Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Jumuiya ya Watu Wanaojitolea Kujenga Mashule Nchini Iran Chapa
17/05/2014
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Jumuiya ya Watu Wanaojitolea Kujenga Mashule Nchini IranAlasiri ya leo (Jumamosi) kumefanyika tamasha la ngazi ya mkoa la watu wanaojitolea kujenga mashule katika mkoa wa Tehran. Tamasha hilo limefanyika kwenye ukumbi wa makongamano ya kimataifa wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Katika kongamano hilo kumetangazwa pia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na wajumbe wa jopo la uongozi wa Jumuiya ya Watu Wanaojitolea Kujenga Mashule nchini Iran, mkutano ambao ulifanyikaa tarehe 5 Mei 2014.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kuwa, kuwepo majimui ya watu wanaojitolea kujenga mashule nchini Iran ni jambo muhimu sana na ni miongoni mwa baraka nyingi za Mapinduzi ya Kiislamu.
Vile vile ameashiria namna wananchi wanavyohisi kuwa ni jukumu lao kushiriki katika harakati mbali mbali za kheri na kusisitiza kuwa: Nukta hii nayo ni muhimu sana kwamba wananchi hawasiti hata kidogo kujitokeza na kushiriki kwa hamasa kubwa katika mambo ya kheri kila wanapohisi pana ulazima wa kufanya hivyo.
Ameongeza kuwa: Katika kila sehemu ambayo tumepata nguvu na msukumo wa kuonesha kazi na njia sahihi - bila ya kutegemea - wananchi walijitokeza kwenye kazi hiyo na kushiriki vilivyo ndani yake na mfano wa wazi wa jambo hilo ni namna wananchi walivyojitolea na kushiriki vilivyo katika kulihami taifa wakati wa vita vya kujihami kutakatifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema: Hatua ya wananchi ya kulipa uzito suala la kujenga mashule inaonesha namna jamii ya Iran ilivyoelewa umuhimu wa kuwasomesha na kuwaelimisha watoto wao.
Ayatullah Udhma Khamenei aidha ameashiria kuwa, kila kazi ambayo viongozi na maafisa wakuu wa Iran wameikabidhi kwa wananchi, kazi hiyo imefanikiwa na kupata maendeleo makubwa.
Ameongeza kuwa: Huu ni uzoefu mzuri sana kwamba, kila wakati kazi ilipokabidhiwa kwa nguvu adhimu na isiyo na mwisho ya wananchi, kazi hiyo ilistawi na kufanikiwa.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa nasaha tatu kuhusiana na suala jema la kujenga mashule.
Nasaha za kwanza ni kwamba; watu ambao wameingia katika jambo jema la kujitolea kujenga mashule, wanapaswa kuliendeleza jambo hilo kwa shauku, msukumo na mapenzi makubwa na wajue kuwa ni hiyo sadaka yenye kuendelea na isiyo na mwisho.
Nasaha zake za pili zimevilenga vyombo vya habari na hasa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB ya kwamba vyombo hivyo vina jukumu la kuwaelimisha na kuwajulisha vizuri wananchi kuwepo kwa jambo hili muhimu.
Na nasaha za tatu na za mwisho za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zilihusiana na wajibu wa kuweko ushirikiano mzuri baina ya Wizara ya Elimu na Malezi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na watu wanaojitolea kujenga mashule pamoja na kuzingatiwa sana umadhubuti na uimara wa shule zinazojengwa.
 
< Nyuma   Mbele >

^