Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Waziri Mkuu wa Pakistan Aonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Chapa
12/05/2014
Supreme Leader Meets with Prime Minister of PakistanAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na Waziri Mkuu wa Pakistan, Bw. Nawaz Sharif na ujumbe alioandamana nao na kutaja sababu kuu ya kuweko uhusiano mzuri na wa kidugu baina ya mataifa mawili ya Iran na Pakistan kuwa ni kuwepo mambo mengi yanayowaunganisha pamoja wananchi wa nchi hizi mbili ya kiutamaduni na kidini na wakati huo huo ameelezea kusikitishwa kwake na kupunguwa kiwango cha ushirikiano wa nchi hizi mbili katika masuala ya kiuchumi akisema kuwa: Kuna mikono ya kigeni ambayo inatumia mbinu mbali mbali kama vile kuleta ukosefu wa amani katika mpaka mrefu wa pamoja wa nchi hizi mbili ili kuzusha mpasuko baina ya mataifa mawili ndugu na rafiki ya Iran na Pakistan na baina ya tawala za nchi hizo, hivyo inabidi watu wawe macho na wasiruhusu kupotea fursa nzuri na kubwa ya kustawisha uhusiano baina yao.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia umuhimu wa kupanuliwa uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan kadiri inayowezekana na kutekelezwa kivitendo miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na mradi wa bomba la gesi ya Iran kuelekea Pakistan.
Aidha amemkhutubu Waziri Mkuu huyo wa Pakistan akimwambia: Ni matumaini yangu kuwa, katika kipindi cha utawala wa wa serikali yako nchini Pakistan, kutashuhudiwa harakati nzuri katika uhusiano wa nchi hizi mbili kwenye nyuga tofauti.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amesisitiza kuwa, katika kustawisha uhusiano wa pande mbili, nchi mbili za Iran na Pakistan hazipaswi kusubiri idhini kutoka kwa mtu yeyote yule na kuongeza kuwa: Marekani ambaye ukhabithi wake uko wazi kwa kila mtu, ni miongoni mwa tawala ambazo zinafanya njama za kuzusha mpasuko baina ya Iran na Pakistan, na tab'an mbali na Marekani yako madola mengine nayo yanafanya njama hizo hizo.
Vile vile ameashiria vitendo vya ukosefu wa amani vilivyotokea katika baadhi ya maeneo ya mpaka wa Iran na Pakistan katika miezi ya hivi karibuni na kusema kuwa: Kuna baadhi ya watu wanafanya njama za makusudi za kuharibu usalama katika mpaka mrefu wa nchi hizi mbili na sisi hatuwezi kuamini kuwa matukio hayo yanatokea vivi hivi tu bila ya kufanywa kwa makusudi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza kuwa: Tab'an sisi tuna taarifa za kuaminika zinazoonesha kuwa kuna harakati zinafanyika katika eneo la Baluchistan Pakistan kwa lengo la kuharibu usalama katika mipaka ya nchi hizi mbili.
Ayatullah Udhma Khamenei ameyataja makundi ya kitakfiri kuwa ni hatari kwa Waislamu wote, wawe Waislamu wa Kishia au Waislamu wa Kisuni na kuongeza kuwa: Kama hakutafanyika jitihada za kupambana na makundi ya kitakfiri, basi makundi hayo yatatoa pigo kubwa na kuuletea madhara zaidi ulimwengu wa Kiislamu.
Mwishoni mwa miongozo yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea matumaini yake kuwa uhusiano wa Iran na Pakistan utazidi kuimarika siku baada ya siku.
Bw. Jahangiri, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran naye amehudhuria mazungumzo hayo.
Katika mazungumzo hayo, Bw. Nawaz Sharif, Waziri Mkuu wa Pakistan ameelezea kufurahishwa kwake na safari yake ya kutembelea Iran na kuonana tena na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Vile vile ameashiria kumbukumbu nzuri za safari ya Ayatullah Udhma Khamenei huko nchini Pakistan na mjini Lahore na kusema: Mimi wakati wa safari yako hiyo nilikuwa Waziri Kiongozi wa jimbo la Punjab ambalo makao makuu yake ni Lahore na kwamba mapokezi makubwa sana uliyoyapata na mapenzi makubwa yaliyooneshwa na wananchi wa Pakistan kwako yanazidi kuthibitisha ni kiasa gani mataifa yetu haya mawili yalivyo na mfungamano mkubwa wa kiutamaduni, kidini na kihistoria.
Waziri Mkuu wa Pakistan vile vile ameashiria mazungumzo mazuri aliyoyafanya na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu mjini Tehran na kuongeza kwa kusema: Nitafanya juhudi zangu zote kuhakikisha kuwa kiwango cha uhusiano wa kiuchumi wa nchi hizo mbili kinakuwa na kustawi zaidi na mbali na kurejea katika kiwango cha dola bilioni tatu kwa mwaka kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, kiwango hicho kipande na kiongezeke zaidi na nitafanya juhudi za kuhakikisha kuwa mradi wa bomba la gesi unahuishwa.
Waziri Mkuu wa Pakistan pia ameelezea kusikitishwa sana na vitendo vya uvujifu wa amani vilivyotokea katika miezi ya hivi karibuni kwenye baadhi ya maeneo ya mpaka wa nchi hizi mbili na huku akiutilia nguvu uhakika wa kuweko mikono ya nje inayojaribu kuzusha mpasuko baina ya nchi hizi mbili ndugu na amemuhakikishia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akimwambia: Ninapenda kukuhakikishia kuwa, serikali ya Pakistan haitafumbia jicho wala kudharau hatua yoyote ile ya kupambana na wanaohatarisha amani katika mipaka ya nchi hizi mbili, na itaendelea kuunga mkono hatua za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uwanja huo.
 
< Nyuma   Mbele >

^