Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Viongozi wa Nchi na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
08/09/2014
Officials and Military Commanders Visit Supreme Leader in HospitalViongozi wa ngazi mbali mbali wa Iran wameendelea kumtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu.

Leo asubuhi, Dk Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Ayatullah Hashemi Shahroudi, Mkuu wa Baraza Kuu la Kutatua Hitilafu za Mihimili Mikuu, Bw. Jahangiri, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk Mahmoud Ahmadinejad, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislamu, Bw. Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran pamoja na makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa vikosi vya ulinzi na viongozi wengine mbali mbali wa Iran wamekwenda katika hospitali alikolazwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumjulia hali.

Vile vile Daktari Hashemi, Waziri wa Afya wa Iran amefika hospitalini hapo na kuona kwa karibu maendeleo ya matatibabu anayoendelea kupatiwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 
< Nyuma   Mbele >

^