Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ayatullah Misbah Yazdi, Ayatullah Gerami Qomi Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
10/09/2014
 Ayatollah Javadi Amoli and Ayatollah Kharrazi Visit Supreme Leader in HospitalLeo Jumatano ambayo ni siku ya tatu ya tangu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei alipolazwa katika hospitali moja ya umma alikofanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate), shakhsia na viongozi mbali mbali nchini Iran wameendelea kwenda hospitalini hapo kumjulia hali.
Ayatullah Misbah Yazdi na Ayatullah Gerami Qomi leo wamekwenda kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe uzima kamili wa haraka.
Vile vile Meya wa jiji la Tehran, Mkuu wa Baraza la Mji wa Tehran, mawaziri mbali mbali wa serikali pamoja na wanachuoni kadhaa na wataalamu wa sheria wa baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) mkoani Golestan na baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na shakhsia na viongozi wengine wa Jamhuri ya Kiislamu katika sekta tofauti, nao wamefika hospitalini hapo alipolazwa Kiongozi Muadhamu na kumuombea dua ya umri mrefu uliojaa baraka na kupata ahueni ya haraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
 
< Nyuma   Mbele >

^