Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Wajumbe wa Kamati Kuu na wa Tamasha la Itikafu Waonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Chapa
05/05/2014
Wajumbe wa Kamati Kuu na wa Tamasha la Itikafu Waonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya KiislamuWajumbe wa Kamati ya Itikafu na wajumbe wa tamasha la tatu la Iran nzima la kielimu na kiutamaduni la itikafu, leo wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, shauku kubwa waliyo nayo watu wengi sana nchini Iran na namna wananchi wa nchi hii walivyoipokea kwa shauku kubwa ajabu sunna nzuri ya itikafu, ni miongoni mwa baraka za Mwenyezi Mungu na ni katika ushahidi na madhihirisho ya nguvu za Mapinduzi ya Kiislamu katika kuendesha mambo.
Amesisitiza kuwa, watu waliopewa dhamana ya kusimamia na kuendesha sunna hiyo ya Mtume wanapaswa kufanya kazi zao kwa mipangilio mizuri na yenye hekima nyingi na vile vile wafanye uchunguzi kuhusu mambo yanayoweza kudhoofisha sunna hiyo na kuandaa mazingira ya kuzifanya nyoyo za watu zizidi kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na zizidi kuwa safi kwa baraka za itikafu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameitaja ibada ya itikafu kuwa ni kuikabidhi kikamilifu roho kwa Mwenyezi Mungu katika kuilea kiibada nafsi sambamba na kuwa na shauku na hamu kubwa ya kujistawisha kimaanawi na kuongeza kuwa: Mapenzi makubwa yasiyoelezeka ya vijana wa Iran katika kushiriki vilivyo kwenye itikafu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu jambo ambalo leo hii linaonekana wazi kabisa katika misikiti yote ya Iran inabidi yaheshimiwe na yatukuzwe na yafanywe kuwa ni fursa muhimu yenye thamani kubwa.
Vile vile amebainisha kuwa, itikafu inapaswa isihusishwe na kitu kingine chochote isipokuwa ibada na mtu kumzingatia Mola wake Mtukufu na kuongeza kuwa: Kufundisha na kuizoesha nafsi kuishi na kuamiliana na watu wengine Kiislamu, kuwa na uhusiano wa kirafiki na wa kidugu na watu wengine waliomo katika itikafu na vile vile kufunzwa mafundisho wa dini, ni miongoni mwa fursa nyingi zinazopatikana katika ibada iliyojaa nuru ya itikafu.
Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuwa na mipangilio makini na wajibu wa kufanya uchunguzi wa kina na unaotakiwa kuhusu masuala yanayoweza kuharibu moyo na maana halisi ya itikafu kuwa ni jambo la dharura na kusisitiza kwamba, katika mipangilio hiyo inabidi jambo la asili liwe ni kuzikurubisha nyoyo na roho za wanaofanya itikafu kwa Mwenyezi Mungu na katika upande wa pili kumuondoa kikamilifu mtu aliyemo katika itikafu kwenye mazonge yaliyozoeleka katika jamii na mashaka yaliyojaa katika maisha yake ya kila siku.

 
< Nyuma   Mbele >

^