Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Maulamaa wa Ulimwengu wa Kiislamu Wamtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Hospitalini Chapa
10/09/2014
 Shakhsia kadhaa walioshiriki katika Kongamano la Maulamaa wa Kiislamu katika Kuunga Mkono Muqawama wa Palestina, wamekwenda hospitalini ili kumjulia hali Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate).
Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amemwakilisha Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah na kuwasilisha salamu za Katibu Mkuu huyo wa Hizbullah kwa Kiongozi Muadhamu akimuombea dua za afya njema na umri mrefu uliojaa baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Shakhsia na maulamaa wengine waliokwenda kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni pamoja na Allama Sayyid Sajid Naqavi, mmoja wa maulamaa wa Pakistan, Ayatullah Asef Muhsini, mmoja wa maulamaa wakubwa wa Afghanistan, Sheikh Sadruddin Qopanchi, Imam wa Ijumaa wa mji mtakatifu wa Najaf huko Iraq, Sayyid Ali Fadhlullah, mmoja wa maulamaa wa Lebanon, Bw. Ahmad Sambi, Rais Mstaafu wa visiwa vya Comoro na Sheikh Ahmad az Zeyn, Mkuu wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu ya Lebanon.
Shakhsia na maulamaa wengine wa kigeni waliomtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali ni pamoja na Sheikh Abdul Naser al Jabari, Mkuu wa Chuo Kikuu cha ad Da'awa na mmoja wa maulamaa wa Lebanon, Sheikh Abdul Ghani Shamsuddin, Katibu Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kusini Mashariki mwa Asia, Sheikh Alauddin Za'atari, Makamu wa Mufti Mkuu wa Syria pamoja na Ozhan Asil Turk Mkuu wa chama cha Saadat cha Uturuki na kuelezea kuridhishwa kwao na hali nzuri waliyomkuta nayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuomba Allah amzidishie afya njema na ampe uzima kamili wa haraka.
 
< Nyuma   Mbele >

^