Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Awasilisha Sera Kuu za "Afya" Chapa
06/04/2014
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amewasilisha sera na siasa kuu za "afya" baada ya kushauriana na Halmashauri ya Kulinda Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran. Amefanya hivyo ikiwa ni katika kutekeleza mada ya kwanza ya kifungu cha 110 cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Matini ya siasa hizo kuu za afya ambazo zimewasilishwa na kukabidhiwa kwa wakuu wa Mihimili Mitatu Mikuu ya dola na mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:

Bisimillahir Rahmanir Rahim.

Sera Kuu za Afya

1 - Kutoa huduma za mafunzo, utafiti, afya, tiba na uwezo wa kiafya uliosimama juu ya msingi na matukufu ya kibinadamu - Kiislamu na kuwekewa misingi mizuri masuala hayo katika jamii.
1 - 1 - Kutia nguvu mfumo wa kuchagua, kuainisha thamani, kufundisha na kulea walimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu na viongozi na kuleta mabadiliko katika mazingira ya kielimu na ya Vyuo Vikuu ili yanasibiane na matukufu ya Kiislamu, maadili ya tiba na adabu za kitaalamu.
1 - 2 - Kuleta elimu kwa watu kuhusu haki na majukumu yao ya kijamiii na kustafidi vizuri na uwezo wa mazingira mbali mbali yanayotoa huduma za afya kwa ajili ya kukuza umaanawi na maadili ya Kiislamu katika jamii.
2 - Kufanikisha nadharia ya afya ya pande zote na mwanadamu aliye salama kiafya katika sheria zote, sera za utekelezaji na sheria mbali mbali kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
2 - 1 - Kuipa kipaumbele kinga mbele ya tiba.
2 - 2 - Kuifanya ya kisasa wakati wote mipango na ratiba za afya na matibabu.
2 - 3 - Kupunguza mambo ya hatari na uchafu unaotishia afya kwa kutegemea ushahidi wenye itibari ya kielimu.
2 - 4 - Kuandaa mfungamano wa afya kwa ajili ya mipango mikuu ya ustawi.
2 - 5 - Kutia nguvu vielelezo vya afya kwa ajili ya kuweza Iran kushika nafasi ya kwanza katika eneo la Asia ya kusini magharibi.
2 - 6 - Kufanyiwa marekebisho na kukamilishwa mifumo ya ufuatiliaji, usimamiaji na kutathmini mambo kwa ajili ya kulinda kisheria haki za wananchi na wagonjwa na kutekelezwa kwa njia sahihi sera na siasa kuu za afya.
3 - Kutia nguvu na kuboresha usalama wa kiafya wa nafsi na saikolojia katika jamii kupitia kuenezo mfumo wa maisha wa Kiislamu - Kiirani, kutia nguvu misingi ya familia, kuondoa vikwazo na vizuizi vinavyosababisha matatizo katika maisha ya mtu binafsi na ya jamii, kueneza mafundisho ya kimaadili na kimaanawi na kutia nguvu vielelezo vya usalama wa kisaikolojia.
4 - Kuanzisha na kutia nguvu miundombinu inayohitajika kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na malighafi za madawa, chanjo, mazalisho ya kibiolojia na masuala yake ya lazima pamoja na vifaa vya kitiba vyenye ubora na viwango vya kimataifa.
5 - Kuainisha mahitaji na kuzia kuingizwa mahitaji yasiyo sahihi na kuruhusu kuingizwa vitu kwa kutegemea tu mfumo wa miongozo na uainishaji wa kizahanati, mpango wa kijenasi na kurefusha maisha na mfumo wa kitaifa wa dawa nchini pamoja na kutunga sera na usimamiaji makini katika uzalishaji, utumiaji, uingizaji wa dawa, chanjo na mazalisho ya kibiolojia na vifaa vya kiafya kwa lengo la kuunga mkono na kusaidia uzalishaji wa ndani na kupanua wigo wa kusafirisha nje bidhaa.
6 - Kudhaminiwa usalama wa chakula na kupata kiuadilifu matabaka yote ya wananchi chakula salama, kinachotakiwa na cha kutosha, hewa safi, suhula za tiba za watu wote, bidhaa salama za kiafya sambamba na kuchungwa viwango vya kitaifa na vigezo vya kieneo na kimataifa.
7 - Kutenganishwa majukumu ya usimamiaji, kudhamini fedha na kutoa huduma katika masuala yote ya afya kwa lengo la kutoa majibu, kusimamisha uadilifu na kutoa huduma za tiba kwa wananchi kwa kiwango, ubora na namna inayotakiwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
7 - 1 - Kusimamia mfumo wa afya wenye utungaji sera za utendaji, mipango ya kiistratijia, kuanisha thamani na kusimamiwa na Wizara ya Afya, Matibabu na Elimu ya Tiba.
7 - 2 - Kusimamia vyanzo vya afya kupitia mfumo wa bima kwa kutegemea Wizara ya Afya, Matibabu na Elimu ya Tiba na kushirikiana vituo na asasi mbali mbali.
7 - 3 - Kuandaliwa huduma na watu wanaotoa huduma katika asasi za kiserikali, za umma na za binafsi.
7 - 4 - Kufanya uratibu na kupangilia mambo yaliyotangulia kutajwa hapo juu ili yaoane na utendaji kazi kwa namna ambayo itaainishwa na sheria.
8 - Kuongeza na kuzidisha ubora na usalama wa huduma na usimamiaji katika mambo yote na ya kila upande ya masuala ya usalama katika kalibu ya kulinda uadilifu na kupewa uzito wa hali ya juu uwajibikaji, kutolewa taarifa za uwazi zenye taathira nzuri, umakini na kustafidi vizuri na masuala ya afya katika fremu ya kanali ya afya na matibabu inayokubaliana na mfumo wa uainishaji viwango kupitia:
8 - 1 - Kueneza uchukuaji misimamo na hatua kulingana na matokeo ya utafiti wa kina na wa kielimu katika kusimamia masuala ya kiafya, elimu na huduma za matibabu kupitia kutunga viwango na miongozo, tathmini ya teknolojia za masuala ya afya, kuleta mfumo wa kuainisha viwango kwa kuzipa kipaumbele huduma za kuboresha masuala ya afya na kinga na kuyaingiza kwenye mfumo wa masomo na elimu za tiba nchini.
8 - 2 - Kuongeza ubora na usalama wa huduma za kusimamia na kuchunga masuala ya afya pamoja na kuleta na kueneza mfumo wa kutawala na kupewa umuhimu mkubwa zahanati pamoja na kuainisha viwango.
8 - 3 - Kutungwa mpango unaokusanya mambo yote kwa ajili ya kusimamia, kuwasaidia na kuwaunga mkono majeruhi wa vita na jamii ya walemavu nchini kwa lengo la kuboresha masuala yao ya kiafya na kuongeza uwezo wao.
9 - Kustawisha kwa wingi na kwa ubora bima za afya na matibabu kwa shabaha ya:
9 - 1 - Kuhakikisha watu wote nchini wanakuwa na bima za awali.
9 - 2 - Kushughulikiwa kikamilifu mahitaji ya kimsingi ya tiba na mashirika ya bima kwa ajili ya matabaka yote ya jamii na kupunguza hisa ya watu kuanzia gharama za matibabu hadi ifike mahala ambapo mgonjwa mbali na maumivu ya ugonjwa, asiteseke kwa wasiwasi na matatizo mengine yoyote.
9 - 3 - Kutoa huduma zaidi ya zile zinazotolewa na bima ya awali kupitia bima za nyongeza chini ya fremu ya ajenda za kisheria na za wazi kwa namna ambayo kiwango cha huduma za kimsingi za tiba wakati wote kiwe katika ubora unaotakiwa.
9 - 4 - Kuainisha kifurushi kikuu cha huduma za kiafya na kitiba katika kiwango cha bima za kimsingi na za nyongeza kupitia Wizara ya Afya na Matibabu na kununuliwa na mfumo wa bima na kuweko usimamiaji makini wa utekelezaji wa kina wa vifurushi vya afya kupitia kuondoa uchukuaji wa hatua za ziada na kujiepusha na gharama zisizo za dharura katika mchakato mzima wa matibabu, kuainisha ugonjwa hadi kwenye kutibu ugonjwa.
9 - 5 - Kutiwa nguvu soko la usimamiaji kwa ajili ya kutoa huduma za bima ya matibabu.
9 - 6 - Kubuni na kuainisha viwango vya ushuru wa huduma na usimamiaji wa masuala ya afya kwa kutegemea ushahidi uliopo kwa msingi wa thamani muhimu na kwa kuzingatia haki iliyoainishwa kiutaalamu na ya kweli ya watu na kwa kiwango kimoja na kutumiwa katika sekta za kiserikali na zisizo za kiserikali.
9 - 7 - Kufanyiwa marekebisho mfumo wa ulipaji uliosimama kwenye ubora wa utendaji, kuongeza ubora, kuleta mapato ya kiuadilifu na kuvutia misukumo chanya ya watu wanaotoa huduma na kuzipa mazingatio maalumu shughuli na kazi za kukuza ubora wa masuala ya afya na kinga katika maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo.
10 - Kudhamini vyanzo vya kifedha vya kudumu katika sekta ya afya kwa kusisitiza mambo yafuatayo:
10 - 1 - Kuweka wazi sheria za mapato, gharama na kazi.
10 - 2 - Kuongeza hisa ya masuala ya afya yanayooana na kuongezeka ubora katika kutoa huduma za afya na matibabu, kuanzia uzalishaji ghafi wa ndani ya nchi hadi kwenye bajeti ya umma ya serikali kwa namna ambayo itakifanya kiwango cha Iran katika suala hilo kuwa juu ya wastani wa kiwango hicho katika nchi za eneo la Masharitiki ya Kati kwa shabaha ya kutekeleza malengo ya muda mrefu na ufanikishaji wa malengo hayo.
10 - 3 - Kuwekewa vizuizi mazalisho, bidhaa na huduma zenye madhara ya kiafya.
10 - 4 - Kutolewa ruzuku kwa ajili ya sekta ya afya na kuhakikisha ruzuku hizo zinatolewa kwa shabaha na mipango maalumu kwa ajili ya afya na matibabu kwa lengo la kuleta uadilifu katika sekta ya afya na kuboresha masuala ya afya hususan katika maeneo yasiyo na huduma na kutoa misaada maalumu kwa matabaka ya wahitaji yenye kiwango cha chini cha mapato.
11 - Kuongeza welewa, kutekeleza ipasavyo majukumu, uwezo na ushiriki makini na wenye taathira kubwa wa watu binafsi, wanafamilia na watu wote katika jamii kwa ajili ya kudhamini, kulinda na kustawisha masuala ya usalama wa kifya kwa kutumia uwezo wa asasi mbali mbali, taasisi za kiutamaduni, kielimu na vyombo vya habari nchini, chini ya uangalizi na usimamiaji wa Wizara ya Afya, Matibabu na Elimu ya Tiba.
12 - Kusomwa upya, kubainishwa, kuenezwa na kustawishwa pamoja na kuwekewa misingi mizuri matibabu ya jadi na ya mitishamba.
12 - 1 - Kueneza tabia ya kupanda mimea ya dawa chini ya usimamizi wa Wizara ya Jihadi ya Kilimo na kusaidia na kuunga mkono ustawishaji wa ubunifu mbali mbali wa kielimu na kiufundi katika uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za madawa ya jadi chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya, Matibabu na Elibu ya Tiba.
12 - 2 - Kuandaa viwango na kuzifanya ya kisasa mbinu za kuainisha maradhi na matibabu kwa kutumia tiba ya jadi na vifaa vinavyotokana na tiba hiyo.
12 - 3 - Kubadilishana tajiriba na uzoefu na nchi nyingine katika uwanja wa tiba za jadi na za mitishamba.
12 - 4 - Usimamiaji wa Wizara ya Afya, Matibabu na Elimu ya Tiba kwa suala zima la kutoa huduma za tiba ya jadi na dawa za mitishamba.
12 - 5 - Kuleta miamala na mabadilishano ya kimantiki baina ya tiba za jadi na tiba za kisasa kwa ajili ya kuongeza kwa pamoja uzoefu na mbinu za matibabu.
12 - 6 - Kurekebisha mfumo wa maisha katika suala zima la lishe.
13 - Kustawisha kwa wingi na kwa ubora mfumo wa ufundishaji na utoaji elimu ya matibabu kwa sura ya kuangalia shabaha na malengo maalumu, kuzingatia masuala ya usalama wa kiafya, kuzingatia mahitaji ya watu katika jamii, kutoa majibu na kusimamisha uadilifu katika kulea nguvu kazi makini, bora, inayoheshimu maadili ya kazi na iliyojipamba kwa maadili ya Kiislamu, yenye utaalamu wa hali ya juu na yenye utambuzi na ustahiki unaotakiwa kwa kuzingatia mahitaji ya maeneo tofauti nchini.
14 - Kuleta mabadiliko ya kiistratijia katika utafiti wa elimu ya tiba kwa kuzingatia mfumo wa kisasa na mipango maalumu kwa ajili ya kupata marejeo ya kielimu katika sayansi na fani mbali mbali na kutoa huduma za afya na kuifanya Iran kuwa kambi kubwa ya masuala ya afya katika eneo la Asia ya kusini magharibi na katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.
 
< Nyuma   Mbele >

^