Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Hadhara ya Watu wa Mashairi na Fasihi Chapa
12/07/2014
 Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei leo usiku (Jumamosi) ambayo imesadifiana na usiku wa kukumbuka siku ya kuzaliwa "Karimu Ahlul Bayt" Imam Hasan al Mujtaba, Alayhis Salaam, ameonana na hadhara ya watu wa utamaduni, shaha wa malenga na wahadhiri wa tungo za kishairi na fasihi ya Kifarsi, malenga chipukizi na majimbi wa tungo za kifarsi nchini Iran pamoja na washairi wa lugha hiyo kutoka nchi za Tajikistan, India, Afghanistan na Pakistan.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Imam Hasan al Mujtaba AS kama ambavyo ametoa pia nasaha juu ya umuhimu wa kustafidi vizuri na kutumia kwa njia bora pepo shwari za kimaanawi na tukufu za mikesha ya Laylatul Qadr. Amesema jukumu la kwanza kabisa na la asili la tungo za kishairi ni kuakisi na kutoa majibu kwa fikra, hisia na dukuduku za malenga na kuongeza kuwa: Tab'an kazi kuu ya utungo wa kishairi ni: ni kuingia na kuathiri faragha ya akili na chemba za nyoyo za watu na kuwalisha fikra walengwa.
Vile vile ameashiria njama za mashetani za kujipenyeza kwenye sehemu pweke ndani ya fikra za watu na kupandikiza humo fikra za kishetani akisisitiza kuwa: Malenga ana jukumu - kama walivyofanya majimbi na mashaha wa malenga katika historia ya Kifarsi - la kuingia kwenye faragha na chemba za fikra na nyoyo za watu, kuikhutubu sehemu pweke katika fikra na nyoyo za walengwa na kuzijaza matukufu ya kiroho na kimaanawi na kuzitajirisha kwa kupuliza humo roho ya matumaini, uchangamfu, harakati na maendeleo. Amesema, mambo hayo ndizo ngao na nguzo muhimu za kujenga muundo halisi wa taifa la Iran na kulifanya imara taifa hilo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kupambana na mambo maovu katika jamii kuwa linategemea watu wenyewe kujirekebisha wao wenyewe kwanza na kuwa na misukumo ya maana, matumaini na harakati nzuri.
Amma kuhusu faida za kijamii za tungo za kishairi amesema: Vielelezo za kiutamaduni, manufaa na faida za kiutamaduni ndiyo mambo yanayotoa sura na muundo wa kiutamaduni wa taifa fulani; na kwamba tungo za kishairi nazo zinapaswa kulinda muundo huo wa kitaifa, na kuutajirisha na kuhakikisha unakuwa safi.
Akibainisha umuhimu wa utambulisho wa kiutamaduni, Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Utambulisho wa kiutamaduni ndicho hicho kitu kinachoitwa "urazini na mantiki ya kimaanawi" na "busara ya watu wote" na kwamba mambo hayo ndiyo asili na chemchemu cha maisha na vitu vinavyolipambanua taifa moja mbele ya taifa jingine. Amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran na Imam wetu mtukufu (Imam Khomeini - quddisa sirruh) naye amechimbuka na kuleleka kutoka katika utambulisho huo huo wa kiutamaduni na kuweza kpambika kwa hekima kubwa na fikra aali.
Amesema kuwa, kuweko misukumo muhimu inayotakiwa katika kulinda utambulisho wa kiutamaduni huandaa uwanja wa kupatikana hisia za udharura wa kila mtu kutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kupambana na mashambulizi ya waziwazi ya adui kwa utambulisho huo wa kitaifa.
Amesema: Tatizo la baadhi ya watu ni kuwa, hawaoni asili ya mashambulizi makubwa mno ya kambi iliyokula kiapo cha kushambulia utambulisho wa Kiislamu na utambulisho wa kiutamaduni wa taifa la Iran, licha ya kwamba mashambulizi hayo ya adui yako wazi kabisa, amma malenga na watungaji wa tungo za kishairi wao husimama imara kulinda utambulisho huo kwa kutumia vipaji vyao vya kisanaa, kuona kwao mbalimbali na uwezo wao kugundua nukta angalifu na madukuduku yaliyopo katika jamii.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea na hotuba yake kwa kukumbushia matukio machungu yanayotokea hivi sasa duniani kama vile hujuma za madola ya kibeberu dhidi ya uhuru, utajiri, dini, umaanawi, kunga za kijamii na maadili ya mataifa mengine pamoja na kupindua kwao ukweli na uhalisia wa mambo kwa kutumia ubeberu wao wa kipropaganda na kuashiria matukio machungu yanayoshuhudiwa hivi sasa katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mashambulizi ya kikatili yanayoendelea sasa hivi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo wasio na ulinzi akisema: (Inasikitisha kuona kuwa) baadhi ya wakati (madola ya kibeberu) yanazusha makelele makubwa mno ya kipropaganda duniani kwa sababu ya kuuliwa mnyama fulani tu, lakini mashambulizi ya hivi sasa huko Ghaza ambayo (hadi hivi sasa) yameshapelekea kuuawa zaidi ya watu 100 tena basi watoto wadogo, wasio na hatia - malaika wa Mungu - waliodhulumiwa; si tu ukatili huo hauyashughulishi madola hayo ya kibeberu lakini hata imefikia kuwa, Marekani na Uingereza zimejitokeza hadharani na kuunga mkono rasmi mashambulizi hayo ya kinyama.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Ukweli wa mambo ulivyo hivi sasa duniani ni kuwa, madola ya kibeberu yanaunga mkono bila haya wala soni, kila jambo baya, ovu na kila ufasidi na najisi ambayo itadhamini maslahi yao na katika upande wa pili yanakabiliana kinyama na kwa ukatili mkubwa na kila kitu kisafi na kitukufu ambacho kinakinzana na maslahi yao.
Baada ya kubainisha uhakika huo mchungu, Ayatullah Udhma Khamenei ameuliza swali akisema: Malenga - ambaye ana hisia, welewa wa kina, ufahamu na nguvu kubwa za kubainisha vizuri mambo - ana jukumu gani mbele ya matukio hayo na hali iliyopo hivi sasa?
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu swali hilo akisema: Jukumu la malenga na mtungaji wa tungo za kishairi ni kutumia kipaji chake ambacho kwa hakika ni neema na hujja mbele ya Mwenyezi Mungu, kuiunga mkono kambi inayodhulumiwa na kutangaza haki na uhakika wa mambo kwa kutumia kipaji chake cha kishairi.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea kufurahishwa kwake na mafanikio na hatua nzuri zilizopigwa na malenga nchini Iran hususan malenga chipukizi na tungo zinazohusiana na Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Sharti kuu linaloweza kuufanya utungo wa kishairi ukumbukwe milele na uwe na taathira kubwa ni kwamba mbali na kutakiwa kuwa na madhumuni na maana nzuri, utungo wa kishairi unapaswa pia kuwa na muundo na sura bora kabisa ya kisanii.
Kabla ya hotuba ya Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, malenga kadhaa chipukizi na majimbi wa tungo za kishairi za lugha ya Kifarsi wamesoma baadhi ya tungo zao mbele ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
 
< Nyuma   Mbele >

^