaa wanawake, hima, irada na azma madhubuti na sahihi kwa ajili ya kuingia kwenye njia mbali mbali zilizojaa fakhari na awape furaha na afya njema watoto wetu na azipe usalama, mapenzi na mahaba familia zetu. Jukumu letu ni kuangalia tulikotoka kwa ajili ya kupata somo na ibra na tuangalie mbele kwa ajili ya kuwa na mipangilizo mizuri na maamuzi sahihi.
Mwaka uliopita ulitangazwa kuwa ni mwaka wa "Hamasa ya Kisiasa na Hamasa ya Kiuchumi." Alhamdulillah hamasa ya kisiasa imeshuhudiwa vizuri katika medani mbali mbali, hamasa hiyo imeshuhudiwa katika chaguzi na vile vile katika maandamano makubwa makubwa na pia katika mahudhurio ya wananchi kwenye nyuga tofauti na katika jitihada na harakati mbali mbali ambazo zilifanywa na viongozi pamoja na wananchi katika kipindi kizima cha mwaka ulioisha. Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa kubadilika serikali moja na kuja serikali nyingine, ulikuwa ni mwaka wa kukabidhiana madaraka na jambo hilo lilifanyika kwa utulivu kabisa na kwa usalama wa hali ya juu na Alhamdulillah imeweza kujitokeza kongwa nyingine katika silisila na mnyororo mrefu wa uongozi nchini.
Katika upande wa "Hamasa ya Kiuchumi" kazi ambayo ilipaswa ifanyike na matumaini ambayo yalitarajiwa kutimia hayakutimia. Kulifanyika jitihada mbali mbali ambazo zinastahiki kushukuriwa, lakini kazi kubwa ambayo ilitarajiwa kufanyika katika "Hamasa ya Kiuchumi" bado iko mbele yetu na tuna jukumu la kuhakikisha kuwa hamasa hiyo inatokea. Suala la kimsingi yaani la kiuchumi kwa nchi yetu na kwa taifa letu ni suala muhimu na mwisho mwa mwaka (uliomalizika hivi punde) wa 1392 (Hijria Shamsia), Alhamdulillah kumeshuhudiwa kujitokeza uwekaji msingi muhimu wa kifikra na kimitazamo kuhusu "Hamasa ya Kiuchumi," na siasa za "Uchumi wa Kusimama Kidete" zimetangazwa (mwishoni mwa mwaka huo) na hivi sasa mazingira yameshaandaliwa kwa ajili ya Inshaallah kufanyika jitihadi zinazotakiwa katika suala hilo.
Tukija katika mwaka huu wa 1393 (Hijria Shamsia) mtazamo wangu mimi hakiri wa Mwenyezi Mungu ni kuwa, kuna mambo mawili muhimu zaidi hivi sasa kuliko mambo mengine yote, suala la kwanza ni hili suala la uchumi na la pili ni suala la utamaduni. Katika nyuga zote hizo mbili na kwenye medani zote hizo mbili, kuna matumaini maalumu, na matumaini hayo ni ya pamoja, ni matumaini kwa viongozi wa nchi kama ambavyo matabaka mbali mbali ya wananchi nayo yanatarajiwa yashiriki vilivyo kwenye ufanikishaji wa mambo katika medani hizo. Kitu kinachotumainiwa na kutarajiwa kutimizwa katika kujenga maisha na mustakbali unaotakiwa, kamwe hakitawezekana bila ya kushiriki wananchi. Hivyo mbali na jukumu la kuongoza mambo ambalo viongozi nchini wanapaswa kulitekeleza, ushiriki wa wananchi katika nyuga zote hizo mbili nao ni jambo la lazima na la dharura, iwe ni katika uga wa uchumi au katika medani ya utamaduni. Bila ya kushiriki wananchi hakuna jambo lolote litakaloweza kutendeka na wala makusudio na malengo yaliyokusudiwa hayataweza kufikiwa bila ya kushiriki wananchi. Wananchi katika makundi mbali mbali ya wananchi wanaweza kutoa mchango mkubwa sana iwapo watakuwa na irada na azma ya kweli ya kitaifa. Viongozi nao kama wanataka kutekeleza kwa ufanisi kazi zao hawana njia nyingine ila kutegemea msaada wa wananchi. Hivyo viongozi nchini nao wanapaswa kuingia kijihadi katika medani ya amali kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwa msaada kutoka katika taufiki na auni ya Mwenyezi Mungu na muawana wa wananchi. Wanatakiwa waingie kijihadi namna hiyo katika uga wa kiuchumi na pia katika uwanja wa utamaduni. Mimi Inshaallah nitatoa ufafanuzi wa mambo yote hayo katika hotuba yangu ya siku ya Ijumaa nitakapozungumza na wananchi. Hivyo kwa mtazamo wangu, kitu ambacho tutakuwa nacho katika mwaka huu mpya ni uchumi ambao utachanua kwa kusaidiana viongozi na wananchi, na utamaduni ambao kwa hima ya viongozi na wananchi utaweza kuelekea kwenye ufanikishaji wa harakati kubwa ya nchi yetu na ya taifa letu. Hivyo nimeamua kutangaza kaulimbiu ya mwaka huu na jina la mwaka huu kuwa mwaka wa "Uchumi na Utamaduni wenye Azma na Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."
Ni matumaini yangu Mwenyezi Mungu Mtukufu atawasaidia wananchi wetu na viongozi wetu muhtaramu katika jitihada zao za kutekeleza majukumu yao katika uwanja huo na kuufanya moyo mtukufu wa Waliyul Asr (Imam wa Zama, Imam Mahdi AS) utufurahie na roho toharifu ya Imam wetu mtukufu na za mashahidi wetu azizi ziwe radhi nasi na zitufurahie.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 

 
< Nyuma   Mbele >

^