Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Rais Hassan Rouhani Amtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Hosptalini Chapa
08/09/2014
President Hujjat ul-Islam Rohani Visits Supreme Leader in HospitalRais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi amekwenda hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate).
Akiwa hospitalini hapo, Rais Rouhani amemuomba Mwenyezi Mungu ampe ahueni ya haraka Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Baada ya kumjulia hali Kiongozi Muadhamu, Rais Rouhani amezungumza na waandishi wa habari na kuelezea kuridhishwa kwake na hali aliyomuona nayo Kiongozi Muadhamu na kutokana na kufanyika kwa mafanikio makubwa upasuaji huo na kwa jinsi madaktari wanavyomtunza baada ya upasuaji. Amesisitiza kuwa: Watu wote wanapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu na amuongezee mafanikio Kiongozi Muadhamu katika kulitumikia taifa la Iran na ulimwengu mzima wa Kiislamu.
Vile vile Rais Rouhani amesema kuwa hali jumla ya Kiongozi Muadhamu ni nzuri sana, ni mzima na yuko salama kabisa. Amesema machofu linakuwa ni jambo la kawaida kabisa baada ya upasuaji na kwamba timu ya madaktari bingwa imefanya upasuaji huo kwa namna iliyo bora kabisa na katika upande wa kutunzwa na kuhudumiwa baada ya upasuaji pia bila ya shaka kunafanyika kwa umakini huo huo wa hali ya juu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, dua za wananchi wa Iran kwa ajili ya Kiongozi Muadhamu ni dua za daima na za kila siku na kuongeza kuwa: Hali ya Kiongozi Muadhamu ni nzuri sana, hivyo wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi kabisa, lakini pamoja na hayo waendelee kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu kama kawaida yao ili aendelee kuwa salama.
Rais Rouhani amegusia pia safari yake ya nje ya nchi ambayo ilikuwa imeshapangwa tangu zamani na kuongeza kuwa: Hamu yangu ni kwamba nibakie Tehran, lakini Kiongozi Muadhamu mwenyewe amenieleza kuwa niendelee na safari yangu hiyo kama ilivyopangwa.
 
< Nyuma   Mbele >

^