Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq Amtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
09/09/2014
 Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Ammar Hakim, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq, leo jioni (Jumanne) amekwenda hospitalini kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu.
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq ameelezea kufurahishwa kwake na hali nzuri aliyomkuta nayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe afya kamili haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Ayatullah Javad Amouli, mmoja wa wanavyuoni wakubwa wa Kiislamu, leo jioni naye amekwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuombea dua za kheri, uzima na afya njema.
 
< Nyuma   Mbele >

^