Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Viongozi na Shakhsia wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
08/09/2014
Officials Visit Supreme Leader in HospitalLeo jioni (Jumatatu) Ayatullah Amoli Larijani, Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Jannati, Katibu wa Baraza la Walinzi wa Katiba na Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Hassan Khomeini, wamekwenda hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) na kuelezea kuridhishwa kwao na hali nzuri waliyomuona nayo Kiongozi Muadhamu, na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu uliojaa baraka.
Itakumbukwa kuwa, mapema leo asubuhi (Jumatatu) Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefanyiwa kwa mafanikio upasuaji wa tezi kibofu ambapo Daktari Marandi, mkuu wa timu ya madaktari wa Kiongozi Muadhamu ameelezea kuridhishwa kwake kikamilifu na jinsi zoezi zima la upasuaji lilivyofanyika. Amesema, upasuaji umefanyika kwa muda wa chini ya dakika 30 na kilichofanyika ni kupigwa ganzi sehemu iliyokusudiwa kufanyiwa upasuaji tu bila ya kuhitajika dawa ya kulaza.
Leo asubuhi pia na baada ya kufanyika upasuaji huo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu amekwenda kumtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Hospitalini. Rais Rouhani ameelezea kuridhishwa kwake na namna kazi ya upasuaji ilivyofanyika kwa umakini wa hali ya juu na timu ya madaktari bingwa akisisitiza kuwa, inabidi sote kwa umoja wetu tumshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na hali nzuri ya kiafya aliyomkuta nayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 

 
< Nyuma   Mbele >

^