Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mkutano wa Kiongozi Muadhamu na Waendeshaji wa Kongamano la Kumuenzi Ayatullah Mishkini Chapa
15/05/2014
Mkutano wa Kiongozi Muadhamu na Waendeshaji wa Kongamano la Kumuenzi Ayatullah MishkiniLeo asubuhi(Alkhamisi), Hujjatul Islam Walmuslimin Mohammad Golpayegani, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesoma matini ya hotuba ya Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na waandaaji na waendeshaji wa kongamano la kumuenzi Ayatullah Mishkini tarehe 28 Farvardin 1391 (mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia sawa na Aprili 16, 2012 Milaadia).
Hujjatul Islam Walmuslimin Golpayegani amesoma matini ya hotuba hiyo leo katika kongamano la kumuenzi aalimu huyo mwanaharakati lililofanyika katika Taasisi ya Kielimu na Kiutamaduni ya Darul Hadith, mjini Qom.
Katika mkutano wake na waitishaji wa kongamano hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria shakhsia isiyo na mbadala na isiyo na kifani ya Ayatullah Mishkini na kusema kuwa: Marhum Ayatullah Mishkini, mbali na upande wake wa kidini, kimaadili, kisiasa na taqwa, alikuwa pia mtu mwenye dhuku nzuri na anayependa na kuvutiwa na uzuri wa vitu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile alizungumza kwa kusisitiza kuhusu shakhsia iliyokusanya mambo mengi sana ya Ayatullah Mishkini na historia yake ndefu ya kushiriki vilivyo katika mapambano ya kimapinduzi na akaongeza kuwa: Ni jambo linalostahiki kabisa kumuenzi Ayatullah Mishkini na kusambaza maandishi na athari zake nyingine.
 
< Nyuma   Mbele >

^