Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Habari za Karibuni Kabisa Kuhusu Upasuaji Aliofanyiwa kwa mafanikio Kiongozi Muadhamu Chapa
08/09/2014
 Supreme Leader undergoes successful surgeryAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo Jumatatu asubuhi amefanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) katika hospitali moja ya umma na Alhamdulillah operesheni hiyo imefanyika kwa mafanikio makubwa.
Kabla ya kuelekea hospitalini, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza na mwandishi wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB na kusema: Mimi hivi sasa ninaelekea hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.
Ameongeza kuwa: Tab'an hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Hata hivyo, hiyo haina maana ya kwamba wananchi wasiniombee dua, lakini Inshaallah hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani huu ni upasuaji wa kawaida kabisa.
Mwishoni mwa maelezo yake Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Inshaallah rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu zitaambatana na upasuaji huo na mambo yote yatafanyika vizuri sana.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na timu ya madaktari imeuhakikishia umma kuwa hali ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inaendelea vizuri sana.
 
< Nyuma   Mbele >

^