Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Rais na Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Chapa
12/07/2014
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alasiri ya leo (Jumatatu) ameonana na Rais pamoja na Baraza la Mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuzungumzia kwa muhtasari baadhi ya mafundisho matukufu na aali yaliyomo kwenye kitabu cha Nahjul Balagha na nukta kadhaa za kiakhlaki na kimaadili.
Katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ushahidi kutoka katika nukta mbali mbali za amri ya kiserikali ya Amirul Muminin Ali Alayhis Salaam kwa Malik Ashtar na kutumia miongozo hiyo ya Imam Ali AS kutoa nasaha jumla kuhusu wajibu wa kuilinda "Baytul Maal" - hazina ya nchi - na udharura wa kuwa na hisia kali katika matumizi ya hazina hiyo, pamoja na wajibu wa kujiepusha na kuchukua hatua kwa pupa kutokana na hasira, kujiweka mbali na tabia ya kuwa na misimamo mikali, maneno ya hasira na kuhamaki hamaki pamoja na majivuno na kiburi.
Ameongeza kuwa: Imam Ali Alayhis Salaam alitufundisha kwamba, njia pekee ya kuweza kuepukana na matendo na sifa hizo mbaya kuwa ni mtu kuidhibiti nafsi yake kupitia kuwa na mfungamano wa kimoyo, kimaanawi na kivitendo na Mola wake Mtukufu.
Ayatullah Udhma Khamenei pia amesema, kuisoma kwa mazingatio Qur'ani Tukufu pamoja na kutumia vizuri fursa ya mwezi wa Ramadhani kwa kutekeleza ipasavyo amali zake ni miongoni mwa njia bora kabisa za kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kuidhibiti nafsi.
Baada kuzungumzia nukta za kiakhlaki na kimaadili, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia masuala ya kiutamaduni na kugusia wasiwasi uliopo kuhusu masuala hayo akisisitiza kuwa, makosa ya kiutamaduni si kitu ambacho kinaweza kufidiwa kirahisi.
Ameongeza kuwa: Ni jambo la dharura kuzijua vizuri siasa za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuzitekeleza kivitendo siasa hizo katika masuala ya utamaduni.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Kubadilisha njia ya masuala ya kiutamaduni kwa hali yoyote ile na kutoka katika fremu na kalibu ya siasa za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu kutavuruga nidhamu ya kifikra na utambulisho wa kweli wa jamii ya Iran.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia masuala ya ukulima na huku akielezea wasiwasi wake kutokana na kubadilishwa na kutumiwa visivyo ardhi za kilimo amesema: Kuharibu ardhi za kilimo ni kutia hasara isiyofidika kabisa na inabidi Wizara ya Jihadi ya Kilimo na Taasisi ya kulinda mazingira zilifuatilie kwa uzito wa hali ya juu suala hilo.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia matukio ya kusikitisha yanayoendelea hivi sasa katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina na mauaji ya kinyama yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina hususan wanawake na watoto wadogo na kusema kuwa msimamo na hatua zilizochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na serikali yake ni nzuri sana.
Amesisitiza kuwa: Masuala ya Ghaza kwa kweli yanasikitisha mno na kwamba utawala wa Kizayuni unatumia mghafala uliotawala katika ulimwengu wa Kiislamu kufanya jinai hizo kubwa huko Palestina.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kitendo cha Wazayuni maghasibu cha kuwaua kinyama wananchi wa Ghaza kilipaswa kuziamsha tawala na mataifa ya Waislamu ili ziweke pembeni tofauti zao na kuungana na kuwa kitu kimoja.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Hujjatul Islam Walmuslimin Hasan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ripoti fupi kuhusu kazi zilizofanywa na serikali yake tangu ilipoingia madarakani miezi 11 iliyopita.
Amesema: Kuleta utulivu katika sekta na sehemu mbali mbali nchini, kudhibiti mfumuko wa bei, kufanya juhudi za kuondoa tatizo la kuzorota kiuchumi na kuleta ustawi wa kiuchumi, kuanza kutekeleza awamu mpya wa mpango wa kutoa ruzuku kwa malengo maalumu, kudhamini usalama wa chakula kwa matabaka ya watu dhaifu, kupunguza gharama za matibabu na kuwaweka wananchi wote wa Iran ndani ya huduma za bima, kuweka mipango ya kukabiliana na matatizo ya mazingira, kudhibiti maji ya mipakani na kuufanya kuwa wa kisasa mfumo wa ukulima nchini pamoja na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mafuta na gesi ni miongoni mwa kazi na mipango ya serikali ya 11 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Rais Rouhani ameongeza kuwa, mafanikio ya serikali yanatokana na taufiki na msaada wa Mwenyezi Mungu, uungaji mkono wa wananchi na msaada wa kila upande wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kwamba: Ni matumaini yangu kuwa, juhudi hizi za serikali zitayaletea mustakbali mzuri matabaka yote ya wananchi wa taifa la Iran.
Mwishoni mwa mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Khamenei, amewasalisha hadhirina Sala za Magharibi na Isha na baadaye kula futari pamoja naye.
 
< Nyuma   Mbele >

^