Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hali ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni Nzuri Kikamilifu na ni ya Kawaida Kabisa Chapa
08/09/2014
Head of Medical Team: Supreme Leader in Good HealthBaada ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) leo asubuhi kwa mafanikio makubwa, Daktari Marandi, mkuu wa timu ya madaktari wa Kiongozi Muadhamu amefanyiwa mahojiano na kuelezea kuridhishwa kikamilifu na mchakato mzima wa kazi hiyo ya leo ya upasuaji. Daktari Marandi amesema kuwa, upasuaji huo umefanyika bila ya kupigwa dawa ya kulaza, bali imepigwa ganzi sehemu iliyokusudiwa kufanyiwa upasuaji na hali ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni nzuri kikamilifu na ni ya kawaida kabisa.
Daktari Marandi vile vile amesema: Upasuaji wa tezi kibofu ni kazi nyepesi sana kwa watu wenye umri mkubwa na hata kwa watu wenye umri wa kati na mara nyingi huhitajika kutolewa kabisa tezi kibofu.
Amesema, kwa muda sasa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa na tatizo hilo na hivi sasa ndipo madaktari walipoona kuwa ni wakati unaofaa kabisa kufanyika upasuaji huo, na kwamba Kiongozi Muadhamu hakuwa na njia nyingine isipokuwa kukubali ushauri wa madaraktari.
Mkuu wa timu ya madaktari wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusu mchakato wa kufanyika upasuaji huo kwamba: Upasuaji huo umefanyika leo asubuhi kwa muda wa chini ya nusu saa. Kilichofanyika ni kupigwa ganzi tu sehemu palipokusudiwa kufanyiwa upasuaji bila ya kuhitajika kutumika dawa za kulaza na wala kugusa sehemu nyingine zisizotakiwa.
Ameongeza kuwa: Katika muda wote wa upasuaji, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa na fahamu zake kamili na alikuwa akizungumza kama kawaida na hivi sasa pia hali yake ni nzuri na amenitaka niwatoe wasiwasi wananchi kwa kuwaeleza hali yake.
Daktari Marandi ameashiria namna Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alivyosisitizia sana kufanyika upasuaji huo katika hospitali ya umma na kuongeza kuwa: Kiongozi Muadhamu amesisitiza sana kwamba wagonjwa wengine katika hospitali hiyo wasisumbuliwe na ndio maana upasuaji umefanyika mapema asubuhi.
Akijibu swali kuhusu wakati ambapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ataruhusiwa kurudi nyumbani, Daktari Marandi amesema, mara nyingi wagonjwa wote wanaofanyiwa upasuaji wa namna hiyo kubakishwa hospitalini kwa muda wa siku tatu hadi tano ili kuangaliwa hali zao na jambo hilo litafanyika pia kwa Kiongozi Muadhamu.
Ameendelea kusema: Baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani pia, kama ilivyo kwa wagonjwa wengine wote, itabidi na yeye awekewe miko na ijapokuwa Kiongozi Muadhamu kwa kawaida ni mtu madhubuti mwilini na ni mchapakazi mahiri mwenye harakati nyingi, lakini atalazimika apunguze mashinikizo ya kazi zake kwa wiki kadhaa kama ambavyo baadhi ya kazi zake pia itabidi aziache kabisa. Tab'an anavyopenda yeye mwenyewe ni kuwa hali yake iwe nzuri haraka ili aweze kurejea haraka katika kazi zake za kawaida.
Vile vile mkuu wa timu ya madaktari wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameishukuru timu nzima ya madaktari waliofanya upasuaji huo na hosptali alikofanyiwa upasuaji kwa jitihada zao kubwa za kutekeleza kwa mafanikio upasuaji huo na kuwashukuru wananchi wa Iran kwa dua zao zilizojaa ikhlasi za kumuombea salama Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 
< Nyuma   Mbele >

^