Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu Chapa
03/06/2014
Supreme Leader Meets with Participants of 31st Quran CompetitionsAnga ya Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) mjini Tehran imehinikiza uturi wa kutuliza nyoyo wa maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu, katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kutukufu Imam Zaynul Abidin, Aliyyu bnil Husain maarufu kwa lakabu ya Imam Sajjad AS. Wahadhiri, maqarii na "mahufadh" bora wa mashindano ya thelathini na moja ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu, wamefanya mahafali ya kuwa na mapenzi na kuwa karibu na Qur'ani Takatifu, mahafali ambayo yamehudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja lengo la mwisho na kuu la kuhifadhi na kusoma Qur'ani kuwa ni kuelewa na kutendea kazi mafundisho yake pamoja na kuwa na ukuruba na mapenzi makubwa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu.
Aidha amebainisha kuwa, uongofu wa Mwenyezi Mungu na kufahamu vigezo vikuu vya Qur'ani katika masuala nyeti kama vile kumtambua adui, ni mambo ambayo yanapatikana kupitia kuwa na ukuruba na mapenzi na Qur'ani Takatifu.
Amesisitiza kuwa: Kuwa karibu na Qur'ani Tukufu, kuwa na tadibiri na kuzama ndani ya maana na mafundisho ya Kitabu hicho kitukufu, ndiko kutakakouletea umma wa Kiislamu heshima uliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, hatua ya mabarobaro na vijana wa Iran ya kuipokea vizuri harakati ya Qur'ani nchini Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ameongeza kuwa: Mapenzi na kuwa karibu na Qur'ani, kunaifanya jamii izidi kuwa karibu na utekelezaji wa mafundisho muhimu sana ya kitabu hicho na kwamba hilo ndilo lengo bora zaidi na la juu kabisa la kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.
Vile vile amesema, kuwa karibu na Qur'ani Takatifu ni ishara ya kuwa tayari moyo wa mwanadamu kwa ajili ya kupokea uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa: Matatizo makubwa yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu leo hii yanatokana na ulimwengu huo kujiweka mbali na mafundisho ya Qur'ani na matokeo yake ni Waislamu kughafilika na njama na ukhabithi wa maadui wa Uislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameitaja njia ya kufidia mapungufu hayo makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu kwamba ni kuwa na welewa wa kina kuhusiana na vigezo vya Qur'ani Tukufu na kufafanua zaidi kwa kusema: Baada ya kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, maadui wa Uislamu walizidisha njama zao dhidi ya Uislamu na kuzifanya tata zaidi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema: Siasa za maadui wa Uislamu ni kuzusha vita vya ndani vya kupokezana, na kuwafanya ndugu kuuana wao kwa wao katika jamii za Waislamu, na kwamba kitu kinachosikitisha zaidi ni kuwa, kuna baadhi ya watu katika umma wa Kiislamu hawazioni siasa hizo za maadui na wako tayari kushirikiana na mashetani kuendesha vita dhidi ya ndugu zao Waislamu, bali wako tayari hata kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Waislamu wenzao.
Vile vile amewashukuru wote walioendesha na walioshiriki mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu na kuongeza kuwa: Umma wa Kiislamu unaweza kufikia kwenye heshima uliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa baraka za kuwa na mapenzi na kuwa karibu na Qur'ani Tukufu.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammadi, Mwakilishi wa Faqihi Mtawala ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Wakfu na Mambo ya Kheri ya Iran, ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa sikuu za mwezi wa Shaaban hususan sikukuu ya kukumbuka siku ya kuzaliwa Imam Sajjad Alayhis Salaam na huku akiashiria kiwango cha juu cha mashindano hayo na jinsi mashindano ya mwaka huu ya 31 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalivyopokewa na washiriki wengi kutoka mataifa tofauti amesema: Katika mashindano ya mwaka huu, nchi 71 za mabara tofauti duniani zimetuma wawakilishi wao ambapo mashindano hayo yalisimamiwa na majaji 10 kutoka nje na watano kutoka Iran huku wajumbe watatu wakiwa ni watazamaji.
 
< Nyuma   Mbele >

^