Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Maayatullah Udhma Hamedani na Alavi Gorgani Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hosptalini Chapa
11/09/2014
 Maayatullah Udhma Noori Hamedani na Alavi Gorgani wamekwenda hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ikiwa ni siku ya nne tangu alazwe katika hospitali ya umma baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu.
Maayatullah Udhma Noori Hamedani na Alavi Gorgani wamemuombea dua Kiongozi Muadhamu za ya kupata uzima wa haraka na afya nzuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Vile vile Ayatullah Rasti Kashani, Mwakilishi wa Ayatullah Vahid Khorasani pamoja na wawakilishi kadhaa wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) na maimamu wa Ijumaa wa mikoa mbali mbali ya Iran pamoja na mafudhalaa, maulamaa na walimu kadhaa wa Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) wamekwenda hospitalini kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuombea afya ya haraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Wengine waliokwenda hoptalini hapo kumjulia hali Kiongozi Muadhamu ni pamoja na mfawidhi wa haram tukufu ya Abdul Azim Hassani na shakhsia pamoja na viongozi wengine kadhaa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta tofauti, na wote wamemuomba Mwenyezi Mungu ampe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umri mrefu uliojaa baraka na afya kamili ya haraka.
 
< Nyuma   Mbele >

^