Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan Chapa
09/04/2014
Kiongozi Muadhamu Aonana na Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya leo (Jumatano) ameonana na Rais Ilham Aliyev wa Jamhuri ya Azerbaijan na kusisitiza kuwa, ujirani mwema na mifungamano ya kidini, kiutamaduni na kihistoria iliyopo baina ya nchi mbili ndiyo sababu kuu inayopelekea kustawi uhusiano baina ya dola hizi mbili na kuongeza kuwa: Inabidi uhusiano wa nchi hizi mbili na serikali za nchi hizo ustawi na kuimarika siku baada ya siku na kuondoa vizuizi vyote vinavyokwamisha uhusiano huo kwa kuwa na nia za kweli za kisiasa na kulipa uzito wa hali ya juu suala la kufuatilia vilivyo na kwa karibu wmakubaliano yanayofikiwa baina ya pande mbili.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kutia nguvu uhusiano baina ya wananchi na itikadi zao za kidini kuwa ndiko kunakoweza kuzidhaminia mafanikio serikali zilizoko madarakani na kuongeza kwamba: Si sahihi kuruhusu misimamo mikali ya baadhi ya mirengo ya watu ieneze chuki misimamo ya kufurutu ada ya kidini, na hivyo kuzusha mifarakano kati ya madhehebu mbali mbali ya Kiislamu na kwa njia hiyo kuvunja mshikamano na umoja wa kitaifa katika nchi za Waislamu.
Vile vile ameyataja mazungumzo na makubaliano yaliyofikiwa baina ya Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Azerbaijan na kuundwa kamisheni ya pamoja na kiuchumi kuwa ni jambo muhimu na kuongeza kwamba: Kiwango cha mabadilishano ya kiuchumi baina ya nchi mbili hizi kiko chini sana ikilinganishwa na uwezo na suhula za nchi hizo na kwamba ana matumaini ziara ya hivi sasa ya Rais wa Azerbaijan nchini Iran utakuwa ni utangulizi mzuri wa kustawishwa ushirikiano wa kiuchumi na wa kieneo baina ya nchi hizo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba kuweko nia ya kweli ya kisiasa na kupewa uzito masuala ya kuimarisha uhusiano wa nchi mbili ni mambo ya lazima katika suala hilo na kuongeza kuwa: Tab'an kuna baadhi ya watu na madola ya kibeberu ukiwemo utawala wa Kizayuni (wa Israel) hawafurahishwi na kustawi uhusiano baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan na muda wote wanafanya njama za kukwamisha uhusiano huo lakini iwapo masuala husika yatapewa uzito mkubwa na kama itakuweko irada na nia ya kweli ya kisiasa, itawezekana kabisa kushinda njama zote hizo.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan ameelezea kufurahishwa kwake na ziara yake ya nchini Iran na kusema kwamba anga ya mazungumzo ya pande mbili ilikuwa nzuri sana.
Ameongeza kuwa: Kamisheni ya pamoja ya kiuchumi ya Iran na Azerbaijan tayari imeanza kazi zake leo leo na kwamba ziara yake hii imeweka jiwe la msingi la kustawishwa uhusiano wa pande mbili katika nyuga zote zikiwemo sekta mbali mbali za ufundi na viwanda, biashara, usafiri na usafirishaji bidhaa pamoja na utalii.
Vile vile ameitaja misimamo mikali ya kidini kuwa ni hofu na wasiwasi wa pamoja wa nchi mbili za Iran na Azerbaijan na huku akitilia mkazo uwepo wa mifungamano ya kihistoria na kiutamaduni baina ya mataifa ya nchi hizi mbili amesema: Azerbaijan ina nia na irada ya kweli kabisa ya kustawisha uhusiano wake na Iran.
Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan vile vile amezitaja siasa huru na za kujitegemea za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni kigezo chema na za kipekee katika eneo hili na ulimwengu mzima kiujumla chini ya kivuli cha miongozo ya busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Azerbaijan inauhesabu uwezo na nguvu za Iran kuwa ni uwezo na nguvu zake na kwamb mifungamano madhubuti iliyopo baina ya nchi mbili haiwezi kuruhusu njama za maadui zitie doa katika uhusiano wa nchi hizi mbili.
 
< Nyuma   Mbele >

^