Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Viongozi na Maafisa wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
09/09/2014
 Jioni ya leo (Jumanne) viongozi kadhaa pamoja na maafisa mbali mbali wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu wamekwenda hospitalini kumjulia hali Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Naibu wa Kwanza wa Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na mkuu wa Mahakama Kuu nchini, Mwanasheria Mkuu na viongozi wengine wa Chombo cha Mahakama, na vile vile wajumbe kadhaa wa Halmashauri Kuu ya Kuainisha Maslahi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni na Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu na wakuu kadhaa wa kamati mbali mbali za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran), Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB pamoja na manaibu na wasaidizi wake wamekwenda hospitalini hapo kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuombea dua za ahueni ya haraka.
Aidha shakhsia wengine mbali mbali akiwemo Mfawidhi wa Haram ya Bibi Maasuma (SA) ya mjini Qum, wakuu wa baadhi ya taasisi za Mapinduzi ya Kiislamu, Katibu wa Baraza Kuu la Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) na mudir wa Hawza pamoja na walimu mbali mbali na maulamaa wa Hawza za Qum, mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Jamiatul Mustafa, Mkuu wa Huduma za Hawza, Wawakilishi wa Fakihi Mtawala Mikoani na katika taasisi mbali mbali za Kiislamu pamoja na viongozi wengineo na vile vile wawakilishi wa Maayatullah Udhma Sistani, Shirazi na Zanjani, ni miongoni mwa shakhsia ambao leo wamekwenda hospitalini kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ikiwa ni siku ya pili tangu alipolazwa hapo jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) katika hospitali moja ya umma nchini.
 
< Nyuma   Mbele >

^