Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Katibu Mkuu wa Hizbullah Aelezea Kufurahishwa kwake na Hali Nzuri ya Kiafya ya Kiongozi Muadhamu Chapa
08/09/2014
 Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon, leo jioni (Jumatatu) amepiga simu kuulizia hali ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu mapema leo asubuhi.
Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea kufurahishwa kwake mno baada ya kusikia kwamba hali ya Kiongozi Muadhamu inaendelea vizuri na amemuomba Mwenyezi Mungu ampe afya kamili haraka iwezekanavyo.
Itakumbukwa kuwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefanyiwa kwa mafanikio makubwa upasuaji huo katika hospitali moja ya umma na alisisitiza sana kwamba wagonjwa wengine wasisumbuliwe katika hospitali hiyo ndio maana upasuaji ulifanyika mapema asubuhi.
 
< Nyuma   Mbele >

^